Makamanda Polisi Mikoa Arusha na Mbeya wateremshwa vyeo

hivi polisi kama hatekelezi matakwa ya chama wanamshusha cheo. Anyway the time will come when no more solution of that nature will work, citizens has decided, the system can never accomodate such decision.
 
Unajua wewe ni mbishi kuelewa falsafa hii, mbona iko wazi " demotion by promotion" wewe unajiona umepandishwa cheo lakini hata ukilala ukianza kutafakari eneo ulilopelekwa hakuna issue. Kwanza vyeo walivyokua navyo viliwafanya wajulikane sana na hali ya watanzania walikua wakiogopwa sana. Sasa huku walikopelekwa saa ngapi watajulikana. nani atawaogopa. Sanasana watakachokutana nacho ni shikamoo nyingi tu. Nakwataarifa yako wengi kati yao watakimbia tu.
Staki kubishana na wewe.

Sawa kabisa "Pomotion by Demotion and vise verse"
 
Yule rpc aliyesababisha matatizo makubwa huko arsha kwa ajili ya kujikomba hatimaye amehamishiwa kwenye kitengo kipya makao makuu ya polisi dsm. Nafasi yake imechukuliwa na rpc liberatus anayetokea manyara kuja hapo arusha. Ni matumaini kuwa liberatus kama jina lake lilivyo atakuwa liberal na kutenda haki

source: Magazeti mengi ya leo jumapili




..bola ayekuepo huyo Liberatus ndo kaletwa amalizie kazi yenu,kuua kwake ni kitu cha kawaida jaribuni kufuatilia alikopitia utapata jibu,usimsifie m2 ambaye umjui tuulize sisi huyu ni noma, haya maneno yangu utayakumbuka siku moja
 
tehe tehe tehee. Kweli siku hizi polisi wanashindana na lundenga!
Tatizo ni kwamba hivi viwp havifananii na upolisi ukikutana navyo mitaani. Vinajirusha clubs kwa kwenda mbele na vinavaa nguo za ajabu ajabu kiasi ambacho huwezi kujua kama jeshi la polisi lina nidhamu ya mavazi!

kuna ki wp kimoja nilikiona kimebenua sketi tupaja tuzuri nikakitamani....yaani kidogo kiharibu mambo kwa ku kitizama tu!
 
..bola ayekuepo huyo liberatus ndo kaletwa amalizie kazi yenu,kuua kwake ni kitu cha kawaida jaribuni kufuatilia alikopitia utapata jibu,usimsifie m2 ambaye umjui tuulize sisi huyu ni noma, haya maneno yangu utayakumbuka siku moja

ukiua kwa upanga na wewe utakufa kwa upanga ......ajihoji!
 
Yeah ni lazima police force ifanyiwe marekebisho.polisi wetu wanatia huruma ila na wao wanajisahau kama wanapigika kama raia wengine.Niliwaambia polisi Geita kwamba wasikubali kutumiwa na mabosi wao vibaya.Waige mfano wa wenzao Misri

Niliwaambia waone haya kutumiwa na wakubwa zao vibaya kuumiza watanzania wenzao huku wao waki-share bunduki na risasi(vitendea kazi).the guys are hustling for real....

Kuna tatizo kubwa zaidi ambalo halipaswi kurukwa. Kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma, uhuru wa kweli wa kitaaluma kazini Tanzania ni kama haupo. Tena mahali penye maslahi ya kifedha au kisiasa usitegemee ukiwa Waziri, NW, KM, DG, n.k. kama utaachiwa utumie kanuni na mantiki za taaluma yako. Yatatoka maagizo toka juu (HQ, Ikulu, n.k.) kuhusu hatua gani wakulu wanataka uchukue. Nani apewe tenda, nani atimuliwe, nani afunguliwe kesi .... Ikija kwa majeshi ndio kabisaa.

Kwa hali hiyo, tatizo kubwa si la kitaaluma bali ni mfumo wetu wa kuendesha nchi kama kijiwe cha wateule fulani wenye madaraka ya uhai au kifo kwa wenzao. Kama kweli mtoto wa Rais naye anaweza kutoa amri/maagizo kwa watendaji na yakatekelezwa kama ilivyosemwa kwenye post moja hapa, tutegemee nini hata tukiwa na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha kwenye kazi zao? Kwa hali ilivyo sasa, mabosi wa Polisi kama akina Andengenye wana machaguo mawili tu; ama kujikomba waendelee kudumu kazini hata kwa kudharauliwa au kujiuzulu wakabangaize na wananchi wenzao mitaani.

Jawabu pekee ni kujenga mfumo wa majeshi huru na imara yasiyoweza kuingiliwa kirahisi na wanasiasa au matajiri wasio na maadili. Hilo ndilo changamoto kuu la wanamageuzi wa kweli nchini. Kupambana na individual police officers katika mfumo tulio nao haitupi jawabu la uhakika kwa tatizo hili. Ni kama kubadilisha mawaziri kulikofanyika hivi punde ilhali inajulikana wengi walikuwa wanatumikia maslahi ya bosi wao wa Magogoni na washkaji zake wanaowatumia kama kete kwenye mchezo wa draft.
 
kama mtakumbuka, Arusha ilikuwa ikikamiwa na ACP Mpwapwa wakati Andengenyi akiwa masomoni uingreza kabla na baada ya uchaguzi mkuu, hivyo inawezekana ndo kuandaliwa kwenyewe. Ila the guy is very strict hata akiwa arround polisi wote wanamgwaya.
 
Kwa uelewa wangu mdogo cheo cha Mkuu wa Utawala na Rasilomali watu ktk Jeshi letu la Polisi siyo kikubwa kwa madaraka tu bali hata rushwa anayopokea mwenye hiki cheo ni kubwa kulinganisha na RPC wa mikoa! Huyu ni mungu mtu ktk jeshi la polisi! Nadhani amechukua nafasi ya kamishina Mtweve kama sikosei. Acheni mchezo na hiyo nafasi!
 
Back
Top Bottom