Makalio ya kichina yananitesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makalio ya kichina yananitesa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jan 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td align="left" bgcolor="#cccccc"><table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td class="news1">

  </td> <td class="news1" align="right" width="150">
  </td> </tr> </tbody></table></td> </tr> <tr> <td bgcolor="#999999">[​IMG]</td> </tr> <tr> <td class="morenews" align="left" bgcolor="#f3f3f3" valign="top"><!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Juanita, aliyasema hayo alipokutana na waandishi wetu, Kariakoo, Mchikichini, Dar es Salaam, alipokwenda kufanya ‘shopping’ ya vitu vyake binafsi.

  Alisema, makalio yake yanampa mateso makubwa, kwani mara kwa mara amejitahidi kuyapunguza lakini hakuna mafanikio yoyote ambayo ameyapata mpaka sasa.

  “Jamani haya si makalio yangu, ni ya kichina,” alisema Juanita huku akitoa machozi na kuongeza: “Sijui ni lini Mungu atanisaidia kuondokana na mateso haya.”

  Juanita aliendelea kusema: “Wakati mwingine nashindwa kutembea barabarani, kila nikionekana machoni kwa watu naonekana kituko, watu wananishangaa na kunizomea.

  “Fikirieni wenyewe haya ni mateso kiasi gani, sina raha lakini nimeyataka mwenyewe. Nimejitahidi kutumia dawa kupunguza hayapunguziki.”

  Akiongea ‘in & out’ juu ya ishu yake, Juanita alisema, alishawishika kuanza kutumia dawa za Kichina ili kukuza makalio baada ya kuanza kuchekwa na wenzake mtaani kuwa ni kimbaumbau na hana wowowo.

  Alisema, kutokana hali ya kuchekwa mara kwa mara, aliona ni vema afanye juu chini ili kuitengeneza heshima yake, ndipo alipoamua kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za “kuumua makalio” ambazo zimemfikisha alipo sasa.

  “Nilianza kutumia mwaka juzi, mabadiliko yakawa ya ghafla, mtaani watu wakawa wananipongeza kuwa nina shepu nzuri, hipsi safi lakini haikuishia hapo, makalio yangu yaliongezeka kila siku.

  “Mwaka jana ilikuwa hatari, nikaanza kujiona ni binadamu wa peke yangu, nikawa naona aibu lakini kuna siku mtu aliniletea picha ya yule mshiriki wa Maisha Plus, Efrancya Mangi, nikaambiwa naye anatumia.

  “Aliyeniletea hiyo picha aliniambia, Juanita usidhani upo peke yako, akaongeza, mbona Efrancya naye anatumia dawa za kichina lakini yupo kawaida na umbo lake ni kubwa kuliko langu? Nilimkubalia na kujiona kumbe mimi si wa ajabu,” alisema Juanita.

  Aliongeza: “Baadaye nikapigwa na butwaa baada ya kusoma habari gazetini kuwa Efrancya yeye makalio yake si ya kichina, bali ni umbo lake halisi, kwa kweli kuanzia hapo niliumia sana na kila siku naona yanakua kiasi ambacho kama mnavyoniona, hata huyo Efrancya ni cha mtoto.”

  Kuhusu mtindo wake wa maisha kwa sasa, Juanita alisema kuwa analazimika kupunguza pirika za maisha kwa sababu mitaani watu wakimuona wanamzomea hasa akipita Kariakoo.

  Alisema, maisha yake ni magumu lakini hulazimika akiwa na safari akodi taksi kwa sababu akipanda daladala watu huacha mazungumzo yanayowahusu na kumjadili yeye waziwazi kitu ambacho alikielezea kwamba huwa kinamuuma.

  “Hata nyumbani mimi naonekana mtu mzima wakati ni mdogo, wazazi wangu wanajitahidi kunifanya niwe na furaha lakini uwezo wao ni mdogo, ila pamoja na umbo langu lakini ni mwepesi mpaka huwa najishangaa,” alisema Juanita.

  Alipoulizwa dawa hizo za kichina alinunua hapa Bongo kwa nani, kati ya Maimartha Jesse au Khadija Shaibu ‘Dida’ ambao wamekuwa wakihusishwa na biashara hiyo, Juanita alijibu kuwa hajanunua kwao, isipokuwa aliletewa na rafiki yake kutoka China.

  “Huyo rafiki yangu huwa anaziuza Morogoro, sasa alikuwa ananiletea na zilifanya kazi haraka, lakini za kupunguza zimeshindwa, hivi sasa ameniahidi akienda tena anatinunulia,” alisema Juanita.

  Awali, waandishi wetu wakiwa ‘bize’ katika misele yao ya kipaparazi, walimuona Juanita akitoka ndani ya taksi na kuingia kwenye duka moja, linalouza vifaa mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani, Kariakoo.

  Mapaparazi wa Ijumaa, walishtushwa na kelele za Wamachinga, waliokuwa wakizomea na kupiga miluzi, hivyo kugeuka na kumshuhudia Juanita akijitahidi kutembea kwa aibu kabla ya kumfuata na kufanya naye mahojiano.

  Huko nyuma, mwandishi wa gazeti hili amewahi kuzungumza na Efrancya ambaye alisema kuwa makalio yake ni ya kawaida, kwani familia yao yote ipo hivyo.

  “Hata mama yangu yupo hivi, najua kuna watu wanaamini mimi natumia dawa za kichina lakini siyo kweli,” alisema Efrancya.
  Kilio cha Juanita na makalio ya kichina, kinakuja baada ya miezi miwili iliyopita kutokea kifo cha Miss Argentina 1994, Solange Magnano aliyefariki dunia alipokuwa akifanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio.

  Solange, 38, alifariki baada ya kukumbwa na tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu (pulmonary embolism) akiwa kwenye hospitali moja iliyopo jijini Buenos Aires, Argentina.

  Mbali na tukio hilo, lipo lingine la dada mmoja tuliyemnasa kwa jina moja la Semala, anayeishi Keko Magurumbasi, Dar ambaye anahaha kupunguza tumbo lake ambalo linakua kila siku.

  Habari kutoka kwa mtu wake wa karibu zinasema kuwa Semala alitumia dawa za kuongeza tumbo matokeo yake kuzidi kipimo alichokihitaji, hivyo kuwa kubwa zaidi.

  “Ni kubwa sana, anatumia dawa za kupunguza wapi,” alisema mtoa habari wetu.
  Maimartha na Dida, kwa muda mrefu wamekuwa wakituhumiwa kuuza dawa za kichina za kuongea au kupunguza maumbile, ingawa muda wote wamekuwa wakikanusha.

  Watangazaji hao wenye majina makubwa, wamewahi pia kukaguliwa na maafisa wa serikali, kutoka mamlaka zinazohusika lakini hakuna dawa ya kichina wala harufu yake iliyokutwa kwenye maduka yao.

  Gazeti hili linawaasa warembo kujihadhari na matumizi ya dawa ambazo hazijapitishwa kitaalamu, kwani zimebainika kuwa na athari hasi kubwa kuliko chanya. Ni vema wakajiamini na kujikubali kulingana na jinsi Mungu alivyowaumba, kwani kinyume chake ni kuchukua uamuzi mbaya ambao baadaye unageuka ni mateso. Mhariri.
  http://www.globalpublisherstz.com/2008/06/17/kumbukumbu_ya_bongo.html


  </td></tr></tbody></table>
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! ukitaka uzuri sharti udhurike! hii inatisha! duh! Wo wo wo linaumuka kama limetiwa hamira! Makubwa haya!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  maneno safi sana haya..mkuu kumbe umo katika mambo ya scriptures
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  hawa watu wanautani; makalio ya kichina? nionesheni mchina mwenye makalio kama haya! Dunia nzima ukitaka kuwa na makalio kama hayo ni lazima uwe na damu ya kiafrika.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiongozi wanazungumzia madawa ya kichina ya kuongeza hayo maungo..ambayo dada zetu wameyafakamia ;)
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mazee,

  Scriptures are full of philosophy. Philosophy & Natural Sciences are my main interests, sometimes I feel like my 24hrs a day are not enough for me to explore and educate myself on this stuff.
   
 8. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  safi sana dada, zidisha zaidi dawa za kuumua ******, mbona bado hayajaumuka hayo? vitako vidogo kama hivyo rafiki yangu unaanza kulalamika?
  mwambie rafiki yako wa china aje na zile toleo jipya, hizo zinakuza ****** within a fraction of a second!! try that one!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280

  Nafahamu.. ndio maana nasema kama hizo dawa zipo kwanini wao Wachina wenyewe wasiwe na makalio ya kufuru?
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda wao haziwaumui..:D
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  njoo kwangu mama, mimi sibagui...yawe ya kichina, ya kizaramo twende kazi...
   
 12. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  kama ndio wife inamtokea kitu kama hicho, sharti arudi kwao
   
 13. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Amuone daktari wa kichina pia, vinginevyo nani alaumiwe? Hayo yote yameletwa na tamaa zake, labda amtafute mwanamme mwenye tochi ya kichina, nadhani wataendana.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Huyu ni obese case mbona mpaka usu mikono imejazana au navyo alivipaka hiyo hamira?Apunguze kula ovyo
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Utakoma kumrekebisha muumbaji
   
 16. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mbona kama anayafurahia haonyeshi huzuni yeyote ile tena katabasamu vzr sana mmmh
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  kweli aliyesema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hapo juu hajakosea mmh
  Mbona hatuliziki na tulivyoumbwa
   
 18. k

  kamaghe Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanakunywa hizo dawa kwa sababu hawajiamini na maumbo yao
   
 19. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yaani kuna watu wa ajabu sana. Kwa nini uamini dawa ya kukufanya unenepe hivyo? Hawajui inaweza kuwaletea athari nyingine mbaya katika miili yao? Hivi ni kitu gani kinawafanya wawe na maamuzi kama haya? Elimu ndogo, kutaka kupendwa zaidi na wanaume, kuwa mrembo au kutokuwa na kitu kingine tena katika maisha cha kufanya?
   
 20. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ukubwa wa puto kiboko yake mwiba....aje kwangu huyo gwaride lake lazima atakonda bila dawa.
   
Loading...