CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,984
- 4,083
Rank | Country | Debt amount |
---|---|---|
1. | Egypt | $11,968,321,674 |
2. | Angola | $3,153,816,667 |
3. | South Africa | $2,669,800,000 |
4. | Côte d'Ivoire | $2,117,559,620 |
5. | Kenya | $2,058,982,100 |
6. | Nigeria | $1,840,875,000 |
7. | Ghana | $1,644,377,000 |
8. | Morocco | $1,499,800,000 |
9 | Democratic Republic of Congo | $1,294,500,000 |
.10. | Tunisia | $1,259,139,338 |
======
Hii ndio orodha ya nchi 10 za Africa zenye deni kubwa zaidi huko Shirika la Fedha Duniani ( IMF )
Kwa msiofahamu, Nchi Tisa kati ya kumi ndio nchi zinazoshikilia uchumi wote wa Africa,
Hawa ndio magwiji wa kuchota Fedha za IMF kutoka bara la Africa tena kwa riba kiduchu ambayo ni chini ya asilimia moja tena kwa muda wa miaka 15.
Ukiangalia katika orodha ya nchi tajiri kabisa barani Africa utakuta ni hawahawa magwiji wa uchotaji wa maokoto huko IMF.
Hoja yangu Leo, Nikwanini Tanzania yenye kauchumi kiduchu inaogopa kukopa wakati ,hawa makabaila na Matajiri wa kupindukia kama Misri, Nigeria, Morocco, Ghana, South Africa mababa wa uchumi Africa wanakopa kwa kasi kiasi hiki, Why Tanzania tunakwama wapi?
Nchi yetu ya Tanzania kwa kiasi kikubwa inamazezeta ambayo yanawatisha Watanzania wenzao kwamba kukopa dhambi tena ishara ya kufilisika kwa nchi kumbe wanataka kuwafanya Watanzania waendelee kuutamia umasikini wao.
Ombi langu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba ongezeni kasi ya kukopa ila tu mkope IMF sio maeneo mangeni ili kuepuka riba kubwa.
Nasisitiza Leo, Tanzania tukopeni zaidi ili kujenga miradi yenye output ili na sisi GDP ya nchi yetu na yenyewe ipande kama ile ya EGYPT pamoja na kuwa kinara wa madeni IMF bado ndio nchi tajiri barani Africa.
Kazi iendelee.