Makaka wasomi na dada msomi walivyojinadi jana huko Arusha

Makaka wasomi na dada msomi walivyojinadi jana huko Arusha

Sasa ninakuruhusu nenda kwenye toviti ya NBAA akirudi ndipo tutaelewana.

Unayeongea naye ni Muhasibu qualified Accountant ninaelewa ninachokueleza.Otherwise hakuna haja ya kuisotea CPA

CPA(T) Maana yake Certified Public Accountant of Tanzania certificate hii ndiyo inayokufanya Muhasibu uwe Muhasibu.Anayejiita Muhasibu akawa hana hii certificate ni sawa na Lawyer asiye kuwa na Cheti cha kupractice/advocate.

Pole ndiyo wenyewe tunavyoelewana.Ukimkuta anayejiita Accountant halafu hana CPA anajifurahisha tu lakini kwetu bado hajaqualify kuwa Muhasibu.

Bahati mbaya sana kama mhasibu hujui tofauti iliyopo dah pole sana mkuu. Bado hujaiva kwenye fani ya uhasibu. Sasa kwa mfano unaposema wewe ni qualified accountant una maana gani hasa? hahahahaha.

Kwa ishu ya lawyer na advocate ndo hapo napo nimeona kumbe una uelewa mdogo sana kwenye hizi mambo!

You are still young, keep learning dogo!
 
Kuna profession mbili tu dunia nzima Mkuu.
a)LEGAL PROFESSION na
b)UDAKTARI

Course zingine hizo hazina sifa ya PROFESSION hata kidogo.
Hehehehehe kukariri kuna shida sana mazee.....so, mambo ya rocket science unayachukuliaje kwa mfano? nimekutukana kwa hasira.....!!!!
 
Masha mkali eeh😀

Ila umesikia alivyochapia?

Kasema "I have decided to make a decision".

How can you decide to make a decision?

Is it possible?
Yeah in Swahili umeamua kufanya maamuzi............ Yuko vizuri jamaa ktk lugha
 
Masha mkali eeh😀

Ila umesikia alivyochapia?

Kasema "I have decided to make a decision".

How can you decide to make a decision?

Is it possible?
"Nimeamua kufanya Maamuzi"
Put this in English
 
"Nimeamua kufanya Maamuzi"
Put this in English

Ndo matatizo ya kufikiri kwa Kiswahili na kujaribu kuongea kwa Kiingereza ukidhani utakuwa unaleta maana ile ile kumbe unaharibu lugha ya watu.
 
Ndo matatizo ya kufikiri kwa Kiswahili na kujaribu kuongea kwa Kiingereza ukidhani utakuwa unaleta maana ile ile kumbe unaharibu lugha ya watu.
Usitake kujifanya unajua sana wewe Bwege.
Iweke hii sentensi kwa Kiingereza

"Nimeamua kufanya Maamuzi"
 
Usitake kujifanya unajua sana wewe Bwege.

Hasira za nini wee bwanaaa...

Sijifanyi najua. Ni kwamba ninajua.

Wewe siyo wa kubishana na mimi kuhusu usahihi wa sarufi na sintaksi za lugha ya Kiingereza.

Hunifkii hata kidogo.

Iweke hii sentensi kwa Kiingereza

Sawa

"Nimeamua kufanya Maamuzi"

"I have made a decision" [is grammatically, syntactically, and logically sound].
 
Ukisoma IT halafu ikawa ulichosoma chuo ndo hicho hicho lazima uwe nyuma ya wakati tena pengine kuliko huyo wakili!

But all in all, hapa ni suala la wakili... ukiniambia kuna wakili msomi ina maana kuna wakili asiye msomi vile vile!! Hapa ndipo ningependa kufahamu huyo wakili asiye msomi anakuaje?!
Sasa anayofanya Mwakyembe huoni anafaa kuwa mfano Wa yule asiye msomi. Unaandika thesis anaikana, anatishia kufuta chama ambacho yeye ni mwanachama, anatoa amri kwamba hatà wale ma bushmen wasandawe wásioane mpaka wawe na vyeti vya kuzaliwa. Yaani watu wanajitahidi kuwa mbali na huduma za kisasa yeye analeta longolongo. Isingekuwa raid kitengua kauli hiyo jamii ingekwisha. Waweza kusema hapo kuna mwanasheria msomi?
 
Hawa jamaa wanapenda sana kujiita wasomi...

Sio mbaya... ila kwa usomi huu ambao bosi wao anapiga marufuku ndoa bila ya cheti cha kuzaliwa... Hapana asee...

Kwa wakristo kwa mfano ndoa inakuwa ndoa halali baada ya kufungishwa na padre/mchungaji. Suala la kupewa vyeti (vya serikali) hufanyika baada ya ndoa kufungwa... mwisho kabisa wa ibada. Hii inamaanisha cheti hutolekwa kwa hitaji la serikali lakini ndoa kama ndoa kiimani haihitaji cheti.

Ni heri kusomea Kemia ukajua kuitafsiri sheria kuliko kuwa mwanasheria afu ukashindwa kuijua sheria.
Wala huyo c boss wetu ni karagosi tu
 
DAHHH WASOMI WA KIBONGO BWANA NI VILAZA KINOMA, MASKINI KISWAHILI CHENYEWE TU KINAWAPIGA CHENGA, HALAFU WANAVAMIA LUGHA ZA WATU YAANI NI KICHEKESHO! JAMANI KUNA POLICE PRISON? HALAFU YULE MWENGINE NAE AMEDICIDE TO MAKE DECISIONS? KUJUA KIINGEREZA SIO DALILI YA USOMI WALA KUONGEA KISWAHILI HAINA MAANA HUJASOMA HIYO TAALUMA YAKO!
NI USHAMBA ULIOPITILIZA ETI KIKAO CHA WANAOJIITA WASOMI, KUTOKA TANZANIA, HALAFU LUGHA YA MAWASILIANO ETI NI KIINGEREZA?
SWALI HIVI MNAMDANGANYA NANI KUWA NYIE MNAJUA KIINGEREZA KULIKO KISWAHILI?
CCM BADO ITATAWALA TANZANIA KWA MIAKA 200 IJAYO DAHHHHH
 
Masha mkali eeh😀

Ila umesikia alivyochapia?

Kasema "I have decided to make a decision".

How can you decide to make a decision?

Is it possible?
Hapo aliongea lugha ya kiswahili kwa lugha ya kiingereza " nimeamua kuchukua/kufanya maamuzi..."
 
Huyo wa mwisho atakuwa alisoma koromije au ukanda huo huo, lugha ya mama huwa haipandi!
 
Ndo matatizo ya kufikiri kwa Kiswahili na kujaribu kuongea kwa Kiingereza ukidhani utakuwa unaleta maana ile ile kumbe unaharibu lugha ya watu.

..kwa maoni yangu wote wamezungumza chini ya viwango.

..tena haijalishi walizungumza kiingereza au kiswahili.

..nadhani waTz hatuna communication skills. Sikutegemea mawakili wasomi washindwe kujieleza/kujinadi kama inavyothibitika ktk video hapo juu.
 
Back
Top Bottom