Yaani kutokana na maelezo yako ndiyo maisha yangu yanavyokwenda. Mimi ni Mkrito na ninasali kawaida, mambo yangu mengi Mungu ananionyesha kwenye ndoto, ninaweza kuomba kazi, interview nikaota niko kwenye interview na maswali nitajibu na nitapata kazi, sasa nikiamka inabidi niandike maswali kwenye diary yangu, baada ya miaezi sita au mwaka ni kweli nitaomba kazi na interviwer sura itakuwa familiar baadae ndiyo ninakumbuka niliota hii ndoto.
Kazi yangu ya sasa inamajukumu ya kusafiri sana, ninapofika sehemu mpya nitakumbuka hii sehemu nilishafika, na ninakumbuka njia nilizopita, lakini baadae ndiyo ninakumbuka niliota.
Ni zawadi Mungu aliyonipa na inanisaidia sana.