Mtu asikudanganye, dunia hii ina pande mbili ulimwengu tunauona na ule tunauhisi/ hatuuoni. lakini hizi zote zinafanya kazi kwa kutegemeana, mambo yote yanaanza kufanyika kwenye ulimwengu tusiouna kwanza halafu matokeo yake ndiyo tunayaona mwilini, yaani phyisical world. mtu akipata kitu alikipata kizuri au kibaya, kilikuwepo rohoni kwanza ndipo kikaja mwili.
Wapo wanaoona mambo haya, wachawi waganga wa kienyeji, watakatifu, baadhi ya viongozi wa dini zenye muunganiko wa kweli na Mungu wanaona.Hivyo ndiyo maana ni rahisi kumwambia mtu fanya hivi au hivi utashinda. mfano anayesema chumvi na mfupa wakitimoto alipata wapi hayo maneno? lazima aliambiawa na waona fahamu eimu hii. ni elimu njema kuijua maana ndiyo chimbuko la kufanikiwa kwetu.
Mtu akikwambia uongo mambo haya hayapo. either yeye anafaidika na upande huo na hataki wewe ujue ili usimpinge, au hajui kwa maana ni kipofu au anatumiwa aseme hivyo ili usifahamu. Kwa kawaidaa binadamu akifahamu kitu ukombozi unakaribia maana ataanza kupambani ili atoke, hivyo anayefaidika na ujinga wako hatapenda ujue ukweli.
Ndoto ni kigezo kikubwa cha kujua upande ulioko, kama unaota mabaya tu ujue jambo baya lipo upenuni linakuja, na kama unaota mema, ujue pia jambo jema lipo upenuni linakuja pia. ukiwa na maarifa unaweza kuyapinga mabaya na yasije, na ukiwa na maarifa unaweza kuyaita mema na yakaja.
Hivyo ni vyema sana kutafuta nafsi na kujifunza juu ya jambo hili kwani ndimo ufanisi wa ubinadamu ulimo. Kuna watu wamejaliwa kabisa wanaona mambo haya, japo inaweza kuwa kwa kipindi fulani kisha uwezo unapotea kulingana na alivyo jipanda na source ya uwezo huo.