Makafara katika ujenzi wa magorofa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,848
730,361
Ni jambo la kificho mno, lisilojulikana na wengine wengi lakini ukweli ni kwamba magorofa mengi uyaonayo yana roho za watu au imevunja mifupa ya watu kwa njia za ajali au yamekunywa damu ya kikafara
Si mara zote wafanyao mambo haya ni wamiliki la hasha bali mambo haya hufanywa pia na wakandarasi na hata waliopewa tenda mbali mbali kwenye site husika... Nia na lengo ni moja tuu kupata zaidi au kujikinga kishirikina
Kama tungekuwa na takwimu za kitaifa si ajabu kati ya kila magorofa kumi saba yamesababisha maafa vilema na makovu... Hili jambo lina level zake kuanzia kutoa kafara dogo la mtu mmoja mpaka ibada za makafara zifanywazo na makandarasi wakubwa kufikia viwango vya freemason
Ndio maana kwenye ujenzi wa mahekalu makubwa ya ibada hufanyika ibada maalum za kumwomba Mungu aepushe mbali mabaya yote kwenye ujenzi husika mpaka mwisho wa ujenzi wake.
Hata wewe kwa kutambua hili fanya hivyo kwenye ujenzi wako hata kama si ghorofa ili nyumba yako isije kuwa ni chanzo cha mabalaa na mitihani ya dunia
 
Mimi yalinikuta hayo nilinunua site nilijenga fasta baada ya miezi 3 nikahamia, yaliyonikuta Mungu ndo anaejua. Kiukweli Nyumbani imenishinda nimeiacha ni majanga mpk Leo sijakaa Sawa.
 
mkuu mshana Jr kafara ya kufukia kuku ina uzito kiasi gani, naomba nipe maarifa hapa, yaan mtu kafukia kuku mahali kama zindiko vile
 
Mshana jr, kwa vile nilikosea na kwakua sikujua Kabla nitafanyaje? Ili Mambo yaeNDE kama yalivokua?
 
Mimi yalinikuta hayo nilinunua site nilijenga fasta baada ya miezi 3 nikahamia, yaliyonikuta Mungu ndo anaejua. Kiukweli Nyumbani imenishinda nimeiacha ni majanga mpk Leo sijakaa Sawa.

Dawa pekee hapo ni kuita watumishi wa kuaminika washushe maombi
 
majanga gani yalikukuta mkuu??

Mengi, nilikosekana na ajali kama Mara 4,mpk siku moja nikapata ajali mbaya Kuna gari ikapanda juu ya gari yangu. tulikua tunalala mke wangu anakuta kitanda kila siku kinacheza, Kuna siKu Kuna mtu aliingia ndani akawa anataka kumuingiza Mtoto wangu kitu mke wangu akagimbana nae sana usingizini, asubuhi tunaamka mtoto amefanya mstari mweusi kwenye kifua.

Mbali ya hayo nilianza kuuza gari,niliuza kiwanja,niliuza duka, niliuza kila kitu.

Nikishtuka nilijua tayari Kuna Mambo siyaelewi na chanzo ni kuhamia Iyo sehemu mpk Leo bado naungaunga.
 
Duh!kumbeeee

Kuna baadhi ya nyakati mmiliki mjenzi/mkandarasi na hata mafundi hawana tatizo bali tatizo linakuwa ni kipande chenyewe cha ardhi... Pengine hapo kilikuwepo kilinge cha wachawi au Pengine palifanyiwa kitu kibaya cha kishirikina au Pengine kuna watu walishawahi kufa au kuawawa hapo na roho zao zikabaki hapo zikisubiri kisasi
 
sasa mkuu mshana kwa hiyo niende nikafukue hapo alipofukia halafu ndio niweke chumvi na fupa la kitimoto au?me nataka jamaa wasiweke tena mauchafu yao kabisa, walipofukia napajua
 
Mimi yalinikuta hayo nilinunua site nilijenga fasta baada ya miezi 3 nikahamia, yaliyonikuta Mungu ndo anaejua. Kiukweli Nyumbani imenishinda nimeiacha ni majanga mpk Leo sijakaa Sawa.
Ilikuwaje mkuu tupe feedback kidogo?je ulihama moja kwa moja
 
sasa mkuu mshana kwa hiyo niende nikafukue hapo alipofukia halafu ndio niweke chumvi na fupa la kitimoto au?me nataka jamaa wasiweke tena mauchafu yao kabisa, walipofukia napajua

Mwaga mkojo kwanza kisha fukua ukiwa umegeuza ndala au viatu halafu malizia kwa kumwaga chumvi kisha fukia mfupa
 
Back
Top Bottom