Makabila yanayoongoza katika Afrika Mashariki kwa kuwa na mazingira bora ya asili ya uzalishaji vyakula

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_2827.JPG


Tangu zamani za kale, mwanadamu alitegemea neema ya asili ya mazingira ya eneo husika kujipatia mahitaji yake muhimu hasa chakula na makazi. Kuna baadhi ya maeneo yalijaliwa kuwa na:
  1. Mvua na maji ya kutosha kwa mwaka mzima,
  2. Joto la kadri (unscorching sunrays) lisiloathiri nishati (nguvu) mwilini,
  3. Wanyama wa mwituni na wa kufuga wa kutosha, hasa ng'ombe, mbuzi, kuku na bata.
  4. Maziwa, mito na ghuba za bahari zenye samaki wa kutosha,
  5. Udongo wenye rutuba, kwa ajili ya kurutubisha mazao, majani na vyakula vya samaki
  6. Kutokuwepo kwa magonjwa hatari: malaria, homa ya manjano (yellow fever), malale (trypanasomiasis/nagana/sleeping sickness), kichocho (schistosomiasis/bilharzia), hivyo jamii ya hapo inakuwa na afya njema.
Kadri vigezo hivi vinapokuwa vingi katika eneo dogo, ndivyo uwezo wa uzalishaji wa eneo husika unapoongezeka. Hali hii ya uzalishaji chakula cha kutosha kwa muda mrefu, ndiyo inapelekea vizazi na vizazi vinavyokulia maeneo hayo kuwa na afya nzuri na ya kutosha.

Ifuatayo ni orodha ya makabila yote 63 makubwa katika Afrika Mashariki, yenye wakazi zaidi ya 500,000 kwa kufuata ubora wa mazingira yake ya kijiografia katika uzalishaji mazao ya chakula.

Average
: A

1: Wanyakyusa (T)
2: Bakonjo (U)
3: Warundi (B)
4: Wahaya (T)
5: Batooro (U)
6: Wakikuyu (K)
7: Bagisu (U)
8: Wakisii (K)
9: Waluhya (K)
10: Wanyarwanda (R)
11: Baganda (U)
12: Waha (T)
13: Wajaluo (K)
14: Wakipsigis (K)
15: Wakurya (K)
16: Wachaga (T)
17: Wameru (K)
18: Banyankore (U)
19: Wakurya (T)
20: Wamasai (K)
21: Wanandi (K)
22: Wapokot (K)
23: Banyoro (U)
24: Wasambaa (T)
25: Waluguru (T)
26: Bakiga (U)
27: Basoga (U)

Average: B:
28: Wapare (T)
29: Wakamba (K)
30: Wambulu (T)
31: Waacholi (U)
32: Walango (U)
33: Walugbara (U)
34: Waalur (U)
35: Wabena (T)
36: Waiteso (U)
37: Bagwere (U)
38: Wahehe (T)
39: Banyole (U)
40: Wadama (U)
41: Wanyiha (T)
42: Wanyilamba (T)
43: Warufiji (T)
44: Wanyaturu (T)
45: Wagiriama (K)

Average: C:
46: Warangi (T)
47: Wamambwe-Lungu (T)
48: Wamasai (T)
49: Wasukuma (T)
50: Wazaramo (T)
51: Wagogo (T)
52: Wamwera (T)
53: Waaringa (U)
54: Wakaramojong (U)
55: Wanyamwezi (T)
56: Wazigua (T)

Average: D:
57: Waturkana (K)
58: Wagarre (K)
59: Wamakua (T)
60: Wasomali (K)
61: Wamakonde (T)
62: Wangindo (T)
63: Wayao (T)

NB:
  • Orodha hii ilichukua eneo dogo la kuwakilisha Kabila husika, hivyo unaweza kukuta Kabila lina alama za juu lakini halijulikani Afrika Mashariki kwa uzalishaji kutokana na kuwa na idadi ndogo ya wakazi (mf. Bakonjo) ama Kabila likapata alama ya wastani but kwa kuwa, lina watu wengi inasaidia kabila hilo kuwa na nguvu (mf. Wakamba). Hivyo kadri kabila linapopata watu wengi, wanafidia baadhi ya madhaifu.
  • Kuna baadhi ya makabila, yakiwemo Wamakonde, Wamakua na Wamwera, maeneo yao bora hayana tofauti kubwa na maeneo mengine ya makabila hayo kama ilivyo kwa baadhi ya makabila wakiwemo Wanyaturu, Wanyilamba, Wagogo, Warangi na Wamambwe-Lungu ambao wana maeneo madogo yenye hali nzuri ya hewa na rutuba lakini maeneo yao makubwa ni duni sana kiuzalishaji kuliko maeneo ya Umakonde ama Umakua, Umwera na Ungindo.
  • Licha ya Wamasai kuingiliana, nimeweka tofauti ya utaifa ili kusisitiza juu ya mazingira bora ya Wamasai nchini Kenya, kama ilivyo tofauti ya Wakurya pia.
  • Idadi kubwa ya makabila ya kitanzania imeangukia makundi C na D kutokana na kutokuwa na mazingira bora kulinganisha Wakenya waliotawala kundi A na Waganda waliotawala kundi B.
 

Attachments

  • IMG_2828.JPG
    IMG_2828.JPG
    408.2 KB · Views: 137
  • IMG_2832.JPG
    IMG_2832.JPG
    435.2 KB · Views: 140
Average: D:
57: Waturkana (K)
58: Wagarre (K)
59: Wamakua (T)
60: Wasomali (K)
61: Wamakonde (T)
62: Wangindo (T)
63: Wayao (T)
Makabila ya Tanzanzia yaliyopo kwenye kundi hili, ni kwasababu tu ya uvuvi. Ardhi yao inarutuba ya kutosha na mvua za kutosha mbaya sana maeneo yao yamebaki mapori tu. Hata kuzunguka nyumba yake ni mapori. Kwa kweli niite tu kuwa wamezubaa sana. JF wa makabila hayo wafanye kitu kuleta mabadiliko.
 
Back
Top Bottom