SoC03 Kwanini katika jamii ya wamasai hakuna watu wenye ulemavu? Serikali inatakiwa kufanya nini ili kukabiliana na jambo hili kupitia utawala bora

Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
Wamasai ni miongoni mwa makabila maarufu katika manila takribani 150 yanayopatikana nchi Tanzania katika kanda za mikoa ya kanda za juu kusini hususani mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, jamii ya kimasai ni jamii maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na sifa ya kipekee ya kutunza na kuhifadhi utamaduni wao wa mavazi, chakula, mazishi, desturi na mambo mengine kadha wa kadha.

Kupitia sifa hizi kusaidia Sana kuwavutia wageni na watalii mbalimbali kutoka nchi za nje Kama vile Australia, Itali, Germany, India, USA na nyingine kutembelea jamii za makabila haya ili kujifunza utamaduni wa watu wa jamii kutoka katika kabila la kimasai, hali hii imesaidia Sana kutangaza utamaduni wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, vile vile pato la nchi limekuwa likiongezeka kila mwaka Kupitia sekta ya utalii na utamaduni hapa nchini.

Kabila la watu wa kimasai limekuwa na mila na tamaduni ambazo ni tofauti na jamii zingine, katika utawala katila hili bado limekuwa na viongozi wake ambao wanamajukumu kwa jamii zao Kama vile Laiboni, ambao hawa kazi yao kubwa ni kutoa sheria na maagizo mbalimbali kwa wanajamii, lakini Morani nao ni vijana wa rika Kati ya 18 mpaka 25 kundi hili la wamasai wanajukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama katika jamii zao dhidi ya uvamizi wa wanyama wakali na maadui zao, kwa upande wa wanawake wa maji shughulisha na kazi ndogondogo Kama vile kukamua maziwa, kurisha mifugo, kupika, kupalilia bustani, kuhudumia magonjwa na watoto nyumbani.

Historia iliyoandikwa katika vitabu mbalimbali vya kidato cha pili na nne inaonesha kwamba Wamasai ni miongoni mwa jamii zilizowahi kuishi katika mfumo wa ujamaa ambao watu wake huwawanaishi katika hali ya kutegemeana katika kila kitu hususani katika uzalishaji mali na mazao yanayopatikana huwa wanagawana sawa kwa sawa, vile usawa katika majukumu ya kazi ulizingatiwa Sana kutokana na jinsia ya mtu, umri na rika hali ambayo iliondoa unyanyasaji wa kijinsia vilevile unyonyaji uliokithiri Kama uliyofanywa katika jamii za utumwa, ukabaila na ubepari.

Kutokana na mabadiliko ya hapa na pale jamii hizi zimekuwa zikibadilika kila siku lakini bado zimekuwa zikiendeleza mila na desturi potofu kila siku, baadhi ya mila na desturi hizo ni Kama vile ukeketaji kwa mabinti wa kike, jambo hili limekuwa ni changamoto kubwa Sana kwa mabinti kwa sababu ndoto za binti wengi wa kike zimekuwa zikikwamishwa na wazazi ambao wanataka watoto wao wafanyiwe vitendo hivi, hivyo basi wengi wao kutoroka nyumbani na kutokomea mahali pasipo julikana hatimaye kubakwa na watu wasiojulikana, kupata maambukizi ya VVU na UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa hali ambayo huatairsha afya yao kwa sababu vifaa vinavyotumika kufanya tohara kwa binti wa kike kuchangiwa na watu zaidi ya mmoja na pia kuwa na kitu au chakavu hivyo kusambaza maambukizi ya magonjwa na kuhatarisha maisha ya vijana wengi na kurudisha maendeleo yao ya kimasomo kwa sababu wengi wao ni wanafunzi.

Katika jamii za kimasai kunamasuala mbalimbali yanaibuka kwao Kama vile makaburi ya wamasai yapo wapi? Kwanini hakuna watu wenye ulemavu kama jamii zingine ambazo zinakuwa na walemavu wa viungo vya mwili,rangi au vitu vingine katika hali hali halisi haukuna watu wenye ulemavu katika jamii hii.

Kwa mtazamo wa haraka haraka inaonesha kuwa watoto wanaozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali katika jamii hizi huwa wanauliwa au kutolewa kafara kwa sababu katika jamii ya wamasai watoto wanaozaliwa na ulemavu wa aina yoyote kwao wanaona kama mkosi mkubwa sana, hivyo basi ili kuondoa mkosi katika jamii zao wanaamua kumuua mtoto yeyote anayeonekana na ulemavu wa aina yoyote

Jambo limekuwa ni la kushangaza na kustaajabisha machoni mwa watu wengi au kupata kusisia katika masikio ya watu wengi lakini inasadikika ukweli ndiyo hyo ,lakini swali la kijiuliza je?, umewahi kumuona mtoto kwenye ulemavu wa ngozi katika jamii za kimasia maishani mwako au mtu kwenye ulemavu katika jamii za kimasai, labla wale ambao wanamepata ukubwani pekee.

Viongozi mbalimbali wa jamii hizi wameonekana wakilifumbia macho jambo hili kwa kuwa ni sehemu ya utamaduni na desturi kwao kwa sababu kwao ni kitu cha kawaida lakini katika hali halisi ni ukiukwaji wa haki za binadamu Kama inavyoeleza katiba yetu ya nchi lakini pia wadau wahaki nchini na ulimwenguni kwa ujumla wanapiga vita vikali jambo hili kwa sababu linaharibu misingi ya upatikanaji wa haki za binadamu katika jamii hususani wenye mahitaji maalumu ikiwemo walemavu,wagonjwa,watoto wa mitaani na wengine wenye mahitaji maalumu.

Hivyo basi Kupitia utawala bora serikali haina budi kuweka Sera na mipango mbalimbali itakayoweza kusaidia kupambana na ukatili kwa watoto wenye ulemavu katika jamii hususani jamii za wamasai ambazo zinaonekana zinaendeleza vitendo vya ukatili wa kuwaua watoto wenye ulemavu pindi wanapozaliwa mara baada ya kuonekana wanaulemavu wa aina yoyote.

Serikali ni muhimili mkuu nchini ambao unamamlaka na nguvu juu la suala hili,hivyo basi hainabudi kufanya mambo yafuatayo ili kunusuru jamii na vizazi vijavyo. Kwanza serikali Kupitia wizara ya afya inapaswa kupiga marufuku wajawazito kujifungulia njumbani ili kuwarahisi kubaini watoto wenye changamoto mbalimbali za afya, kiakili na kimwili ili waweze kupewa matibabu na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu na madaktari vile vile wahudumu wa afya

Sambamba na kuwapiga faini kwa wajawazito wote wanaojifungulia nyumbani ili iwe fundisha kwa wazazi na wanajamii kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto za vifo vya watoto wachanga ambavyo kutokana na kukosa chanjo ya magonjwa nyemelezi ya pepopunda, homa ya manjano, kifafa na kichaa vile vifo vya watoto wadogo vinavyotokana na imani potofu za kishirikina na kichawai juu ya utajiri unaotokana na kuwa na kutoa kafara ya watoto wachanga ili kupata mali na utajiri wa haraka haraka

Kiuhalisia hakuna utajiri unao patikana Kupitia kutoa kafara au kuua mtu Bali utajiri wa halali, haki na kweli unatokana na kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika kazi kwa sababu ukipata bahati ya kuwasikiliza watu waliofanikiwa au matajiri wanakuambia walianza kujituma katika kazi ndogondogo lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda waliweza kufanikiwa.

Pia serikali inatakiwa kuwa ajiri watalamu wa masuala ya kijamii(social worker)ili kusaidia wanajamii wengi wenye mitazamo mibaya juu ya watu wenye ulemavu katika kutengeneza uwelewa kwa wanajamii katika ngazi ya familia,mtaa,kijiji,kitongoji,wilaya na mkoa .Kwa kuanzia wanaweza kufanya kazi katika jamii ambazo zinaonekana zinamatukio ya ukatili wa kijinsia hususani maeneo ya Arusha,Kilimanjaro,Rukwa ,Kigoma,na Mwanza.

Vile vile serikali inapaswa kuanzisha warsha, makongamano na kampeni mbalimbali ambazo zinalenga kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu juu ya watoto wenye ulemavu,hali hii itasaidia kutoka elimu kwa wanajamii juu ya watoto wenye ulemavu katika jamii ,walemavu ni jamii ya watu wenye akili na uwezo wa kufanya mambo makubwa duniani ,hivyo basi serikali haina budi kusaidia harakati mbalimbali za kuelimisha wanajamii kuhusu watu wenye ulemavu.

Pia serikali inashauriwa kukutana na viongozi wa kimila mara kwa mara ili kutoka miongozo na taratibu mbalimbali za serikali na jamii zao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, hatua hii ya serikali itaongeza ufanisi na ufuatiliaji wa karibu wa taarifa na matukio mbalimbali ya vitendo vya ukiukwaji wa sheria na kanuni mbalimbali zilizowekwa na serikali katika kupambana na mauaji wa watoto wachanga.

Katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo nchini serikali haina budi kufanya kazi beta kwa began na wataalamu mbalimbali wa afya, sheria na jamii ili kuja na mikakati ya pamoja katika kupambana na vifo vya watoto wachanga na ukatili unaofanywa juu yao ili kulinda na kutetea haki za watoto kwa sababu watoto ni taifa la kesha kwa hiyo hatua budi kuwalindq na kuwatunza siku zote.
 
Hizi, story hz, ni sawa na kuuliza umeishawahi kuona askari mjamzito?
Walemavu wamasai wapo wengi tu, nimekutana nao, zamani, ilikuwa ngumu kwa hii jamii kuchangamana, sasa hv Maasai wanaishi kila eneo,
Ww umeshawahi kumuona mmasai kwenye ulemavu wa ngozi, kwa nn Kama wapo wapo wapi??
 
Kukabiliana na jambo gani? La wamasai kutokuwa na walemavu? Au la kuhakikisha watu wanazaliwa bila ulemavu?! Watu wengine kama akili zimepiga shot. Hata wanaomuamini Yesu,wanajua walemavu walikuwepo enzi zake.
 
Wamasai ni miongoni mwa makabila maarufu katika manila takribani 150 yanayopatikana nchi Tanzania katika kanda za mikoa ya kanda za juu kusini hususani mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,jamii ya kimasai ni jamii maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na sofa ya kipekee ya kutunza na kuhifadhi utamaduni wao wa mavazi,chakula,mazishi,desturi na mambo mengine kadha wa kadha.

Kupitia sifa hizi kusaidia Sana kuwavutia wageni na watalii mbalimbali kutoka nchi za nje Kama vile Australia,Itali,Germany,India, USA na nyingine kutembelea jamii za makabila haya ili kujifunza utamaduni wa watu wa jamii kutoka katika kabila la kimasai,hali hii imesaidia Sana kutangaza utamaduni wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani ,vile vile pato la nchi limekuwa likiongezeka kila mwaka Kupitia sekta ya utalii na utamaduni hapa nchini.

Kabila la watu wa kimasai limekuwa na mila na tamaduni ambazo ni tofauti na jamii zingine ,katika utawala katila hili bado limekuwa na viongozi wake ambao wanamajukumu kwa jamii zao Kama vile Laiboni,ambao hawa kazi yao kubwa ni kutoa sheria na maagizo mbalimbali kwa wanajamii,lakini Morani nao ni vijana wa rika Kati ya 18 mpaka 25 kundi hili la wamasai wanajukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama katika jamii zao dhidi ya uvamizi wa wanyama wakali na maadui zao,kwa upande wa wanawake wa maji shughulisha na kazi ndogondogo Kama vile kukamua maziwa,kurisha mifugo,kupika,kupalilia bustani,kuhudumia magonjwa na watoto nyumbani.

Historia iliyoandikwa katika vitabu mbalimbali vya kidato cha pili na nne inaonesha kwamba Wamasai ni miongoni mwa jamii zilizowahi kuishi katika mfumo wa ujamaa ambao watu wake huwawanaishi katika hali ya kutegemeana katika kila kitu hususani katika uzalishaji mali na mazao yanayopatikana huwa wanagawana sawa kwa sawa,vile usawa katika majukumu ya kazi ulizingatiwa Sana kutokana na jinsia ya mtu, umri na rika hali ambayo iliondoa unyanyasaji wa kijinsia vilevile unyonyaji uliokithiri Kama uliyofanywa katika jamii za utumwa,ukabaila na ubepari.

Kutokana na mabadiliko ya hapa na pale jamii hizi zimekuwa zikibadilika kila siku lakini bado zimekuwa zikiendeleza mila na desturi potofu kila siku,baadhi ya mila na desturi hizo ni Kama vile ukeketaji kwa mabinti wa kike,jambo hili limekuwa ni changamoto kubwa Sana kwa mabinti kwa sababu ndoto za binti wengi wa kike zimekuwa zikikwamishwa na wazazi ambao wanataka watoto wao wafanyiwe vitendo hivi ,hivyo basi wengi wao kutoroka nyumbani na kutokomea mahali pasipo julikana hatimaye kubakwa na watu wasiojulikana, kupata maambukizi ya VVU na UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa hali ambayo huatairsha afya yao kwa sababu vifaa vinavyotumika kufanya tohara kwa binti wa kike kuchangiwa na watu zaidi ya mmoja na pia kuwa na kitu au chakavu hivyo kusambaza maambukizi ya magonjwa na kuhatarisha maisha ya vijana wengi na kurudisha maendeleo yao ya kimasomo kwa sababu wengi wao ni wanafunzi.

Katika jamii za kimasai kunamasuala mbalimbali yanaibuka kwao Kama vile makaburi ya wamasai yapo wapi? Kwanini hakuna watu wenye ulemavu kama jamii zingine ambazo zinakuwa na walemavu wa viungo vya mwili,rangi au vitu vingine katika hali hali halisi haukuna watu wenye ulemavu katika jamii hii.

Kwa mtazamo wa haraka haraka inaonesha kuwa watoto wanaozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali katika jamii hizi huwa wanauliwa au kutolewa kafara kwa sababu katika jamii ya wamasai watoto wanaozaliwa na ulemavu wa aina yoyote kwao wanaona kama mkosi mkubwa sana, hivyo basi ili kuondoa mkosi katika jamii zao wanaamua kumuua mtoto yeyote anayeonekana na ulemavu wa aina yoyote

Jambo limekuwa ni la kushangaza na kustaajabisha machoni mwa watu wengi au kupata kusisia katika masikio ya watu wengi lakini inasadikika ukweli ndiyo hyo ,lakini swali la kijiuliza je?, umewahi kumuona mtoto kwenye ulemavu wa ngozi katika jamii za kimasia maishani mwako au mtu kwenye ulemavu katika jamii za kimasai, labla wale ambao wanamepata ukubwani pekee.

Viongozi mbalimbali wa jamii hizi wameonekana wakilifumbia macho jambo hili kwa kuwa ni sehemu ya utamaduni na desturi kwao kwa sababu kwao ni kitu cha kawaida lakini katika hali halisi ni ukiukwaji wa haki za binadamu Kama inavyoeleza katiba yetu ya nchi lakini pia wadau wahaki nchini na ulimwenguni kwa ujumla wanapiga vita vikali jambo hili kwa sababu linaharibu misingi ya upatikanaji wa haki za binadamu katika jamii hususani wenye mahitaji maalumu ikiwemo walemavu,wagonjwa,watoto wa mitaani na wengine wenye mahitaji maalumu.

Hivyo basi Kupitia utawala bora serikali haina budi kuweka Sera na mipango mbalimbali itakayoweza kusaidia kupambana na ukatili kwa watoto wenye ulemavu katika jamii hususani jamii za wamasai ambazo zinaonekana zinaendeleza vitendo vya ukatili wa kuwaua watoto wenye ulemavu pindi wanapozaliwa mara baada ya kuonekana wanaulemavu wa aina yoyote.

Serikali ni muhimili mkuu nchini ambao unamamlaka na nguvu juu la suala hili,hivyo basi hainabudi kufanya mambo yafuatayo ili kunusuru jamii na vizazi vijavyo. Kwanza serikali Kupitia wizara ya afya inapaswa kupiga marufuku wajawazito kujifungulia njumbani ili kuwarahisi kubaini watoto wenye changamoto mbalimbali za afya, kiakili na kimwili ili waweze kupewa matibabu na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu na madaktari vile vile wahudumu wa afya

Sambamba na kuwapiga faini kwa wajawazito wote wanaojifungulia nyumbani ili iwe fundisha kwa wazazi na wanajamii kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto za vifo vya watoto wachanga ambavyo kutokana na kukosa chanjo ya magonjwa nyemelezi ya pepopunda, homa ya manjano, kifafa na kichaa vile vifo vya watoto wadogo vinavyotokana na imani potofu za kishirikina na kichawai juu ya utajiri unaotokana na kuwa na kutoa kafara ya watoto wachanga ili kupata mali na utajiri wa haraka haraka

Kiuhalisia hakuna utajiri unao patikana Kupitia kutoa kafara au kuua mtu Bali utajiri wa halali, haki na kweli unatokana na kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika kazi kwa sababu ukipata bahati ya kuwasikiliza watu waliofanikiwa au matajiri wanakuambia walianza kujituma katika kazi ndogondogo lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda waliweza kufanikiwa.

Pia serikali inatakiwa kuwa ajiri watalamu wa masuala ya kijamii(social worker)ili kusaidia wanajamii wengi wenye mitazamo mibaya juu ya watu wenye ulemavu katika kutengeneza uwelewa kwa wanajamii katika ngazi ya familia,mtaa,kijiji,kitongoji,wilaya na mkoa .Kwa kuanzia wanaweza kufanya kazi katika jamii ambazo zinaonekana zinamatukio ya ukatili wa kijinsia hususani maeneo ya Arusha,Kilimanjaro,Rukwa ,Kigoma,na Mwanza.

Vile vile serikali inapaswa kuanzisha warsha,makongamano na kampeni mbalimbali ambazo zinalenga kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu juu ya watoto wenye ulemavu,hali hii itasaidia kutoka elimu kwa wanajamii juu ya watoto wenye ulemavu katika jamii ,walemavu ni jamii ya watu wenye akili na uwezo wa kufanya mambo makubwa duniani ,hivyo basi serikali haina budi kusaidia harakati mbalimbali za kuelimisha wanajamii kuhusu watu wenye ulemavu.

Pia serikali inashauriwa kukutana na viongozi wa kimila mara kwa mara ili kutoka miongozo na taratibu mbalimbali za serikali na jamii zao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, hatua hii ya serikali itaongeza ufanisi na ufuatiliaji wa karibu wa taarifa na matukio mbalimbali ya vitendo vya ukiukwaji wa sheria na kanuni mbalimbali zilizowekwa na serikali katika kupambana na mauaji wa watoto wachanga.

Katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo nchini serikali haina budi kufanya kazi beta kwa began na wataalamu mbalimbali wa afya, sheria na jamii ili kuja na mikakati ya pamoja katika kupambana na vifo vya watoto wachanga na ukatili unaofanywa juu yao ili kulinda na kutetea haki za watoto kwa sababu watoto ni taifa la kesha kwa hiyo hatua budi kuwalindq na kuwatunza siku zote.
Serikali Waanze na wanaotoa mimba na kuzituma chooni. Kutoa mimba ni mauaji makubwa sana na yanapaswa kukomeshwa.
 
Back
Top Bottom