Majuto ya Chid Benz

Wapo wengine wanapona na hayo mambo hata wakiwa vipi ila Kuna doctor mmoja aliwahi nambia Kuna group la damu ukionja ni ngumu kuacha .Na sikumbuki ni group lipi.

Ila pia alisema hata hzi dawa Kuna magroup ya damu wakitumia wakiumwa zinakuwa na nguvu hafifu kulinganisha na group lengine.
 
Breathing na empty wall meditation Mimi ndio naweza zaidi
Mimi napenda kuanza na breathing ya inhale na exhale ya kawaida then naingia kwenye matras zangu za maguru wa lights and sound meditation
 
Inaonekana ilikusumbua sana ndio maana kila muda unatuma hii comment kuashiria ushindi mkubwa 😃
Hapana.

Nimekuwa nikiacha pombe kwa miaka miwili au zaidi, ila sasa nafanya kimoja.

Ninaandika hivi si kwa sababu naona ushindi mkubwa sana, bali kwa sababu nataka kuwatia moyo wanaohangaika kuona kuwa inawezekana.

Ila kuna watu kama wewe wasioweza kuangalia hoja bila kui personalize hamkawii kuanza kunichambua mimi badala ya kuangalia hoja ya msingi kwamba kuna watu wanaweza kukaa bila hata kunywa pombe.

Ni kama unaona kinyongo fulani na kuidogosha juhudi yangu kwamba si mali kitu.

Yani unaumia mimi kuandika sijakunywa pombe toka January 1 2024.

Inakuumiza sana kuona naandika hivyo.

Mtu kama wewe unaweza hata kwenda kwenye msiba ukaionea wivu maiti kuwa inapata attention kubwa kuliko wewe, ukatamani wewe ndiye ungekuwa umekufa uko kwenye jeneza watu wote wanakuangalia.
 
Siumii mkuu nimewaza tu labda kabla hujaacha ulihangaika kama sisi wengine
 
Huku mtaani huyu angepelekwa kwa mtaalamu, wakati mwingine watu wanapigwa "ballistic missile" za asili. Huyo hata akae rehab miaka 10 akitoka tu amekwisha.
 
Atapewa mwili mpya kwa Mungu awe na Imani
 
Mimi nimetumia cocaine kipindi nasoma chuo baada ya Kuona ganja aipandi tena kwa mda wa mwaka mmoja nilikuwa mraibu wa kimya kimya na sababu ni depression na sikuwa na mtu wa kumueleza shida zangu

Ni stori ndefu kidogo lakin namshukuru sijaenda sober na niliacha kwa hiari
 
Pole na hongera sana
 
Siumii mkuu nimewaza tu labda kabla hujaacha ulihangaika kama sisi wengine
Hapana mkuu.

Katika mambo yanayoweza kunihangaisha pombe haipo.

Hapa nimeacha kunywa lakini ndani kuna beer, kuna Scotch, kuna white wine, kuna Tequila, kuna gin, kuna vodka.

Na kila nikiacha kunywa lazima niwe na pombe namna hiyo ndani ya nyumba nijue nimeacha kunywa wakati pombe ninazo, si suala la kuishiwa na pombe ndani tu.

Nazipita kila siku hata sizifikirii mara mbili. Tena kama beer zipo kwenye friji langu la garage chini baridiii, kila nikifungua friji naziona. Ila hata sifikirii kunywa.

Akinitembelea mgeni anayekunywa atakunya anavyotaka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…