Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Wewe nae huelewi au?!kwa makonda wanaenda watu waliotelekezwa sio kulalamika hela haitoshi...matunzo ya mtoto unatoa kutokana na uwezo wa kipato chako
Mkuu, kwa kichwa cha huyo mchepuko anaweza sema huwa hapewi kabisa. Jingine kubwa, wife hajui. Labda ndo kinachomkosesha usingizi.
 
Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara _ Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.
Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake artena haipo sawa najua hatanii ataenda tu, nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika. Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobeto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"... wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone... Ushauri tafadhali..
Mpatie hii keki, atatulia.
20180408_110618.png
 
Nchi hii haina sheria ya kumfunga mtu kwasababu ya child support, kamuulize Mobeto Vs Diamond Platinum...


Acha uoga kama una uoga njop PM usaidiwe.
Mkuu, kuna kadada kananitishia hivo hivo kwamba kesho katanipeleka kwa Makonda. Nimemwambia nenda. Siku za nyuma nilimwambia nataka kwenda na mtoto kwa mkemia mkuu ili tupime DNA nisije kua natunzia mwanaume mwenzangu akakataa. Nikamwambia basi leta mtoto nikae nae nimlee mwenyewe akakataa pia. Nikasema well hupati hata sh 10 tena kutoka kwangu na kweli sikumpa hela tena mpaka leo. Basi kelele zake haziishi kwamba nimetelekeza mtoto na sasa ameibuka na hio ya kwenda kwa makonda kesho nimemwambia nenda. Sasa je hapo sheria inanibana vipi.
 
Hii issue wife ilikuwa bado kumwambia.. kwani inahitaji utulivu vinginevyo naweza haribu kote

Kuna wakati shemeji atajua tu, @USIKUBALI KUISHI KAMA MTUMWA@ Huyo Dada ni kichaa kuna siku atamwambia tu.....
 
[emoji134] [emoji134] [emoji134] Usitake kuniliza mkuu. Sijawahi fikiria kuingia kwenye jaribu kama hili

Hehehehehehe...ndio vzr ukijua unamwambia amlete mumlee nyumbani
 
Aende tu ukomeshwe kwa niaba ya wanaume wenzio wasiopenda kukituliza!zipu waz[emoji52]
 
Laki 2 kwa mwezi.haitoshi?? Au umekuja kutoa kiki kwani akienda utakufa? Kama huna uwezo wa kumpa mil.10 kwa mwezi ufanyaje uibe?? Hata akienda Kuna mahakama zitaangalia kipato chako vs uhalisia...

Nchi hii ina sheria zake haya matamko yatarudi kisheria
Mkuuu kiukweli 200000
Kwa mwezi ni pesa ndogo hasa akiwepo mtoto

Ila huyo mwanamke ameshasoma udhaifu wa jamaa
Na atamwendesha sana kwa style hiyo.

Mie ningekuwa huyu mwanaume ningemwambia nenda tu
Sms za miamala zote ninazo na ukileta ujinga naenda kufile nimchukue mtoto.
 
Anabahati sana ,wenzie tunapata elf 50 kwa miaka 3,naona kesho mm nitakuwa wa kwanza!!
 
Mkuu, kuna kadada kananitishia hivo hivo kwamba kesho katanipeleka kwa Makonda. Nimemwambia nenda. Siku za nyuma nilimwambia nataka kwenda na mtoto kwa mkemia mkuu ili tupime DNA nisije kua natunzia mwanaume mwenzangu akakataa. Nikamwambia basi leta mtoto nikae nae nimlee mwenyewe akakataa pia. Nikasema well hupati hata sh 10 tena kutoka kwangu na kweli sikumpa hela tena mpaka leo. Basi kelele zake haziishi kwamba nimetelekeza mtoto na sasa ameibuka na hio ya kwenda kwa makonda kesho nimemwambia nenda. Sasa je hapo sheria inanibana vipi.

Very good akikupeleka unamuambiaa uliomba DNA kakataaa akubali kupima utaleaaa
 
Wewe usiogope tupo wengi. Kwanza wiki hiii ya kesho, itanyesha mvua ya hatari, kwa iyo zoezi halitafanyika
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] ndoa zitavunjika kama wamama hatutakuwa imara,mm wangu kesho itabidi nimsindikize kazini mpk nirudi nae!
 
Mtoto anaumwa kata bima ya afya NHIF ni elfu 78 kwa mwaka kama sikosei utapunguza gharama
 
Labda niseme hakuna nchi yenye sheria mbovu za child support kama Tanzania, huwezi kufungwa kwa kosa la child support nchi hii na hakuna kiasi maalumu cha kumsaidia mtoto.


Usiogope nenda nae kwa makonda hakuna jipya kule zaidi ya maridhiano kati yako na huyo mwanamke.



NB. LEA MWANAO
 
Back
Top Bottom