Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara _ Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.
Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake artena haipo sawa najua hatanii ataenda tu, nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika. Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobeto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"... wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone... Ushauri tafadhali..
Baba komaa ndio maana ukazaliwa mwanaume...kama mbwai mbwai tu, wanaume tumeumbwa mateso raha kidogo
 
Ukifika usikatae bali mwambie wapime DNA na cheti cha kuzaliwa mtoto apeleke
Maana siku hizi wapo wadada mtoto mmoja anawapakazia wababa watatu kila mmoja anakuwa na cheti cha clinic Ila cheti cha kuZaliwa hana ujanja huwa kimoja na yeye huendelea kuchukua matunzo kote
 
Kama mtoto anaumwa umwa mkatie bima ya afya ya NHIF kwa watoto ni 54,500/= tu kwa mwaka...
Then matumizi tuma 120,000/= kwa mwezi....
Tafuta namna ya kumuambia mkeo una mtoto nje...

Kumuambia mke una mtoto nje wakati hajawahi kuwa na shida ya uzazii ni kumtonesha na kumtuma naye akuletew mtoto wa nje Kwa hasira , hiyo sisi tuliofundishwa na wazee wanasema unasubiri hadi afike miaka 45 kwenda juu , umri huo mwanamke anakua na utu uzima fulani na hawezi kuondoka Nyumbani na hata matamanio yake ya ngono yanaanza kushuka na pia pengine sio rahisi kutaka kukukomoa kwa kwenda nje na mtoto atakuwa amekua Mkubwa hivyo kwake haihitaji kukesha na kumkoshaaa
Na hutakiwi umuambiaa wewe unatuma wapambe wanampelekea kama umbeaa , Sasa akikuuliza nawe unasema “ni kweli mke wangu hizo fununu nazisikia Ila sijawahi kumuona pengine sio wangu hadi nimuone”
Kwa busara zake lazima atakuambiaa mlete akae na Ndugu zake
 
Akienda kwa Makonda huyu utaitwa kupongezwa na probably kuambiwa upunguze na uwe unampa laki tu. Mwambie hiyo Jumatatu akusubiri umsindikize. Jaribu pia kuwa mwanaume. Yaani kijimkwara mbuzi hicho ndo cha kukufanya ukaribie level za Nabii Tito!?
 
Sheria ya nnchi kupitia ustawi wa jamii ni elfu 75 kwa mweziiii. Kwanza laki 2 unampendelea sana mm wife wangu alikimbia akaenda nikamwambia nenda nikaweka mwanasheria sasa anaambulia elfu 75 tu basi.

Uwe na huruma kwa damu yako kama pesa unazo usiangalie hilo japo kuna wamama hufanya watoto mradi anakuomba pesa anakuambia mtoto hiki mtoto kile kumbe anaenda kula na mabwana wewe lipa Kila kitu direct na kila wiki watoe our na hiyo 75 ndio yeye ataamuaa kama anywee au ahonge
 
Itunze hio mesej ya mwamala wa pesa uliomtumia kama ushahidi wako
Kingine—ameshajuwa werkness yako ndio maana anakuendesha kama gari bovu
Akikwambia ataenda kwa makonda kukuripoti
Mjibu—Mbona umechelewa?changamka sasa hivi uwende
Tatazo anakudesh kidoogo wewe mavi debe
Kila unavozidi kumpliz ndio unazidi kumpa bichwa

Huyo MAKONDA naye angekua na watoto wa nje agetuelewa
Huyo bosi wake mwenyewe Anao kila mahali , wengine alikua amewatelekezaa
 
Kaka usiogope, mwache aende. Mwambie aende tena kama vp msindikize.
 
Ongea na mkeo kuhus kuzaa nje. Atakuelewa tu ingawa itamuumiza. Kisha anza utaratibu wa kumchukua mtoto wako. Ukifika ustawi wa jamii waambie mazingira anayoishi mtoto wako si salama. So unataka kumlea mwenyewe. Na uwezo wako n kumlea mtoto tu si na mama ake. Kwa mwezi unaweza kutoa sh 150,000 kw Matumizi ya mtoto.
Mkatie bima ya Afya mtoto n sh 52000
 
Kamchukue mwanao kwa huyo m'mke na ujiandae kumpelekea mkeo huku ukiwa umejianda kwa lolote litakalotokea huko kwa wife wako, maana ulilikoroga mwenyew hvyo ujiandae kulinywa
 
Ulitumwa utongoze mzaramo..shuzi lako hilo pambana nalo mkuu
 
Kumuambia mke una mtoto nje wakati hajawahi kuwa na shida ya uzazii ni kumtonesha na kumtuma naye akuletew mtoto wa nje Kwa hasira , hiyo sisi tuliofundishwa na wazee wanasema unasubiri hadi afike miaka 45 kwenda juu , umri huo mwanamke anakua na utu uzima fulani na hawezi kuondoka Nyumbani na hata matamanio yake ya ngono yanaanza kushuka na pia pengine sio rahisi kutaka kukukomoa kwa kwenda nje na mtoto atakuwa amekua Mkubwa hivyo kwake haihitaji kukesha na kumkoshaaa
Na hutakiwi umuambiaa wewe unatuma wapambe wanampelekea kama umbeaa , Sasa akikuuliza nawe unasema “ni kweli mke wangu hizo fununu nazisikia Ila sijawahi kumuona pengine sio wangu hadi nimuone”
Kwa busara zake lazima atakuambiaa mlete akae na Ndugu zake
Asante mkuu kwa kuniongezea ujuzi..
 
Wanaoenda kwa Makondo ni wale ambao wametelekezwa... Kwani wewe umemtelekeza?

Maana kama pesa unatoa tena ndefu Sanaa....

Be happy man...
 
Nchi hii haina sheria ya kumfunga mtu kwasababu ya child support, kamuulize Mobeto Vs Diamond Platinum...

Acha uoga kama una uoga njop PM usaidiwe.
 
Back
Top Bottom