Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Ningekuwa mm ningewaambia watu wa mtandao nimekosea kutuma hela
 
Mkuu waoenda kule ni wale walio telekezwa. Yaan ambao wametia mimba then wakaingia mitini, ambao unakuta hata sura ya mtoto hawajui. Swala la kiasi gani umpe mwanamke linategemea na kipato unachoingiza. huwezi mpa mill wakati unaingia 5500 kwa mwezi. Acha uwoga wewe
 
Mkuu mweleze tu wife ili huyo mzaramo aache kukuendesha then kwenye hio laki mbili punguza mpe hata laki na kumi ili akili imkae vizuri. kuhusu makonda hili picha mwisho bado hauja andaliwa so usihofu halina madhara
 
abuja.jpg


Ilikuwa kama utani mwaka 2016 tukiwa kwenye daladala za Kimara - Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kiume ikapatika na akajifungua salama salmini.

Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama 250,000/- kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia..
Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa Jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na Mzaramo huyu kama mnavyojua kichwa chake antena haipo sawa najua hatanii ataenda tu.
Nimejaribu kumtumia rafiki zake amshauri imeshindika.

Jana jioni nimemtumia 100,000/- asubuhi hii kanitumia sms hii...
"Unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobetto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"...

Wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea peke yangu.
Ushauri tafadhali.
 
mwambie anakazwa...usimpe hata ndururu huyo chuma ulete, nendeni ustawi wa jamii akaadabishwe...alafu muombe msamaha mkeo na umwambie ukweli
 
Mwambie aende kwa Makonda. Mwanaume ujasiri. Makonda sio sheria.
 
Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara - Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.

Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake antena haipo sawa najua hatanii ataenda tu. Nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika.

Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "Unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobetto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"...

Wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone. Ushauri tafadhali.
Pole sana
 
Huwezi kuishi na huu utumwa, Kama uoga wako ni kwa Makonda, kwa laki 2 hakuna anachoweza lalamika zaidi, that is enough money. Usikae kwenye huu utumwa, mwambie afanye analotaka basi! Hili nalo litapita kabisa, usiwe mtumwa bila sababu.
 
Back
Top Bottom