Mkuu naomba nikuulize baadhi ya maswali Kama hutojali
Karibu Mkuu.
Hivi ni ipi nafasi ya mwanamke kwa mwanaume?
Nitajibu kwa kuchukulia muktadha wa ndoa. Kwa kifupi kabisa, nafasi ya mwanamke ni kumkamilisha mwanaume.
Hii ni kwa kumsaidia:
• Ushauri sahihi katika mambo mbalimbali hasa yanayohusu familia
• Malezi ya familia na watoto
• Kumpa faraja, kumuunga mkono na kumtia moyo katika mambo na hali zote
• Kukaribisha na kuwakarimu wageni wote
• Kumrekebisha, kwa kutumia busara na upendo wa hali ya juu, pale anapokosea
• Kuwa chanzo cha furaha na amani, n.k.
Bottom line: wajibu wa kwanza wa mwanamke (primary responsibility) ni kumtii mumewe katika mambo mema yote yampendezayo Mungu.
Na Ni ipi nafasi ya Roho mtakatifu kwa mwanaume?
Nafasi ya Roho Mtakatifu kwa wanadamu wote, akiwemo mwanaume, ni kutufariji na kutuongoza kupitia mapaji yake saba: elimu, hekima, akili, nguvu, ibada, shauri na uchaji wa Mungu.
Roho Mtakatifu anatusaidia na kutuonesha njia zitupasazo kuzifuata na kuziishi ili kumpendeza Mungu na kuendelea kuwa watoto waaminifu wa Mungu.
Roho Mtakatifu anatufundisha na kutushauri tuweze kutawala mazingira yetu na kufanikiwa bila kuharibu utaratibu aliotuwekea Mwenyezi Mungu wa kuendelea kuifanya dunia mahali pema na salama pa kuishi; sisi na viumbe wengine.
Wote ni wasaidizi Ila ningependa kujua tofauti zao.
Utofauti wao ni:
• Wakati mwanaume anamsaidia mwanamke na mwanamke anamsaidia mwanaume; Roho Mtakatifu anawasaidia wote, mwanaume na mwanamke.
• Mwanamke anamsaidia mwanaume kimwili (physically)
zaidi wakati Roho Mtakatifu anatusaidia sote kiroho.
• Mwanamke anamsaidia mwanaume kwa msaada wa Roho Mtakatifu wakati Roho Mtakatifu mwenyewe (bila msaada wa yeyote) anamsaidia mwanaume na mwanamke.
Tofauti kubwa kuliko zote: mwanamke ni mwanadamu na anaweza kuwa na mapungufu yake hasa katika kutimiza nafasi yake kama mke; wakati Roho Mtakatifu ni Mungu na amekamilika, hana mapungufu.
Wasalaam.