Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,698
- 2,560
Wah! Tikerra hii ni post nzuri na unachokisema ni jambo ambalo lipo na vijana wengi sana huku kwetu uswazi washaumia kutoka na kutumia, kuuza au kusafirisha madawa ya kulevya. Ila ninatofautiana kuhusiana na hao uliowaita viongozi wetu walishughulikie ili swala manake wao kwao ni mtaji ni sawa sawa ulivyosikia million zaidi ya 15 zimetumika kuamisha omba omba Dar.
Tatizo la madawa la kulevya ni la kijamii zaidi kuliko linavyochukuliwa sasa kwamba ni la kijinai na hakuna jitihada za muda mrefu ambazo zinalenga kukomesha utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya. Mateja wengi wamekufa kwa kujidunga, wengi pia wamepata ukimwi kwa kutumia madawa kutokana na kushirikiana vifaa vya kujidunga na zaidi na zaidi mateja pia wanakuwa mashoga (Injected drug users) na mateja wakikamatwa na kuwekwa magerezani ndio wanakuwa mabibi za watu huko kutokana na mahitaji yao ya madawa na huko hayapatikani.
Kibaya zaidi watumiaji wanakuwa na mchango mdogo sana katika jamii kama sio kuwa mzigo, mateja wamekuwa ombaomba na wezi. Addiction kupita kiasi ndio sifa kubwa ya utumiaji wa madawa. Tatizo hili ni la kwetu zaidi wana jamii kuliko hao viongozi ambao wako buzy wanajihudumia.
Ni wakati muhafaka kwa jamii forum members kutoka sehemu mbali mbali duniani kutoa uzoefu wao labda inaweza kusaidia kumaliza hili tatizo nilishawahi kusikia Uholanzi wao wameruhusu utumiaji wa madawa ya kulevya na utumiaji ukapungua. Kunamaeneo mengine wananyonga kama Singapore na China .