Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

Sio inasemekana, Kikwete ameshawahi kusema kwua alipelekewa orodha ya majina ya wauza unga, inashangaza kuwa hadi leo ahtujaona hatua zozote kuchukuliwa licha ya yeye kusema kuwa ameyakabishi kwa taasisi inayohusika na mambo hayo

Huenda uchaguzi unapokaribia, ndio majina yanaanza kuisogelea mahakama...
 
Sure Mwanakijiji wakikutumia anika hapa, japo kuna watu watasema ukamatwe kwa kuiba 'nyaraka ya siri'.

Yupo Gembe atadai ukamatwe kwa kumiliki nyaraka za siri za serikali - MAJINA YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA !! Lo kweli kokoro huzoa mengi - we acha tu!!
 
Yupo Gembe atadai ukamatwe kwa kumiliki nyaraka za siri za serikali - MAJINA YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA !! Lo kweli kokoro huzoa mengi - we acha tu!!

Mag.

Mie Nilikuwa mstari a Mbele sana kuwaomba watu wataje Majina ya madawa ya kulevya ile leo kwasababu nimemzungumzia Slaa unadhani mie ni mtu wa Ovyo siyo?

Mtu akishidnwa kujibu hoja siku zote uishia kwenye kuleta Viroja ili kufurahisha jamvi.Na hii inaonesha jinsi gani tulivyo,tunapenda bla bla tu.

Mpka kesho ,Mie nahitaji kufahamu wauzaji wa madawa ya kulevya..Kwa hili mag umenikosea na nimekuweka kundi moja ya wale wanasiasa wenye kuedekeza siasa za maji machafu!
 
Kweli mkuu, hivi hii issue imefia wapi maanake imefunikwa hadi leo.
Naona jamaa anaogopa kuwataja
 
Inawezekana kabisa wamechatiliwa chao hivyo wamejikalia kimya kama sio wao waliosema wana majina,inawezekana kabisa kwa leo ukiwauliza wakasema hawajawahi hata kuzungumziwa mambo hayo ,zaidi ni ya magazetini.
 
hiyo mbona sio ishu sana ya MAFISADI yapo LIVE na hatua hazijachuliwa juu yao tena wao wameiba kwa serikali sembuse hao wanafanya hiyo biashara kwa kujificha.! tatizo serikali LONGO LONGO nyingi na hakuna amtendo ya ukweli katika kuchukua hatua mi nasema hiyo biashara kuimaliza ni kazi kwa sababu hakuna hatua madhubuti inayofanyika,tutapigwa kalenda na mara hichi mara kile huku muda unapotea vile vitu vya kufanya kutuletea maendeleo vina stop,waTz tunapiga mastori. INATIA HURUMA SANA.
 
Kama sikosei Mh. Kikwete alidiriki kusema ana majina ya wauza madawa ya kulevya wakubwa sikumbuki ni mwaka gani lakini nadhani ni 2007. Sasa miaka 5 inaisha hasemi lolote na hatuja sikia waliokamatwa kwa maelekezo yake.

Nachelea kusema rais hapo ulitupiga changa la macho ili tujue wawajua kumba hakuna lolote. Katika makosa ambayo watanzania wamefanya ni kuchagua rais muongo na malipo yake ni makubwa.

Kama kweli hukudanganya basi wataje kabla ya kumaliza muda wa miaka yako 5.
 
nakumbuka alisema nayo alipokuwa anaingia 2005 lakini inawezekana on the way kile kikaratasi kilidondoka ndiyo maana hata kampeni zake za 2010 hakutaja hilo
 
Atafanya nini hapo jk wakati kuna mashemeji, wakwe na maswahiba kwenye listi, ile ilikuwa danganya toto, hana lolote.
 
Ana majina ya watanzania wote Raisi wetu. Ameyafanyia nini? Ina maana Usalama wa Taifa hawakuwa nayo? Taarifa za kiintelligensia hakuna? Zipo za maandamano tu!
 
Katika mambo mengi yanayonishangaza ni pamoja na hili. Nakumbuka mkuu wa kaya alipewa majina ya vigogo wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya na kwa mkwara akasema atayatangaza lakini hadi leo yupo kimya. Je anawalinda au na yeye ndo boss wao? kama hapana basi atakuwa anapenda sana hiyo biashara maana hadi sasa angekuwa ameshawachukulia hatua.
au ndo yale ya EPA alipowaambia rudisheni fedha kisha mambo yanaisha.
Wawakilisha wetu je kwa nini wasihoji hili huko mjengoni hayo majina yatolewe na yawekwe wazi? Kaka na Dada zetu wanazidi kuwa vichaa kwa mkuu kukaa kimya na hiyo list mfukoni.
Kama aliwahi kuwataja naombeni wana JF mnifahamishe maana mimi sijasikia:sad:
 
Back
Top Bottom