Majina waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 haya hapa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Wanafunzi 1, 073, 941 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 wakiwemo wavulana 514, 846 na wasichana 559, 095 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Desemba 14, 2022 na Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2023 imeongezeka kwa wanafunzi 166, 139 sawa na ongezeko la asilimia 18.30 ikilinganishwa na wanafunzi 907, 802 walopata alama ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.

Majina waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 haya hapa

Kati waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2, 775 sawa na asilimia 0.26 ambao kati yao wavulana ni 1, 491 na wasichana 1, 284
 
Kwa nini walimu wanawajazia wanafunzi fomu za kuchagua shule?
 
yaani tamisemi hawajajishughulisha kabisa kufanya selection, haiwezekani shule ina wastani wa 290 na tunajua uwezo wa watoto unawapeleka watoto wote shule ya kata
Kwakweli hili linashangaza sana.
 
Back
Top Bottom