Majibu ya wanawake wa Gongo la Mboto

Majibu ya wanawake wa Gongo la Mboto

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Wanawake wengi ambao wanaishi Gongo la Mboto (Masister duh) ukiwauliza wanakaa wapi watakujibu wanakaa "Airport"

Sasa huwa najiuliza, wewe unakaa Gongo la Mboto kabisa tena ukifika Gongo la Mboto unapanda daladala kisha unachukua bodaboda ukishuka kwenye bodaboda unachukua baiskeli mpaka nyumbani lakini ukiulizwa unakaa wapi? Unasema nakaa "Airport"

Tofauti sana na wanaume, mwanaume atakwambia mi nakaa Gombs mwanangu au UK.Kina dada, kama unakaa Gongo la Mboto sema unakaa Gongo la Mboto na sio kusema unakaa Airport.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Hakyanani,kuelekea octoba 25 tutasikia mengi sana.
 
unaonea aibu unapolala, kuna watu wanapatamani hata huko la mboto, mambo mengne hayana akili na wanaoyafanya hawana akili pia
 
hahha airport!!? nlikua sijawai fikiria hili ila kweli wapo karibu nayo bnah
 
Ila hilo jina tu " Gongo la Mboto" baya.. Wafanye mchakato walibadilishe.
 
Kwahyo Umepatia PHD kwa uchunguzi kama huu?
 
Gombs lol
umenkumbusha ile college yetu ya Udom ng'ong'ona, huwezi kuisema unasema ng'ox
 
Na wadada wanaokaa Tandale!!!, Ukiwauliza wanapoishi watakwambia wanaishi Kijitonyama!!!
wale wa manzese ya switkona hadi Tipi, watakwambia wanakaa Sinza.
wale wa Wazo, Watakwambia wanakaa Mbezi Beach.
yani shida tupu!!!
 
Kitu Ng'ox kwa 'wajasi' daaaa kweli maisha yanaenda kasi sana.....asee!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom