A
Anonymous
Guest
Najua nikitoa hapa kero yangu hapa Jukwaa la Fichua Uovu, kero yangu itafika kwa wahusika.
Kero yetu/yangu kubwa ni kwa Wahudumu wa CRDB Tawi la Gongo la Mboto lililopo pale Mzambarauni Kiukweli, Dar es Salaam, wale wahudumu ni wasumbufu na wanakera mno.
Nitoe kisa kimoja, Jumanne ya Novemba 28, 2023 nilienda pale kuchukua kadi yangu mpya baada ya kupoteza ya zamani,
nilitumiwa SMS tarehe 25 Nov kwamba kadi ipo tayari nikachukue pale.
Basi nikaomba ruhusa kazini kwamba nitachelewa kufika kwa saa kadhaa, nikaahidi hadi saa nne Asubuhi.
Nilifika mapema Benki na kulazimika kusubiri wafungue, ulipofika muda wao wa kufungua hakuna hata mpangilio mzuri unaotuongoza wateja, haijulikani usimame wapi, wahudumu wanashindwa hata kuwapanga wateja.
Ilipofika zamu yangu nikawaeleza shida kilichonipeleka pale, wakauliza nilipata SMS, nikawaambia ndio na kuwaonesha.
Basi mhudumu mmoja akaingia ndani kutafuta kadi, alikaa huko kuanzia saa mbili hadi saa tano hakutoka, wakati huo mimi nimeaga kazini kuwa saa nne nitaingia wa kuwa nilijua ni suala la kwenda kuchukua kadi tu.
Basi nikaondoka bila huduma, kiukweli huduma ya pale hovyo sana wahusika wajue hilo.