Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

kwa hili naona umeanza kuonyesha rangi yako halisi...YES this is your truely color!
 
Mwongo na mzushi. Siku yenu inakuja na tutawafunga na kuwanyang"anya mali na nyumba zenu zote na ikiwezekana kuwanyonga. Cku inakuja kigwangala wewe na JANGILI mkuu wenu kinana mtanyea debe. Siku zinahesabika
 
wapi mafisadi wakubwa hakuna mtoto wa kumdanganya humu
 
Nanukuu "Si kila mtu aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi wapo pia"

Aisee Mh. unamaanisha hii sentensi? na je chama kimekupa ridhaa kutoa kauli hii? isnt this a
conclusion? Athante thana kwa ithibitisho.
 
mkuu MBWA WA MANZESE, ni wazi maelezo marefu ni sawa na miruzi mingi, ungelikuwa ukweli ingeandikwa mistari miwili au mitatu na tungeelewa ila haya angeyepeleka mahakamani kujitetea

 
Mbona issue ya Kinana chama kinamjibia kwa nguvu zote?
Sikushangaa kupata jibu lako. Tatizo la watu kama wewe hamtofautishi utendaji wa bunge na vyama au serikali na vyama.

Kwa nini Msigwa ameenda kulisema bungeni ambako Kinana hana uwezo kisheria wa kwenda kulijibu au kumpeleka mahakamani?. Na ikumbukwe, analikuwa ana muda wa kulisema jina la Kinana pale alipowambia watu kuna KIGOGO anafanya biashara ya nyara za nchi. Lakini kwa kujua kama anaganganya, hakufanya hivyo ili kuogopa kushitakiwa mahakamani. Wabunge wa CHADEMA wanatumia vibaya, sheria inayowalinda ili kujinufaisha kisiasa.

Kwa mawazo yako, ulitaka Kinana aende bungeni kujibu tuhuma wakati katiba ya nchi kipengele cha 100 inasema hivi,

100 (1) There shall be freedom of opinion, debate and in the National Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly.

(2) Subject to this Constitution or to the provisions of any other relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to anything which he has said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of a petition, bill, motion or otherwise.

Tumia akili uliyopewa kuelewa mambo na siyo akili ya kishabiki.
 
Dah, Daktareeee, Mbunge na mfanya biashara, kaaazi kweli kweli!
 
Niwape pole wale wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili,
haswa familia yangu, ndugu, marafiki na wananchi wa Nzega;
ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.

Mkuu HKigwangalla ,
Hapo Juu kwenye Quote Nadhani wote uliowa orodhesha hawafiki hata 7

PS
Mbona ile issue ya Said Bagaille umekuwa unairuka sana, haiwezekani Kila siku usakmwe wewe tu.
Kuna ka Ukweli Hapa isee
 
Last edited by a moderator:
Hamisi, uwe muwazi kwa hili. Umesema wewe unamiliki hisa 40% na mkeo 11% ambazo zote jumla ni 51%. Je 49% zilizobaki zinamilikiwa na nani? Watoto wako au nani?
 
Sasa kama huna sababu ya kuthibitisha lolote kwa yeyote humu nini kimekufanya uandike mgazeti wote huo na kuuweka humu? Si ungeandika na kubandika huko kwenye litovuti lako la www.hamisikigwangalla.com....

Kuna watu walimshauri aulete huu mjadala hapa jamvini yeye na hasimu wake ili mbivu na mbichi zijulikane. Rejea katika status zake kwenye facebook page yake.
 
hata kama ingekuwa kweli ungekubali?...hata kinana amekataa kata kata...ili hali watanzani tuna ujua kweli....
 
Bwana @HKingwangalla, Nilichofurahi toka kwako ni kuwa angalao unathubutu kujitetea, ingawa doesn't make that much sense -- jipange upya!
 

Upo sawa kabisa maana unakuwa upo kwenye chungu kabisa lazima utajipendelea kwenye kujipakulia kama tulivyokuwa shule ukiwa kwenye kitengo cha msosi unakula vinono, haikatazwi ila ni kwa kiasi kila kitu na si mambo hadharani sana, mbona wengine hawalalamikiwi? najua na wao wana vikampuni vyao pia

Kingine MSUKUMO WA JAMII unawafanya wawe hivyo maana kama akishindwa ubunge alafu akawa hana kitu akirudi huku uraiani anachekwa amefulia wakati alikuwa na nafasi nzuri ameshindwa hivyo kuna ambao wanachachalika kwa umakini lakini wangine wanakomba mboga mpaka wanashikwa mkono
 
Bwana HKigwangalla, Nilichofurahi toka kwako ni kuwa angalao unathubutu kujitetea, ingawa doesn't make that much sense -- jipange upya!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu debe tupu haliachi kuvuma, au siju niseme mkono mtupu haulambwi, au fuata nyuki ule asali? anyway kwa kifupi ni kuwa unapokuwa kiongozi baadhi ya watu lazima nao wanatamani kuwa kama wewe au kuchukua nafasi yako, kumbuka kuwa kuna WATU wanamani kuchukua nafasi ya MUNGU pia!! ili iweje? Mungu nae keshasema hapendezwi na wanaotaka nafasi yake na anao wivu mkubwa juu yao wanajifanya nao ni Miungu!!! No more comments!! nimepita...
 
Hamis bwana hivi tangu lini mbunge akawa ni wa CCM akawa sio fisadi?kwani mara ngapi umekuwa ukisimama hata mbungeni kutetea mafisadi?na hii ni kwa sababu ni mafisadi wenzio,hivi unataka kuniaminisha wewe ndo hutaki dezo?kama hutaki dezo kwa nni uliomba msamaha wa kodi?acha kutongopea wewe bwana umekwepa kodi ili ujinufaishe full stop,maelezo mareefu hadithi nyingiiii,sasa umemwanisha nani.nyinyi ngojeni tu,siku zinahesabika.
 
Mheshimiwa mbunge maelezo yako yamesomeka, lakini jinsi unavyoonyesha inatupa picha fulani sio nzuri.
1. Wewe si mtendaji wa kila siku wa kampuni, hivyo huwezi kujua katika kazi za kila siku nini kinafanyika.
2. Kama kampuni kuna msemaji, ambaye naamini si wewe. ingekuwa hekima sana pamoja na kutuhumiwa wewe lakini umetuhumiwa kupitia kampuni hivyo ingekuwa ni vizuri msemaji wa kampuni kusema hayo tena kwa vithibitisho na list halali na sio tu kwa maneno.
3. Kama ni uongo kwa nini unakubali kila siku kusamehe bila kwenda mahakamani?. Unapaswa kuwashitaki hao ili wathibitishe madai yao nawe uthibitishe madai yako mbele ya vyombo vya sheria.

Kwa kusema hivyo, Bado haujaondoa doa katika akili za wasomaji wa ile taarifa kwa taarifa hii. Na unapaswa kwenda mbali zaidi ya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…