Majibu ya DNA yanavyowasababishia matatizo Maafisa Ustawi wa Jamii

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Licha ya kipimo cha vinasaba kuwa uthibitisho wa mwisho kwa wazazi wanaotaka kuthibitisha uhalali kwa watoto, mara kadhaa maofisa ustawi wa jamii huingia kwenye lawama majibu yanapotoka.

Hayo yameelezwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam, Namara Elisha wakati wa mafunzo ya maofisa ustawi wa jamii juu uelewa wa sheria ya vinasaba yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Elisha ameeleza kuwa mara kadhaa migogoro ya wazazi inapofikia kuhitaji ulazima wa kufanyika kwa kipimo hicho wapo ambao hukataa kukubaliana na majibu.

“Hii ni changamoto ambayo tunakutana nayo utakuta ili kupata suluhu ya mgogoro ni lazima kifanyike kipimo na wenyewe wanaridhia lakini majibu yanapotoka, wanakataa kuyakubali.

“Hapo ndipo tunapoingizwa kwenye lawama maofisa ustawi wa jamii kwamba tunahusika kutengeneza majibu yaegemee upande mmoja, tunakabiliana na hili kwa kuzungumza nao ndio maana mafunzo haya kwetu ni muhimu,”amesema Elisha.

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko amesema maofisa ustawi wa jamii wana wajibu wa kujua kwa undani kuhusu kipimo cha vinasaba kwa kuwa ni mojawapo ya eneo wanalokumbana nalo kwenye usuluhishi wa migogoro.

“Hili ni kundi linalojibu maswali kwenye jamii hivyo ni muhimu kwao kufahamu utaratibu wa kuomba kipimo cha vinasaba, kujua vinavyofanyika na mlolongo wake hivyo ni muhimu kwao kujua.

Ni kundi linalopaswa kupewa maelezo ya kina kuhusu mnyororo mzima wa kipimo cha vinasaba unavyofanyika na utaratibu wa uchukuaji matokeo maana maswali ni mengi huko,” amesema Dk Mafumiko.

MWANANCHI
 
Waache kupokea rushwa ili wapindishe ukweli wa majibu halisi.
 
Elimu ya nini mnawadekeza wenyewe bhana wao wametaka kupima kuwa hawaaminiani mnategemea majibu yakionyesha mtoto ni wa baba na huyo mama lazima mwenye kusababisha kuja hapo atayakataa ..kutoa Elimu ni kuwadekeza wekeni desk la kulipa na kupokea majibu waende na majibu yao huko...
 
Licha ya kipimo cha vinasaba kuwa uthibitisho wa mwisho kwa wazazi wanaotaka kuthibitisha uhalali kwa watoto, mara kadhaa maofisa ustawi wa jamii huingia kwenye lawama majibu yanapotoka.

Hayo yameelezwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam, Namara Elisha wakati wa mafunzo ya maofisa ustawi wa jamii juu uelewa wa sheria ya vinasaba yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Elisha ameeleza kuwa mara kadhaa migogoro ya wazazi inapofikia kuhitaji ulazima wa kufanyika kwa kipimo hicho wapo ambao hukataa kukubaliana na majibu.

“Hii ni changamoto ambayo tunakutana nayo utakuta ili kupata suluhu ya mgogoro ni lazima kifanyike kipimo na wenyewe wanaridhia lakini majibu yanapotoka, wanakataa kuyakubali.

“Hapo ndipo tunapoingizwa kwenye lawama maofisa ustawi wa jamii kwamba tunahusika kutengeneza majibu yaegemee upande mmoja, tunakabiliana na hili kwa kuzungumza nao ndio maana mafunzo haya kwetu ni muhimu,”amesema Elisha.

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko amesema maofisa ustawi wa jamii wana wajibu wa kujua kwa undani kuhusu kipimo cha vinasaba kwa kuwa ni mojawapo ya eneo wanalokumbana nalo kwenye usuluhishi wa migogoro.

“Hili ni kundi linalojibu maswali kwenye jamii hivyo ni muhimu kwao kufahamu utaratibu wa kuomba kipimo cha vinasaba, kujua vinavyofanyika na mlolongo wake hivyo ni muhimu kwao kujua.

Ni kundi linalopaswa kupewa maelezo ya kina kuhusu mnyororo mzima wa kipimo cha vinasaba unavyofanyika na utaratibu wa uchukuaji matokeo maana maswali ni mengi huko,” amesema Dk Mafumiko.

MWANANCHI
Dawa ni kuwaambia waache uzinzi na kubambikiziana watoto.
 
Back
Top Bottom