Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Mbona amejibu hayo mawili aliyopelekewa mwenye pm tu na ameacha kujibu kero nyingi nyingine zilizoadikwa hata kwenye ile thread yake ya kushukuru kukaribishwa? Mfano mmoja ni kero ya barabara kufungwa kwa watu kuziba barabara kinyume na sheria kule sehemu za Jangwani Beach; kitu kinachosababisha mafuriko/ maradhi nyumbani mwa watu wakati wa mvua!!! Waziri shuhurikia kero hizi ingawa hazina mshiko kama mradi wa Kigamboni.
 
Mheshimiwa,

Naomba niulize swali moja dogo tu kupanga miji kisheria na kuweka utaratibu wa kutaka activities fulani zifanyike na zengine zifanyike kule kunahitaji gharama kiasi gani? Mfano jiji la Dar-es-Salaam ambalo halina plan ya msingi mnashindwa kweli kuwaambia wakaazi wa kariakoo mfano kufanya biashara zao maeneo ya ilala na magomeni kuondoa foleni mjini. Mkaishinikiza serikali ofisi zake za mawaziri na taasisi zengine isipokuwa TRA, Bandari na Benki Kuu zikabakia mjini nyengine zote zikahamia maeneo ya mwenge, ubungo na manzese kusambaza vitega uchumi maeneo hayo? Finally mjini kukabadilishwa na kuwa na taasisi za kifedha, mahoteli, shopping malls tu ili kupunguza foleni na vile vile kuleta urban tourism.

Kama ni ngumu sana basi tuajiri sie tukushauri vp ufanye ili kuleta faida ya taifa letu na maendeleo kwa ujumla.

Uko sawa sana mkuu. Maana magari yangekuwa yanapishana tu, wa Mwenge wanaenda ofisini kwao Temeke wa Ilala wanaenda Gongolamboto wa Mbagala wanaenda Ilala kwa mujibu wa maeneo yao ya kazi. Foleni ingelipungua sana. Hata ghivyo, yote tutazunguuka, shortest way ni kwamba CCM wamefika critical point ya kufanya jambo lolote, hawashauriki hata iweje. Kama kuna Wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake na watoto; kuna Polisi, mgambo na kila upuuzi then kinachowafanya kushindwa kuwakamata watoto wadogo wanaokaa barabarani na kuomba ili wawarudishe kwao au wale wahitaji wa kweli wawarudishe shuleni unadhani hii serikali itaweza nini zaidi. Sasa jiulize ni maendeleo gani ya jamii, ni wanawake gani wanaosaidiwa ikiwa wwenyewe wanajifungulia majiani, ni watoto gani wanaowahudumia ikiwa wenye shida za kweli wanawapita barabarani na magari yao wakiomba.
 
wewe umejuaje kuwa linaweza kuanguka siku yoyote kwani jengo linaongea kwamba ulizungumza nalo au umetumia vigezo gani kusema jengo litaanguka wakati wowote jaribu kufafanua kwani unaweza ukaona jengo linaufa mkubwa tu halafu likakaa miaka hata kumi bila kuanguka.

Wewe bila shaka sakata la hili jengo umedandia leo. Nakushauri rejea kwenye threads na maelezo ya siku za nyuma kuhusu hili jengo na kwanini uamuzi ukachukuliwa kuwa libomolewa! BTW majengo huwa yanazungumza na kutoa taarifa yanapotaka kuanguka? Halafu in the worst-case scenario unatetea nadharia ya ''jengo lenye ufa kuweza kukaa miaka kumi bila kuanguka'' kwa sababu halijatoa taarifa kuwa litaanguka!!! What a joke!
 
Mimi siyo mwanasheria. Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

According to kauli mbiu ya PM ya 'piga tu' wanaokiuka sheria it seems kwa upande huu mama Tibaijuka alitakiwa 'abomoe tu'. Kama mtoa hukumu ni mahakama kwa nini serikali hiyohiyo itoe tamko la kuruhusu vyombo nje ya mahakama kuhukumu wahalifu? Tena ingefaa kuanzia sasa wananchi nao wakithibitisha mtu yeyote kafanya uhalifu mfano ufisadi wamshughulikie hapohapo. Mahakama zimefutwa na PM
 
mama tibaijuka, kidumu chama cha mapinduzi. Nikupe ongera kwa ujasili wako wa kuja kutolea majibu humu jukwaani, ukizingatia kwa vuguvugu la ushindani lilivyo kwa sasa, nikupe hongera.

Lakini kuhusu jengo pale mtaa wa indra gadhi, posta. Sidhani kama pingamizi lililo tolewa lina tija, ukizingatia hali ya usalama kwa wakazi wa eneo husika bado si shwari, watu hawana amani na wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru.

Mimi nadhani jengo livunjwe haraka iwezekanavyo, harafu mahakama kuu kama chombo cha kusimamia na kutoa haki, tuone itahamua nini. Haya ni maisha ya watanzania tunayangelea hapa, hatuwezi kuendelea kuyahatarisha kwa pingamizi la mtu mmoja au kikundi cha watu kwa kulinda maslahi yao.

hata ukisema kidumu buku saba hupati
 
Ningelishangaa kama angelijibu kwa ufasaha na walau robo ya maswali aliyoulizwa jukwaani, lakini kwa jinsi alivyojibu ni kwamba ndiyo staili ya kujibu maswali hiyo ya wana CCM. Badala ya kujibu maswali ya Jukwaani unaenda kujibu ya private messages ambayo nayo hayakupata majibu ya kuridhisha. Kuna member walimtahadharisha humu kuwa asije kujibu kwa ile staili yao ya kibungeni-bungeni, yaleyaleeeeeeee
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.

  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.

Samahani mkuu Anna Tibaijuka, nijuavyo mimi Sheria za JF haziruhusu mambo ya private kuyaleta jukwaani. Pamoja na kuwa umefanya kwa nia njema, ningesuggest Invisible akupe BAN kama ya siku tatu tu. Asante
 
Last edited by a moderator:
Uko sawa sana mkuu. Maana magari yangekuwa yanapishana tu, wa Mwenge wanaenda ofisini kwao Temeke wa Ilala wanaenda Gongolamboto wa Mbagala wanaenda Ilala kwa mujibu wa maeneo yao ya kazi. Foleni ingelipungua sana. Hata ghivyo, yote tutazunguuka, shortest way ni kwamba CCM wamefika critical point ya kufanya jambo lolote, hawashauriki hata iweje. Kama kuna Wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake na watoto; kuna Polisi, mgambo na kila upuuzi then kinachowafanya kushindwa kuwakamata watoto wadogo wanaokaa barabarani na kuomba ili wawarudishe kwao au wale wahitaji wa kweli wawarudishe shuleni unadhani hii serikali itaweza nini zaidi. Sasa jiulize ni maendeleo gani ya jamii, ni wanawake gani wanaosaidiwa ikiwa wwenyewe wanajifungulia majiani, ni watoto gani wanaowahudumia ikiwa wenye shida za kweli wanawapita barabarani na magari yao wakiomba.

kweli kuwa na akili ni jambo moja na kutumia akili ni jambo lingine umejaribu kufuatilia hao watoto unaosema wakamatwe unauhakika wote wanakwao na wote wanawazazi wao.

kwa taarifa yako watoto wengi unaowaona dar wengine hata wazazi hawana na wengine hawawajui baada ya kutelekezwa wakiwa wadogo sana .

Mbona hujapendekeza hawa watoto wakirudishwa kwao watalindweje ili wasije mjini tena tulia tafakari majibu utayapata nadhani wewe ni mtu mzima kiasi.
 
Samahani mkuu Anna Tibaijuka, nijuavyo mimi Sheria za JF haziruhusu mambo ya private kuyaleta jukwaani. Pamoja na kuwa umefanya kwa nia njema, ningesuggest Invisible akupe BAN kama ya siku tatu tu. Asante

kafanya hivyo kwa manufaa ya wengine pia ili wanufaike kumbuka huyu ni waziri na yote anayofanya ni kwa manufaa ya taifa.wewe umepata shida gani zaidi ya kunufaika.
 
Wewe bila shaka sakata la hili jengo umedandia leo. Nakushauri rejea kwenye threads na maelezo ya siku za nyuma kuhusu hili jengo na kwanini uamuzi ukachukuliwa kuwa libomolewa! BTW majengo huwa yanazungumza na kutoa taarifa yanapotaka kuanguka? Halafu in the worst-case scenario unatetea nadharia ya ''jengo lenye ufa kuweza kukaa miaka kumi bila kuanguka'' kwa sababu halijatoa taarifa kuwa litaanguka!!! What a joke!

mkuu mimi shida yangu ilikuwa pale ulipo sema kwamba jengo linaweza kuanguka hata kesho hizo na nadharia tu kisheria hazina msingi wowote,madamu swala hili lipo mahakamani taratibu zote za kisheria na kimahakama lazima zifuatwe na si vinginevyo.
 
Navunjaaaaa (in mama Tibaijuka's tone)
Wakuu tunapaswa kumpongeza mama kwa ushujaa wa kuja humu badala ya kumpa majibu ya kebehi kumbukeni kuna mawaziri wengi sana viraza kama Mulugo,Kawambwa,Wasira,Lukuvi nk ambao hawawezi kuja humu ndani mama tafadhali jibu na maswali mengine uliyoulizwa humu ndani
 
kinachowafanya kushindwa kuwakamata watoto wadogo wanaokaa barabarani na kuomba ili wawarudishe kwao au wale wahitaji wa kweli wawarudishe shuleni

kweli kuwa na akili ni jambo moja na kutumia akili ni jambo lingine umejaribu kufuatilia hao watoto unaosema wakamatwe unauhakika wote wanakwao na wote wanawazazi wao.

kwa taarifa yako watoto wengi unaowaona dar wengine hata wazazi hawana na wengine hawawajui baada ya kutelekezwa wakiwa wadogo sana .

Mbona hujapendekeza hawa watoto wakirudishwa kwao watalindweje ili wasije mjini tena tulia tafakari majibu utayapata nadhani wewe ni mtu mzima kiasi.

Umeamua kupotosha au umeshindwa kuelewa nilichoandika? Kuna watoto wanaandamana na watu wazima katika kuomba (sijui kama ni watoto wao halisi au wanawatumia), kuna wengine wapo peke yao. Nilichoshauri ni kwamba hao watoto baada ya kuwakamata watafute sababu za kufanya wanayofanya, kwa wale ambao wana wazazi au walezi basi wawarudishe kwa wazai wao na ikibidi wawashtaki wazazi na wale ambao ni wahitaji wa kweli (wana maisha ya dhiki kweli na hawana wazazi/walezi wa kuwasaidia) Serikali/Wizara ya MJWW ibebe jukumu la kuwapeleka shule kwa gharama za serikali, kwani siamini kwamba Serikali/Wizara haina shule za bweni kwa watoto walio katika mazingira magumu kama hao(Ni suala linalowezekana kwa Serikali kujenga japo shule moja ya bweni kwa kila Wilaya kuanzia ngazi ya Primari hadi Sekondari ambapo watoto kama haowangekuwa wankusanywa na kupelekwa huku kuchukua juhudi za makusudi kuzuia hali hizo zisiendelee). Jamani sio lazima kuitetea Serikali au watendaji wake hata pale wanapokosea, au wanaposhindwa kutekeleza jukumu lao kwa wananchi. Ikifanya vema tutaisifia na ikikosea tutaikosoa kwani sisi wengine ni Watanzania wazalendo hatusukumwi na vyama wala itikadi katika kufanya haya kwa sababu tunaona madhara ya kuwa na Taifa masikini hususan ukiwa kwenye hizi nchi za wenzetu zilizoendelea, wanatuona sie kama wanyama pamoja na kufanya kazi vizuri kuliko wao, simply kwa kuwa tunatoka huko kwenye umaskini unaosababishwa na hao viongozi mnaowatetea kila uchao
 
mkuu mimi shida yangu ilikuwa pale ulipo sema kwamba jengo linaweza kuanguka hata kesho hizo na nadharia tu kisheria hazina msingi wowote,madamu swala hili lipo mahakamani taratibu zote za kisheria na kimahakama lazima zifuatwe na si vinginevyo.

Mkuu, ukishasema ''jengo limejengwa chini ya kiwango'', ni kwamba linaweza kuanguka sekunde mbili zijazo, au siku tatu zijazo, au mwaka mmoja na nusu ujao, au miaka kumi ijayo au lisianguke kabisa. Sasa basi, kwa kuwa hatujui litaanguka lini inabidi kujihami mara moja! na kumbuka mimi nimesema (kama ulivyoninukuu) ''LINAWEZA KUANGUKA''. Sasa kitaalamu kitu cha hatari chenye probability (likelihood) ya kutokea hatuwezi kukaa tu na ''kutegemea'' kuwa hakitatokea kama tuna mbinu za kukiepusha! Tuko pamoja!
 
Ahsante
mama japo umejibu kwa bla bla,suala la kubomoa ghorofa halihitaji
usubiri hukumu ya mahakama we unatakiwa ufanye kazi zako kwa kufuata
sheria.kiujumla serikali imelemewa na mafisadi mmebaki kuwaonea na kuwagandamiza wananchi wa chini wasio na feha.mama kwakuwa we ni mjumbe wa cc ya ccm utakapokuja kujibu maswali mengine nami naomba utueleze chama kina mpango gani wa kuwawajibisha mwigulu,Nape,na wasira kwa kuendesha siasa za kimafia na kibaguzi nchini.

Nilitegemea ungempa support professor kwa kuja hapa kutoa majibu. Hakuna aliye juu ya sheria, hivyo kama kuna zuio la mahakama hakuna budi kusubiri kesi hiyo iishe.
 
Kama viongozi wengine wa umma watakuwa na utaratibu km wa mh. Tibaijuka wa kujitokeza kwenye mitandao hususan huu wa jf kufafana baadhi ya mambo yanayohusu utendaji wao itakuwa safi sana
 
Mimi siyo mwanasheria. Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Waziri hakutakiwa kutangaza.. Siku ya kubomoa ndiyo mhusika anapata taarifa, tena kazi ikiwa imeanza..
 
Samahani mkuu Anna Tibaijuka, nijuavyo mimi Sheria za JF haziruhusu mambo ya private kuyaleta jukwaani. Pamoja na kuwa umefanya kwa nia njema, ningesuggest Invisible akupe BAN kama ya siku tatu tu. Asante

Anna Tibaijuka,Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

Hastahili ban wala lawama!... Meseji za Siri atajibu bilaterally, "siyo kwenye public" .... Amenijibu nimeridhika.
 
Back
Top Bottom