Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Nchi yetu inamkosi sana. Inabidi tuje tuitambikie kabisa. Huwezi kuamini haya yanayotokea. Hata wale tunaowaona kuwa Ni wasomi na exposure nzuri nao wanatuletea ubabaishaji tu. Mtu yeyote makini hawezi kuleta mambo ya photoshop hapa. Ni kama vile sisi tunalilia pipi. Hatuhitaji kulambishwa pipi. Either unakuja na majibu yote na yaliyotimia or you vanish. Hakuna atakayekulaumu. Watanzania wengi tumeishi kwa matumaini kwa muda mrefu sana mpaka tunazeeka sasa. Bla bla hizi zinaudhi sana.
 
Kigamboni New City na Karume Satelite city zinaanza lini? Wenzetu wakenya washaanza city yao na fly over juu.
 
Ahsante
mama japo umejibu kwa bla bla,suala la kubomoa ghorofa halihitaji
usubiri hukumu ya mahakama we unatakiwa ufanye kazi zako kwa kufuata
sheria.kiujumla serikali imelemewa na mafisadi mmebaki kuwaonea na kuwagandamiza wananchi wa chini wasio na feha.mama kwakuwa we ni mjumbe wa cc ya ccm utakapokuja kujibu maswali mengine nami naomba utueleze chama kina mpango gani wa kuwawajibisha mwigulu,Nape,na wasira kwa kuendesha siasa za kimafia na kibaguzi nchini.

Ndg ni bora ukatumia nafasi adimu kumuuliza maswali mhe waziri ambayo atayajibu tena yawe na heshima sio unaanza na kumwambia majibu ya bla bla huu ni utovu wa adabu na wala sio madhumuni ya JF. Huyu ni profesa ameshaaminiwa na UN sasa yeye kuwa waziri wa CCM isiwe shida kumpa sifa zake stahiki.

Kumbuka Tanzania inafuata sheria na kutii amri ya mahakama ni sehemu ya democrasia vinginevyo tusingekuwa na mahakama basi. Hayo ya akina mwigulu anzisha uzi mwingine sisi tutayakujibu na sivyo unavyofanya kuuliza swali ndani ya majibu.
 
Eti mama yangu mpendwa kuna wale waarabu wanaonunua maeneo kigamboni na kuwalipa watu fidia wenye ofisi yao pale mtaa wa samora,ni wewe ndio umewatuma?,manake wanadai kuna cheque yao kuubwa na yenye sifuri nyiiingi wanayoitegemea kutoka wizara yako ,tena nasikia kuna baadhi ya wapimaji wako wameshapewa na magari kwa kazi nzuri waliyoifanya.
 
Mheshimiwa waziri ukipata nafasi naomba unijibu hili.
Mheshimiwa mbunge mwenzenu kada wa CCM, Bwana JUMA NKAMIA alisema kwenye mahojiano na televisheni ya Taifa TBC1 kuwa mtandao wa JF ufutwe kwani ni mtandao ambao hauna sifa ya kuitwa mtandao wa kijamii kwani unaandika uwongo na mambo ya kufikirika na utashi wa mtu.
Mheshimiwa wewe ni member wa JF, unafikiri alichosema kada huyo ni sahihi? nini ushauri wako kweke?

nitakutoa lunch ofisin kesho..
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.

  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.

Jengo hatarishi linasubiri court injunction? profesa hutakiwi kufikiri hivi, court injunction iko na muujiza gani kuzuia jengo lisianguke, hii inathibitisha mama the elites wamekuweka mfukoni vizuri tu.
 
Ndg ni bora ukatumia nafasi adimu kumuuliza maswali mhe waziri ambayo atayajibu tena yawe na heshima sio unaanza na kumwambia majibu ya bla bla huu ni utovu wa adabu na wala sio madhumuni ya JF. Huyu ni profesa ameshaaminiwa na UN sasa yeye kuwa waziri wa CCM isiwe shida kumpa sifa zake stahiki.

Kumbuka Tanzania inafuata sheria na kutii amri ya mahakama ni sehemu ya democrasia vinginevyo tusingekuwa na mahakama basi. Hayo ya akina mwigulu anzisha uzi mwingine sisi tutayakujibu na sivyo unavyofanya kuuliza swali ndani ya majibu.

unachekesha hii ni sawa kumkamata gaidi amevaa milipuko mnamuacha kwa sababu mwanasheria wake ameweka pingamizi mahakamani, huitaji kuwa profesa kudharau court injunction ya namna hii. hapa napata hisia mama anauzika.
 
Mama kalainishwa na mafisadi hana lolote, ni mpuuzi kama majibu yake, kawa mwanasiasa na wanasiasa wote wa hizi nchi masikini ni wapuuzi hata wakiwa ma Dr/Prof
Amani vs Vita ndio kamba waliyobaki nao magamba!

TENA NINASIKIA SIKU HIZI KILA GOROFA LInalojengwa wenye jengo Huwa wanatakiwa kutoa vyumba kuwapatia wakubwa au wake wakubwa, ndio Maana wenye magorofa huwa wanauawa kuzidisha magorofa Kwenda juu ILI kukidhi mahitaji na matokea yake viwango duni, Tafadhali mama acheni oneni huruma! Jengo lililoporomoka ndivyo ilivyokuwa!
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.

  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.
kuhusu kubomoa gorofa,tutaendelea kudanganywa sana

kwa maana aliyejenga naye kafata taratibu zilizopo ndo mana wapo wote mahakamani yan serikeli na mmiliki

so MH.tibaijuka usitutupie mchanga machoni alafu baada uje kusema tumeshindwa kesi kutokana na mgongano wa kisheria

kubali wenye hela ndio wenye nchi,na huwezi kubomoa hilo jengo hata kama sheria imekiukwa

alafu ninaomba na kukukumbusha kufuata taratibu na sheria ya mahali na kitu chochote,

kutofuatwa na kutotii sheria ndio mnatujengea hayo magorofa vimeo

sasa fuata sheria za JF kama unataka kuwa mwanaJF
 
Ndg ni bora ukatumia nafasi adimu kumuuliza maswali mhe waziri ambayo atayajibu tena yawe na heshima sio unaanza na kumwambia majibu ya bla bla huu ni utovu wa adabu na wala sio madhumuni ya JF. Huyu ni profesa ameshaaminiwa na UN sasa yeye kuwa waziri wa CCM isiwe shida kumpa sifa zake stahiki.

Kumbuka Tanzania inafuata sheria na kutii amri ya mahakama ni sehemu ya democrasia vinginevyo tusingekuwa na mahakama basi. Hayo ya akina mwigulu anzisha uzi mwingine sisi tutayakujibu na sivyo unavyofanya kuuliza swali ndani ya majibu.

Ndg ni bora ukatumia nafasi adimu kumuuliza maswali mhe waziri ambayo atayajibu tena yawe na heshima sio unaanza na kumwambia majibu ya bla bla huu ni utovu wa adabu na wala sio madhumuni ya JF.
Hakuna kumhusudu kiongozi anayetuongoza kwenye majanga kila mara,na ataambiwe neno lolote linalomfaa kwa jibu analotoa
Huyu ni profesa ameshaaminiwa na UN sasa yeye kuwa waziri wa CCM isiwe shida kumpa sifa zake stahiki.
mkuu tibaijuka kufanya kazi UN isikupe kimuhemuhe kwamba katika wizara anayoongoza yupo makini kwa kila jambo,
mana yeye ni bimadamu na anatafuta pesa..........
Kumbuka Tanzania inafuata sheria na kutii amri ya mahakama ni sehemu ya democrasia vinginevyo tusingekuwa na mahakama basi.
Ndo mtugengee hayo magorofa ya kipuuzi?demokrasia gani unayoiona apa TZ au ndo ya KUPIGA TU?Je mahakana imeona?
 
Prof Tibaijuka habari , Naomba nianze na swala la ubora wa maghorofa, inasikitisha sana kusikia kutoka kwa waziri msomi tena prof kuwa na kigugumizi kwa majengo ambayo ni bomu linalongoja kulipuka. Tangia orodha zaidi ya majengo 100 hatari kuporomoka Dar kutolewa na amri ya kuyavunja kutolewa hakuna linalotokea zaidi ya longolongo zenye mazingira ya kushindwa kazi, ujuana matumizi ya rushwa au udhaifu wa serikali yote. Nasema haya kwa uchungu kwani mnakurupuka pale tu madhara yanapotokea badala ya kuzuia. Haiingi akilini kama kweli ulijua yale majengo yako kwenye hatari ya kuanguka na kuuwa watanzania masikini wasio na hatia wala uwezo. Ukiwa waziri mwenye dhamana kama kweli bila shaka unauhakika kutokana na wataalamu kwamba yale majengo yana weza kuleta madhara pamoja na kuanguaka sioni ni kwanini hayavunjwi. Kama mnafanya kazi kwa kuzingatia sharia, taratibu, utaalamu na viwango kulikuwa hakuna kesi ya kujibu zaidi ya kuvunjwa. Swala la mji wa kigamboni kupimwa kwa ajili ya maendeleo ni swala zuri sana. Ila sioni kama mlizingatia kwa ukweli kuifanya Tanzania kuwa na miji ya kisasa. Kwa uchumi tulionao ingekuwa ni vyema kupima sehemu ambazo bado hazijaendelezwa ambazo ziko nyingi sana wakati tukizuia ujenga holela kigamboni badala ya kuanza kulipa mabilioni ya fedha ambayo tungeweza kuwa na miji ya kisasa mikubwa mingi na mizuri na kurudi Kigamboni pale uchumi utakapokubali.
 
Anna Tibaijuka,

I am sorry to say this, but bora hata usingeweka hii thread, na pengine hata uwepo wako hapa JF hautusaidii kwa lolote. Pengine kama unaipenda sana JF ungeingia kwa ID ya kujificha tukawa tunagongana kwenye forums mbalimbali, but sio kama Anna Tibaijuka.

Pengine tusikuone tena baada ya haya majibu yako mawili mpaka baada ya miezi miwili. Hii style haikusaidii wewe wala sisi.

Na labda tu kwa tabia uliyoionyesha kipindi hiki kifupi ulichokuwepo JF kinafanya tukufikirie kumbe na wewe "ndio walewale" tu
 
Last edited by a moderator:

Hakuna kumhusudu kiongozi anayetuongoza kwenye majanga kila mara,na ataambiwe neno lolote linalomfaa kwa jibu analotoa

mkuu tibaijuka kufanya kazi UN isikupe kimuhemuhe kwamba katika wizara anayoongoza yupo makini kwa kila jambo,
mana yeye ni bimadamu na anatafuta pesa..........

Ndo mtugengee hayo magorofa ya kipuuzi?demokrasia gani unayoiona apa TZ au ndo ya KUPIGA TU?Je mahakana imeona?

Kinachotakiwa ni mahakama kuangalia hatari iliyopo na kutoa maamuzi haraka lakini si waziri aingilie mahakama. Hiyo ndio tatizo la utawala wa sheria mnaoulilia hapa JF nashangaa leo mnataka waziri awe dikteta.

Tuache chuki zisizo na tija kwa taifa mwacheni mama ajenge taifa
 
Back
Top Bottom