Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Wanamtandao

Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction.
Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha.

Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.

Safi!... Tukienda hivi siasa si chuki, bali maelewano. Ukiulizwa jibu. Huo ndio mwendo.. Kila la Kheri mamaa!...
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.


  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.
Hongera sana mheshimiwa waziri, japo utapata watu wachache sana wa kukuelewa kwa vile wengi humu wameweka mbele siasa na kuukana ukweli kama huu na matokeo yake ni matusi na hili labda ni kwa sababu pia ya watu kutokuwa na hoja katika mada mbalimbali , tatizo linalotokana na uelewa mdogo wa masula ya kitaifa na kimataifa . HOngera tena mheshimiwa waziri wewe ni mfano wa kuigwa .
 
Prof shikamoo,napenda tu kukupongeza kwa uonesha utofauti na wanaccm wenzako ambao wamejificha na hawawi wazi kwenye mitandao ambayo kwa sasa habari nyingi huwekwa iwe ya kweli au la,maisha marefu mama.
wanamtandao

ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. private messages ya tayadi, tarehe 11 juni
kazi unaweza saaana!,, lakini kwa hili la ghorofa, mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama tibaijuka mfukoni. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

jibu. asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo mahakama kuu, kitengo cha ardhi, miscellaneous land application no. 42 of 2013. Tarehe 31 mei, 2013, mhe jaji j.s. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya bw. Mashauri, mwanasheria wa halmashauri ya ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la bi. Rachel, mwanasheria wa mwekezaji (ali raza investments ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo mahakamani. Tusubiri.


  1. private message ya amani ndoyella, ya 11 juni, 2013
ujumbe wako kuhusu mradi wa mji mpya wa kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara kigamboni miwili, mbali na kukutana na kamati ya madiwani, wabunge, na hata kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika kda, wakala wa serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za kda ziko huko huko kigamboni. Mkurugenzi wake bw. Vincent shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka singapore, kwenye ziara ya mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu master plan ya mji mpya wa singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo dar es salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la jf. Kwa hiyo kuhusu kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa kibada unaendelea. Madai ya shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.
 
Serikali imechuka hatua gani kwa maonevu yaliyotokea tegeta kata ya madale maeneo ya kazaroho,nakarekwa,na nakasagwe? sababu wale walio vunjiwa nyumba bado wanahangaika hawana pa kuishi. naomba jibu mama Anna Tibaijuka. mia
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru Mama Anna Tibaijuka kwa kutujuza yale yanayoendelea kuhusiana na AMRI uliyoitoa ili jengo libomolewe.

Hii ndiyo nguvu ya mawasiliano katika dunia ya sasa ambapo sentensi ya mistari SITA inayochukua less than two minutes kuiandika imeondoa SINTONFAHAMU iliyokuwa inaelea hewani kwa muda kuhusiana kile kilichoko nyuma ya jengo kutobomolewa.

Jaribu kuwashauri na watendaji wengine wa chama na serikali hasa mawaziri kujiunga na Jamiiforums ( JF) ili wasogee karibu kwa wananchi katika kupashana habari na kuelimishana.

Apo umejuzwa tu, mkuu kwani kujuza mtu kitu kisiasa ni kazi kubwa?

Ishu watu wakuelewe unachosema..wewe naona umekuwa mrahisi kukubaliana na siasa za Anna..
 
Ahsante
mama japo umejibu kwa bla bla,suala la kubomoa ghorofa halihitaji
usubiri hukumu ya mahakama we unatakiwa ufanye kazi zako kwa kufuata
sheria.kiujumla serikali imelemewa na mafisadi mmebaki kuwaonea na kuwagandamiza wananchi wa chini wasio na feha.mama kwakuwa we ni mjumbe wa cc ya ccm utakapokuja kujibu maswali mengine nami naomba utueleze chama kina mpango gani wa kuwawajibisha mwigulu,Nape,na wasira kwa kuendesha siasa za kimafia na kibaguzi nchini.

Kufuata sheria ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola. Sasa wewe unataka mama aanze kupingana na mahakama? umbulurura nao mbaya sana!
 
Mama Tibaijuka, kidumu chama cha mapinduzi. Nikupe ongera kwa ujasili wako wa kuja kutolea majibu humu jukwaani, ukizingatia kwa vuguvugu la ushindani lilivyo kwa sasa, nikupe hongera.

Lakini kuhusu jengo pale mtaa wa Indra Gadhi, Posta. Sidhani kama pingamizi lililo tolewa lina tija, ukizingatia hali ya usalama kwa wakazi wa eneo husika bado si shwari, watu hawana amani na wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru.

Mimi nadhani jengo livunjwe haraka iwezekanavyo, harafu mahakama kuu kama chombo cha kusimamia na kutoa haki, tuone itahamua nini. Haya ni maisha ya watanzania tunayangelea hapa, hatuwezi kuendelea kuyahatarisha kwa pingamizi la mtu mmoja au kikundi cha watu kwa kulinda maslahi yao.

unaposema kidumu chama cha mapinduzi unamaanisha nini hasa kwenye uzi kama huu ? Au wewe ni Mapuri nini ?
 
uliulizwa maswali mengi sana ya msingi , likiwemo swali langu , nasikitika kwamba sitalirudia , kwanini umeamua kujibu haya mepesi sana kuliko yote ?
 
Kufuata sheria ni
pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola. Sasa wewe unataka mama
aanze kupingana na mahakama? umbulurura nao mbaya sana!

hivi kwa akili yako mahakama itasaidiaje jengo lisporomoke na kugharimu maisha ya watu? jengo limejengwa chini ya viwango na sheria ziko wazi.
 
Mheshimiwa, japo umechelewa kujibu, lakini afadhali wewe umejitahidi. Waswahili walisema heri kenda kuliko kumi nenda uje! Endelea na utaratibu huu wa kujibu maswali ya wana JF, lakini ongeza spindi ya kuyajibu. Hongera
 
Asante mama,lkn naomba kujua nini mtazamo wako kuhusu mapambano ya polisi dhidi ya wamachinga ktk miji yetu hapa nchini
 
kwanza nakupongeza kwa ujasiri uliouonyesha wa kurudi na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo lakini kuna maswali bado yananitatiza 1.Kama mliweza kubomoa uzio pale palm beach pamoja na mmiliki kukimbilia mahakamani mnashindwa nini sasa hivi 2.Kama wameweka court injuction ni vizuri mkaweka sheria kwamba baada ya muda fulani maamuzi yawe yameshatolewa kwa sababu kuna rushwa kubwa mahakamani ndio maana wakati mwingine mnaonekana kama hamfanyi kazi mtindo huo pia umetumiwa na mbunge wa viti maalumu ili asibomolewe nyumba yake 3.Kwa wakazi wakigamboni ni vizuri msiwalipe fidia ila watumie hati yao kuingia ubia na wawekeza arhi yake ndio iwe hisa yake 4.Hivi kweli imeshindikana makampuni yetu kujenga huo mji mpaka zipewe kampuni za nje hamuoni kuwa tuna wadhalilisha wasomi wetu na vyuo vyetu au ni 10%
 
uliulizwa maswali mengi sana ya msingi , likiwemo swali langu , nasikitika kwamba sitalirudia , kwanini umeamua kujibu haya mepesi sana kuliko yote ?

Umeshaambiwa utajibiwa wewe kuwa na subira halafu hiyo tabia ya kuona kwamba swali lako ndiyo la msingi/maana/zito kuliko ya wenzako ni dalili ya ubinafsi.

Hatutaweza kuijenga nchi yetu nzuri ya Tanzania kama nchi yetu itakuwa na watu wabinafsi.
 
Ndiyo umejibu nini sasa. Kati ya hoja nyingi zilizoulizwa kweli Unakuwa na majibu mawili tu? Hivi hammnaga wasaidizi? Nilitegemea timu yako ingekaa ikafanya research nakutoa snap answers kwa hoja zote zilizoulizwa. Sikutegemei wewe ndo ujibu. Hawa ndiyo genius wetu! Where is your experience! Ungejikaliaga na kuwa states woman na kuishauri nnchi. Heshima yako inakuwa questioned un necessarily.
Kaka hebu soma HEADING ya huo uzi then uangalie jinsi ya kulipunguza hilo povu. Afterall hapa sio bungeni. Anastahili pongezi
 
Mimi siyo mwanasheria.
Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama
alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa
amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

magufuli mbona anaweza why yeye ashindwe?
 
umejibu maswali mawili tu tena uliyotumiwa kwa PM,
zingatia sheria za JF mtu anapokutumia private msg.

I was wondering about this. Hapa kwenye uwanja wa wazi watu walimrushia maswali mengi na mazito yanayohitaji majibu yenye kufikirisha, ameyakimbia yote, halafu anatuletea majibu ya maswali mepesi ya kutoka kwenye private messages, huku akivunja sheria za JF zinazomtaka asilete kwenye uwanja wa wazi message ambazo ni private. Siasa za namna hii mama Anna Tibaijuka hazitusaidii, tunataka ufanye kazi kwa weledi kama tunavyokufahamu na si kwa uoga wa kuhofia cheo chako iwapo utasema ukweli na kusimamia ukweli bila kuwahofia wenye fedha na viongozi wenzako ambao wanahodhi ardhi, na kuwaacha wananchi katika hali ya shida, ngumu na yenye mateso.

Tunataka utuambie ni kwanini ofisi ya ardhi inatumia zaidi ya miaka mitatu kutoa hati ya kiwanja au kupima kiwanja cha mtu? Na ni kwanini serikali inauza viwanja ilivyopima kwa bei kubwa sana ambayo wananch wa kawaida hawaiwezi? Je si ni haki ya kila mwananchi kupata kiwanja kilichopimwa? Si ni kazi ya serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anajenga na kuishi katika eneo lililopimwa? Yaani pamoja na kuwa UN habitat, bado unashindwa kabisa kufanya planning ya majiji, manispaa, miji na vijiji vya nchi hii, despite wataalamu lundo uliojaza hapo wizarani? Ndiyo maana mimi huwa nasema wewe, na Chiligati na wazembe wengine waliowahi kuongoza wizara ya ardhi hamna tofauti. Ni vile tu kwamba wewe una exposure kubwa japo haitusaidii kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom