Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Kwanza nikupongeze mama kwa kujitokeza na kujibu maswali..naomba tu unieleweshe incase mahakama itaamua jengo lisibomolewa wakati jengo linahatarisha maisha even from the look..je nyie jama wizara mtachukua hatua gani.? Incase hilo jengo likiporomoka leo na kuclaim maisha ya watu(mungu aebushe) je utakubali kuwajibika wewe pamoja na mwenye jengo,jaji pamoja na team yote inayochelewesha ubomoaji wa hili jengo?
 
Kaka hebu soma HEADING ya huo uzi then uangalie jinsi ya kulipunguza hilo povu. Afterall hapa sio bungeni. Anastahili pongezi
Watu wanafiki kama nyie ndiyo mnayekwamisha maendeleo ya nchi hii. Watu kama nyie ndiye mnayewapa vichwa viongozi wabovu kama akina mama Anna Tibaijuka kwa kuwapigia makofi hata pale wanapoongea pumba. Ina maana wewe hujaona kabisa hoja ya WCM?

Mama Tibaijuka anaulizwa, kwamba maswali yaliyoulizwa hapa yalikuwa lundo, kwanini amekuja na majibu ya maswali mawili tu tena ya kwenye private message? Kwanini hakumtuma secretary wake au katibu mkuu wake au aunde timu ipitie hoja zote za wanaJF hapa halafu azitolee maelezo ya jumla yanayojitosheleza. Kama hakuona umhimu wa kujibu hoja zote zilizoletwa na wana JF amekuja hapa kutafuta nini? Si angewajibu hao waliomuuliza hukohuko kwenye private messages? Sasa alikuwa na sababu gani ya kuja kujibu hapa ilihali maswali aliyoulizwa kwa wazi yote ameyakimbia?

Hii wizara ni moja ya wizara za JK zinazonuka rushwa sana nchini, halafu yeye anakuja na majibu ya rejareja hapa wakati watu wanamatatizo kibao. Halafu na wewe bila aibu unakuja kumtetea? Au hujui kwamba sisi ndiye tunayemlipa mshahara na hivyo tuna haki ya kuuliza utendaji wake? Kaa mbali na unafiki wako unaofifisha maendeleo ya nchi yetu.
 
HAMY-D unanishangaza kuishahuri Serkali ivunje sheria kwa kutoheshimu Amri ya Zuio iliyotolewa na Mahakama! Je utawala wa sheria una mipaka kwa kulenga watu au taasisi fulani tu?
 
Umefanya mikutano miwili katika kata mbili kati ya kata zaidi ya kumi. Chiligati alifanya mkutano mmoja akaingia mitini. Wewe ulitoa ratiba ya kufanya mikutano kata zote lakini ulipofika mkutano wa pili ukaingia mitini baada ya kushindwa kujibu maswali ya wananchi. Hamjawahi kuweza kujibu maswali ya wananchi. Huo ushirikishaji unaosema umefanyika tangu mwanzo ni upi? UN ulikuwa unafanya usanii na utapeli kama huu?

Halafu umeulizwa maswali mengi kwenye uzi, wewe unajibu DM ulizojitumia mwenyewe kwa ID zako nyingine au za watoto wako

Kuwa serious, jibu maswali na kuwa mkweli umri wako wewe mkubwa uwongo na utapeli unafundisha wajukuu zako tabia mbaya
 
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.

Asante kwa majibu mama yangu!
Neno AMANI kwenu wana CCM huwa inamaanisha nini?!
Mkoa wa Kagera ni wa ngapi kwa umaskini nchini?!
Kiwango cha Elimu kimkoa kimepandaje kwa "AMANI" tuliyonayo?
Kwa mkoa wa Kagera, ni amani ya aina gani unaisemea mbele ya Mnyauko wa MIBUNI, MIGOMBA,MIHOGO na uchache wa wananchi katika kufaidika na samaki wa Ziwa Viktoria?!
AMANI ya Tanzania inatokana na WOGA na kile kwetu tunachoita OBULUSHU!
 
Sister Anna sema leo master plan ya Arusha city imeishia wapi ? Kwa hili unalijua wazi .hapana shaka kama unalikumbuka vizuri as your fist project ata kabla ujajiunga na kugombea magamba mp .naulisema iliombea ata ufadhili habitant na ukapewe msaada .sasa kuwa huko kumekugeuza .kutoka uzalendo mpaka ufisadi wa kutowesha Arusha master plan project fund .shame on you fake iron lady .
 
Navunjaaaaa (in mama Tibaijuka's tone)
Wakuu tunapaswa kumpongeza mama kwa ushujaa wa kuja humu badala ya kumpa majibu ya kebehi kumbukeni kuna mawaziri wengi sana viraza kama Mulugo,Kawambwa,Wasira,Lukuvi nk ambao hawawezi kuja humu ndani mama tafadhali jibu na maswali mengine uliyoulizwa humu ndani
Binasi napenda kumpongeza sana mama. this is the most rare chance a mare citizen can ever have in Tanzania. waziri anajibu kero za mwananchi wa kawaida! sio Tanzania hii. mama natoa asante asante sana. mheshimiwa waziri tuna maeneo kule masaki mengi hayajaendelezwa yamekua pori. pia tuna magofu mengi ammbayo hawaishi watu. una mpango gani na hayo maeneo?
 
HAMY-D unanishangaza kuishahuri Serkali ivunje sheria kwa kutoheshimu Amri ya Zuio iliyotolewa na Mahakama! Je utawala wa sheria una mipaka kwa kulenga watu au taasisi fulani tu?

Getstart,

Uzuri sheria sio biblia wala msaafu, icho kipengele cha zuio kinaweza kufanyiwa Amendment then hatua zichukuliwe dhidi ya hilo jengo. Mkuu, mimi ni miongoni mwa watu tunao shuhudia ni namna gani wananchi wanapata shaka sana wakiwa kwenye hilo eneo.

Ina sikitisha kuona mtu mmoja tu ndiye analeta kadhia hiyo kwa wananchi. Kuna utawala wa sheria unaozidi nguvu ya umma?
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa waziri;
Hivi hakuna sheria za ku-deal na mambo ya dharura na hatari kama hili la jengo? Nauliza kwa sababu INASEMEKANA hilo jengo lilijengwa chini ya viwango na kwa kukiuka vibali kama lile lililobomoka! Sasa kweli tuhatarishe maisha ya watu kwa sababu ya kusubiri kesi iliyofunguliwa mahakakamani, tena mfunguaji mwenyewe ni mtu huyo huyo ambaye ameshaua watu kwa uzembe anaotetea?

Angalia mkanganyiko Mwekezaji mwenyewe amewekeza katika eneo ambalo liko chini ya serikali, na serikali ina ubia. Serikali yenyewe ndiyo hii isiyoweza kumwajibisha mtumishi wake mwenyewe hata kama ametenda kinyume na badala yake huendelea kutunzwa na kulindwa maadamu anatetea maslahi ya wakubwa. Unategemea nini hapo?. Serikali hii inaowapenda matajiri waifadhili unadhani ina meno leo ya kumchomoa huyo kinagaubaga?
 
mimi siyo mwanasheria. Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my blackberry 9860 using jamiiforums
asingeweza....simple and clear! Sheria ipo ili pia iweze kuwalinda wahalifu!!
 
Watu wanafiki kama nyie ndiyo mnayekwamisha maendeleo ya nchi hii. Watu kama nyie ndiye mnayewapa vichwa viongozi wabovu kama akina mama Anna Tibaijuka kwa kuwapigia makofi hata pale wanapoongea pumba. Ina maana wewe hujaona kabisa hoja ya WCM?
Ni ajabu kwa kweli kuona eti anapongezwa kwa kuja kuyajibu maswali hapa....kaulizwa makumi kwa makumi ya maswali lakini kayajibu maswali mawili....leo anaonekana ni very exceptional!!! Nilikuwa na swali langu nikaamua niliweke pending nione response ya maswali yaliyopita....is wastage of time kuuliza swali ambalo unafahamu kabisa kwamba huwezi kujibiwa!

Sana sana hapa nimemuweka kwenye watch-list! Sipendi kabisa watu wanaokuja hapa wana-post kisha haooooo, hawajibu hoja ya mtu! Mara nyingi huwa naingia kwenye posts zao, nikikuta mtu ana idadi sawa au inayokaribiana kati ya "Started Posts" na Total Posts, basi nafahamu hawa ndo wale wanaoandika na kuondoka huku wakiwaacha members hapa wanaparuana!
 
Mukaile kilinjwi hukujibu vizuri swali la Kigamboni. Tunaomba kujuzwa picha inakamilika lini, ili tujue hatima yetu?

Mkuu nakuunga mkono! Nakuonyesha kuwa amejikanyaga amekimbilia kusema tulinde amani bila kusema kweli kuwa haki kwa raia ndio inaleta amani ya kweli!
 
Getstart,

Uzuri sheria sio biblia wala msaafu, icho kipengele cha zuio kinaweza kufanyiwa Amendment then hatua zichukuliwe dhidi ya hilo jengo. Mkuu, mimi ni miongoni mwa watu tunao shuhudia ni namna gani wananchi wanapata shaka sana wakiwa kwenye hilo eneo.

Ina sikitisha kuona mtu mmoja tu ndiye analeta kadhia hiyo kwa wananchi. Kuna utawala wa sheria unaozidi nguvu ya umma?

Bahati mbaya unaiangalia kwa upande mmoja tu. Ndiyo maana ingekuwa vizuri hoja zipelekwe mahakamani na pande zote zijieleze, ionekane tatizo liko wapi na hukumu itolewe kwa misingi hiyo ya haki. Ushahuri wako ndiyo ulikuwa unatia shaka 'bomoa halafu hayo mambo ya zuio yafuatie'. Hii si sahihi na wala misingi ya utawala bora. Ungeshahuri Serkali iende huko Mahakamani kupata amendment unayoishahuri nisingekuwa na taabu. Misingi hiyo inalinda haki za mtu mmoja mmoja kama ilivyo haki za taasisi na jumuiya. Mambo ya Msaafu na Biblia hayaingii hapo.
 
Hongera sana mhe prof tibaijuka hakika umeonyesha kuwa wewe ni msomi ulie elimika hukusoma ili upate vyeti NO.umetoa majibu yanayo toa mwanga juu ya utendaji kazi ya wizara yako.
 
Mama Tibaijuka, kidumu chama cha mapinduzi. Nikupe ongera kwa ujasili wako wa kuja kutolea majibu humu jukwaani, ukizingatia kwa vuguvugu la ushindani lilivyo kwa sasa, nikupe hongera.

Lakini kuhusu jengo pale mtaa wa Indra Gadhi, Posta. Sidhani kama pingamizi lililo tolewa lina tija, ukizingatia hali ya usalama kwa wakazi wa eneo husika bado si shwari, watu hawana amani na wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru.

Mimi nadhani jengo livunjwe haraka iwezekanavyo, harafu mahakama kuu kama chombo cha kusimamia na kutoa haki, tuone itahamua nini. Haya ni maisha ya watanzania tunayangelea hapa, hatuwezi kuendelea kuyahatarisha kwa pingamizi la mtu mmoja au kikundi cha watu kwa kulinda maslahi yao.
Hivi unafahamu kwamba nchi hii ina mihimili mitatu?
Profesa kama Anna tibajuka hawezi kuchukuwa mawazo mgando ya kwenye mataputapu kama haya yako.
 
A true leader, listen people first... Give them time to post quite a lot of issues. Then, come to respond on Issues... Kudos ... Nakuhakikishia hauhitajiki ugonge keyboard kila siku hapa JF... Njoo mara chache unavyopata muda lakini shuka Nondo.

I agree we must uphold good governance... At any cost dictatetorship should be left with the opposition side especially with ....
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.


  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.
mama umeingia kwenye kundi la maharamia wa taifa ccm na sasa umebadilika.Nilikuwa nakuheshimu kwa msimamo wako lakini ccm wamekulegeza,wamekugalagaza na sasa wanakutumia,mbunge wetu hutaki maelezo yake wakati ndiye muwakilishi wetu,kwa nini unawarubuni madiwani kwa takrima zako? Kama unaenda kanisani au msikitini muogope mungu wako naomba ujibu moja tu kwa sasa hivi bei ya soko kwa heka moja ni kiasi gani? usimungunye maneno wala usilete longolongo nahitaji jibu sahii.Mwana Kigamboni Daima.
 
Bahati mbaya unaiangalia kwa upande mmoja tu. Ndiyo maana ingekuwa vizuri hoja zipelekwe mahakamani na pande zote zijieleze, ionekane tatizo liko wapi na hukumu itolewe kwa misingi hiyo ya haki. Ushahuri wako ndiyo ulikuwa unatia shaka 'bomoa halafu hayo mambo ya zuio yafuatie'. Hii si sahihi na wala misingi ya utawala bora. Ungeshahuri Serkali iende huko Mahakamani kupata amendment unayoishahuri nisingekuwa na taabu. Misingi hiyo inalinda haki za mtu mmoja mmoja kama ilivyo haki za taasisi na jumuiya. Mambo ya Msaafu na Biblia hayaingii hapo.


Mbona ninasikia MAGUFULI yeye kuamua kuvunja jengo KUBWA KARIBU NA VICTORIA JE YEYE hayathamini Mahakama?
NI mbaya! tunasikia katika maogorofa hiyo watu wamepewa vyumba vyao na HATA jengo lililobomoka kuna watu wailkuwa na vyao humo hizi NI ZA kutoka miomgoninmwa waliowekwa ndani KUToka kwa moja we waliowekwa ndani,
Ndi
o Maana. HATA matikoe ya Kamati hiyo yamewekwa kapuni uraisi NI NDOTO!
 
Mama kalainishwa na mafisadi hana lolote, ni mpuuzi kama majibu yake, kawa mwanasiasa na wanasiasa wote wa hizi nchi masikini ni wapuuzi hata wakiwa ma Dr/Prof
Amani vs Vita ndio kamba waliyobaki nao magamba!
 
Back
Top Bottom