Majibu rasmi ya Mwanakijiji kwa Waziri Mkuu

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 980
DODOMA
Alhamisi Julai 12, 2007
 
Sasa kama 80% ya Watanzania wameridhika na jitihada za kuwaletea "maisha bora" wakati umefika kwa Jasusi kukaa kimya.
 
Kaazi Kwelikweli!
Response Ofisi ya EL ni rhetorics deviating from reality at the ground! The changes we see are meant to so few people- the gap between the rich and poor is also widening at alarming rate! Wananchi wengi bado wanaishi nyumba za 'mbavu za mbwa' hawana uhakikia na mlo! Yet- is that "Take Off" ya Rostow? Au "take off" ya kisiasa?
Mabadiliko yapo kidogo- ila EL asiite this is a "take off stage". Conditions for take off are not ripe yet hapa SSA- hata nchi zenye uchumi mkubwa kama South Africa ‘take off' bado- ‘kupaa' ni kupi huko wana JF?
 
Duh...
"I feel the article bashing Mwanakijiji badala ya kujibu hoja eti...
....lakini anafahamika kuwa ni Mtanzania anayeishi Marekani. Ya pili, yenye kichwa cha habari: "Lowassa: Huu ni mzaha mbaya kwa Watanzania" imeandikwa na anayejiita Chris Alan, ambaye haikuelezwa kuwa ni Mwandishi wa gazeti hilo au la, au mtaalamu wa jambo Fulani, msomi au ni mtu gani. Hakuweka anuani yake wala namba ya simu....
...
Uelewa mdogo wa M.M. Mwanakijiji sawa na wa mwenzake Chris Alen ....Hawajaka tamaa wala kuikimbia nchi yao na kwenda kuishi ughaibuni kama alivyofanya M.M. Mwanakijiji!....

Wandugu mlioko ofisi ya PM..Hoja inajibiwa kwa hoja sio...ku mdegrade mtu...anwani ya nini? Kwa kifupi mmejibu "kihuni"! Hakuna lolote jipya we expected more than that from you!
 
Sasa kama 80% ya Watanzania wameridhika na jitihada za kuwaletea "maisha bora" wakati umefika kwa Jasusi kukaa kimya.

Inategemea na nani anasema hiyo asilimia 80. Yaani hawa jamaa Wameng'ang'ania REDET tu hakuna hata utafiti mwingine. REDET watasemaje zaidi ya hiyo anayodai waziri mkuu?
Kuuamini utafiti wa REDET inatakiwa uwe na akili kama ya mwenda wazimu. Watafiti wasaidizi huchukua posho zao (nusu wakati wanakwenda) kisha wakishafika huko wanahoji watu wawili au watatu na siku mbili zingine wanajifungia kwenye vyumba vya nyumba za kulala wageni wanajaza questionaires kiulaini. Siku ya nne jamaa wanarudi Dar, wanasubiri wiki mbili kisha wanarudisha questionares na baada ya siku tatu wanawasilisha report REDET wanachukua posho yao iliyobaki. Baada ya miezi mitatu Mukandala anatoka na report ya REDET asilimia 80!
 
Ujinga mtupu kwa hao watu wanaotoa majibu hayo. Vitu kama "anajiita" ni uhuni mkubwa. Nani anajali mwandishi anaitwaje? Sasa wamejipachika uzazi na kulazimisha majina ya watu?
Bila shaka ni hii iliyotoka katika Gazeti la TAnzania daima jana nayo watajibu!!

Lowassa, ndege haijapaa wala haijulikani lini itapaa

Padri Kitambo Robert

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/15/makala2.php
 
Kaka mjj, wenzio walinisihi nisichangie mada fulani nikawapuuzia kwani sikudhani kuna umuhimu wowote wa kuwasikiliza. Hata hivyo kitendo cha ofisi mbili za serikali kukujibu ndani ya wiki moja tena kwa maneno makali kinaanza kunipa wasiwasi. Nakuomba sana (na nitakuomba baadaye in private) achana na Tanzania, rudi andika hadithi zako na mambo mengine. Nadhani hawakupangii mema.

asante.
 
What????????????????????
Usitishike Mzee MKJJ...hiyo ni haki yako ya msingi!!!
Wana JF vipi...mbona nahisi "upepo wa kukata tamaa"!!!!
JF "ALUTA KONTINUA"..Tusilale!
 

Are you serious?
 
ALUTA KONTINUA!
Vema kuwa habari imewaingia na wamejibu! Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa- tena mapema. HOJA HUJIBIWA KWA HOJA!
Naomba kuunga Mkono!
 
very serious! kwani analipwa? wote tunamtia hamasa hapa mzee wa watu wakati yakimkuta tutabakia kusikitika tu. Kaka, achana nao hao, nakuomba sana kwa niaba ya kina mama wote. Waache wale nchi yao, usijifanye una uchungu kuliko walioko Tanzania wenyewe.

asante.
 
Bi Senti 50...Mimi ni mama .Count me out kwenye huo uwasilishaji!
....SOTE TUTAKUFA TU KAMA NDIO TUNAKOKUOGOPA ZAIDI. SO LET US DIE FOR A GOOD CAUSE!

TUNASONGA MBELE....
 

..acha uwoga wewe la sivyo utakufa maskini na manung'uniko maisha yako yote na kizazi kijacho ....mawazo yako ni ya hatari sana,unajua zamani nchi nyingi sana hata za WEST walikuwa na tabia ya ukiwapinga au kama hukubaliani nao ni assasination tuu lakini wakagundua ukiua na wewe utaishia kuuliwa tuu kwa hiyo nchi nyingi especially west wameacha kwa hiyo CCM wakicheza hiyo game nao wataishia hivyo tuu maana nature ya binadamu ni hiyo hiyo...si unajua bunduki kila mtu ana yake siku hizi
 
Tena ingekuwa mimi Mwanakijiji ningetumia jina langu la serikali...
Kwa nini mtu ujifiche? Tena sio kwamba watu hawakujui....
 
Watanzania hicho ndicho kinachotumaliza, UWOGA umetuzidi.

Mtikila yuko pale pale nyumbani mbona hawajammaliza? Mrema karusha mabomu yake, mbona hawajammaliza? Ukiwa unasema hovyo na wewe unaiba kama wao hapo watakumaliza, lakini kama huna cha kuficha kwanini uwaogope?

Mwanakijiji wewe endelea tu na maandishi yako. Muhimu sasa unajua wanakutafuta kwahiyo ni kuwa makini na kuchukua tahadhari lakini sio kuogopa. Kama kufa kila mtu atakufa.

Pole Mwanakijiji, wengine tuko nyuma yako na tutasukuma gari lako mpaka livuke kimlima.
 
Nyie mchombezeni mwenzenu tu, akiacha mjane nyuma mtasaidia kulea watoto? akiharibiwa unga wake huko aliko mtamsaidia kulipa bili? Mwanakijiji ulichofanya hadi sasa inatosha, wapatie walioko nyumbani baton ili waendeleze mbio. Believe me, its not worth it.

asante.
 


Naamini haya unayoyaandika hayatoki moyoni mwako, napata shaka kwamba huenda Bi.Senti 50, kweli unawasilisha maoni toka moyoni mwako... Nakumbuka kuna mtu mmoja rafiki yangu alaiwahi kuniambia wakati wa mapambano fulani kwamba "ukitaka kupambana na audi yako, tafuta watu makini uwachanganye miongoni mwao na kazi kubwa ni kuwakatisha tamaa upande wa adui yako ili uweze kusonga mbele kwa KASI, ARI na NGUVU mpya huku adui yako akinyong'onyea na kujiona mnyonge"

Kwa hili bibie (kama kweli ni bibi) umekwama kwani si Mwanakijiji pekee anayeendesha mapambano haya bali ni mfumo na hali halisi inayosukuma mapambano. Hata mwanakijiji leo akiondoka, hata mwingine yeyote akiondoka, ujue wapo wengi ambao hakuna jambo litakalowabadili mawazo... yaani kama hali itaendelea kuwa hivi watazaliwa wengine wenye ari, kasi na nguvu ya kupinga udhalimu na watakaokuja wakikuta hali mbaya zaidi wataweza kufanya mambo ya hatari zaidi. Mungu atupe nguvu ya kuzuia HALI ISIWE MBAYA ZAIDI TUWEZE KUDHIBITI NA KUIKOMBOA NCHI YETU.. HALI IKIZIDI KUWA MBAYA WATU HAWATATAWALIKA, HALI HAITADHIBITIKA...

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…