Majibu rasmi ya Mwanakijiji kwa Waziri Mkuu

Wandugu,

Kwanza kabisa ningeomba posts za Bi centi hamsini zifutwe kwenye hii mada.

Nionavyo, Ofisi ya waziri Mkuu imekurupuka, kujibu ni sawa ila stahili ya maandishi ndio imenishangaza, Jamaa aliyeandika kaandika utafikiri yupo kijiweni anawaandikia machizi. Jibu hoja kwa hoja. Hakukuwa na umuhimu wa kutaja Identities, kusema tu kuwa gazeti la Mtanzania daima ingekuwa enough reference.

Kisha wangechukua hoja moja moja na kuanza kuzichambua kisha kujibu. Eti kwa kuwa Mwanakijiji ametumia msemo wa Nyerere na wao wanatumia, hilo ni kukosa ubunifu na ufupi wa mawazo. Ninashauri serikalini muajiri watu kwa sifa na sio kujuana.

Kama mwandishi aliyeandika hiyo makala yupo humu, naomba anitumie PM nimjibu mwanakijiji, ili akatoe magazetini.

Hoja za mwanakijiji zinajibika na sio kweli kuwa zote ni za kweli.

Kuhusu kutishiwa, mimi kama mwana CCM ninasema hamna kitisho chochote hapo, ni jamaa mmoja tu kakosea na kumjibia Prime minister wetu vibaya. EL ni muelewa wala asingejibu kijazba jazba namna hiyo, Huyo aliyejibu yaelekea ni dizaini ya Mrema na Mbowe au wale Ngangari!

FD
 
Nasikitika kuona wengi wameogopeshwa. Nadhani maofisa husika walijibu hoja kwa nia nzuri. Wangeweza kudharau, na kikaisha. Mimi nawashukuru kwa kujibu hoja, na ni wajibu wetu kukubaliana nao au kujibu. Naomba nijibu kipengele kimoja kama ifuatavyo:

It has been said that statistics are like a bikini: what they reveal is suggestive, but what they conceal is crucial.

Wandugu (tusisahau hawa ni ndugu zetu) wamesema zimejengwa sekondari 1,090. Swali ni hili: zimewekwa waalimu wangapi? Maana sekondari mpya zaidi ya elfu zitahitaji waalimu wapya zaidi ya elfu 10!

Na hiyo idadi kubwa ya watoto walioandikishwa shule za msingi, wanasoma kwenye shule za aina gani? Kwa wastani, wako wangapi kila darasa? Kuna vyoo? Kuna vitabu? Kuna waalimu?

Lazima tuhoji hizo takwimu. Takwimu za REDET nilizidharau tangu wakati wa uchaguzi uliopita. Nazidi kuzidharau sasa.

Perhaps we have taken off, but, in which direction?

Augustine Moshi
 
Ukisoma majibu ya ofisi ya PM kitu kinachokuja wazi wazi ni kwamba serikali yetu haina performance measures. Mafanikio kwao
yanatokana strategic decisions and not the outcomes of these strategic decisions.

Kwa mfano ni jambo zuri kwamba serikali iliamua kutenge bilioni 21 kwa ajili ya kuwasaidia Wajasilimali wadogo wadogo, lakini je
mafanikio ya huo mpango yakoje? Je hizo pesa zimewafikia walengwa? Wangetengeneza mapema juu ya mafanikio yatakuwa judged vipi, wangejua wazi kwamba mpango mzima ni failure kubwa mno na serikali itaishia kupoteza pesa nyingi kwani hazitarudi.

Kuhusu kuongeza shule ili vijana wetu wengi wasome, nalo ni jambo zuri tena zuri sana. Sawa zimejengwa shule zote hizo anazozisema tena kwa nguvu ya wananchi lakini je what next? Hizo shule hazina walimu, hazina vitabu, na kwa ujumla sio mahali pa
vijana wetu kupata maarifa ya kuwasaidia huko mbeleni na badala yake ni kijiwe cha kupotea miaka minne, ni namba ya watu wa serikali kuitumia kuombea misaada na kuwashambulia wanaowakosoa. Lengo linapogeuka kutoka haki ya msingi ya kijana wetu kupata elimu bora na kugeuka kuwa namba hapo ndipo zoezi zima linapokosa maana.

Wanaongelea kupambana na maradhi na hatua wanazochukua, sawa ni jambo jema lakini PM anajua kwamba watoto wanakufa kwenye hizo hospitali kwa kukosa dawa ambayo serikali tayari imeshalipia na inatakiwa itolewe bure? Haitoshi kuingiza pesa kwenye budget kama hazifiki kwa wale waliokusudiwa.

PM na genge lake wako OUT of TOUCH na reality ya maisha ya wananchi wa kawaida, labda ndio maana wanafikiri ndege yao inapaa huku mamilioni ya wananchi wetu wako kwenye train linalodidimia kwenye matope, je wananchi hawa watafika hata huko airport angalau kwenda kuwashangilia hao wanaopaa?

Kama walioandika hiyo makala ndio washauri tulio nao, no wonder miaka karibu 50 bado hatuendi mbele. Inakuwaje Tanzania yenye vijana wengi wenye elimu na uchungu wa nchi yao, inakuwa na civil servants vilaza kama hao? Hao ndio wanatakiwa kumshauri na kumwongoza PM na sio kuandika makala mbovu kama hiyo.

Ukisoma makala yenyewe ni aibu tupu. Wacha niache maana jazba linaanza kupanda.
 
Misingi hii ya uchumi (Kwa Kiingereza: Macroeconomic Fundamentals) ndiyo ambayo mchumi mmoja maarufu Walter Rostow aliita kuwa ni mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza “kupaa” (Kwa Kiingereza: “Pre-conditions for take-off”) kuelekea katika kujenga uchumi imara. Hivyo Waziri Mkuu alipotumia neno “kupaa” alikuwa anamaanisha dhana hiyo ya hatua ya pili ambayo ni “take-off” baada ya kuwekwa misingi ya kukuza uchumi katika Awamu ya Tatu.

Nadhani suala la msingi hapa ni kwamba kwenye makala yake "Mwanakijiji" alitafsiri visivyo maana ya "ndege kupaa" kutokana na kutofahamu chanzo na maana ya dhana ya "kupaa".

Lakini ukitafakari kidogo utagundua kuwa si kosa la "Mwanakijiji" kushindwa kuelewa tafsiri ya msemo "kupaa" kwani ni kosa kwa Waziri Mkuu kukopa dhana ya kisomi ambayo ina maana pekee kabisa kwenye mazingira fulani ya kipekee bila kutaja chanzo chake (i.e., failing to acknowledge source of idea) . Kwa mantiki hii ni wazi kwamba Waziri Mkuu ametenda kosa la "plagiarism".

Kwa kweli ni ajabu na kichekesho kikubwa kwa Waziri Mkuu kutegemea Mtanzania wa kawaida afahamu nadharia za Walter Rostow na hiyo dhana ya “Pre-conditions for take-off”. Huu ni ushahidi tosha wa jinsi hawa watawala wa CCM walivyo out of touch na mtazamo wa wananchi wa kawaida.
 
Ngugu wananchi!
Akutukanaye hakuchagulii Tusi.
Huyu Lowassa ambaye ni mbumbu wa somo la Uchumi leo anajua theories za Walter Rostow?

Na ninyi wapambe wake mliodandia hiyo ndege kama nzi tayari mshatuona wote ni wajinga kwani bosi wenu katurushia elimu tusioijua.

Rostow's Five Stage Model of Development Hizi hapa.

http://www.basu-mallick.de/projekte/Oliver_Basu_Mallick_2005_Rostow_and_Globalization.pdf

Hebu Fungua hiyo lead soma Page 5-8.

PM ofisi ina Vilaza watupu au ni watu walioshiba ufisadi kwa hiyo wanatuonyesha jinsi walivyo hodari wa kutoa majibu ya Ki imla imla.

Endapo hapo ndo mwisho wa uelewa wenu na hayo ndo majibu yenu Rasmi sishangai kwa nini mko kwenye njozi kwamba ndege yenu inapaa.

Pre condition for take off hazikuwa mate ni vipi ndege imeweza kupaa??

Lowassa wachumi wanao kushauri wamekushauri vibaya siku nyingine jaribu ku google mwenyewe au upate Hard copy kama ilvyo kawaida ya wanao uogopa mtandao kama wewe.
 
Huu kweli ni utani usio na kipimo. Hivi kweli PM anaweza kusema kuwa uchumi wetu umejengwa kiasi cha kuanza kupaa. Huyu bwana anapaa yeye na wanamtandao wenzake. Majority of our citizens since they are still asleep especially the so called 80% that voted JK in which might be dreaming.

Hivi uchumi ambao hata haujawahi kukua zaidi ya 6% na nchi yenye kutegemea more than 40% of its budget from donors wanasubutu kusema haya kwa wananchi na kutetea hadharani bila points zenye substance kweli inanitia kichefuchefu.

Wenyewe wamesomesha watoto wao nje wakina MKJJ wametoka wanawaona wanakimbia nchi. Anyway watu wasimtetee EL, barua ile lazima aliiona yeye mwenyewe au PS wake kabla ya kutoka hivyo point zote alizipa baraka kabla ya kutoka. Hiyo inaonyesha uelewa mdogo miongoni mwa watendaji wetu serikalini.
 
Hizo zinaitwa Sound bites na ndio kazi za Spin doctors wa PM.

Ndege kupaa, wanajua matumaini ya kila mtanzania ni ndege kupaa, kwahiyo wakitumia hilo neno kila mtu ataelewa.

They are more interested in scoring points than expressing the realities.
 
hivi mara ngapi wanataja hilo jina la "mwanakijiji".. naanza kuogopa.

Ha ha! Usiogope Mwanakijiji,Huu moto wameuwasha wenyewe kwa matendo yao yasiyolingana na ahadi zao zilizowaweka madarakani. Jee unaogopa "kunyamazishwa?" watanyamazisha wangapi na moto umeshika kasi pande zote? Hapa ni mpaka kieleweke.
 
Somo kwa PM na genge lake kutoka kwa msomi Yunnus:

"Ukitaka kuwasaidia maskini hesabu ni wangapi hujawafikia"
 
Mtu mmoja alisema hivi, nani mjinga kati ya hawa "Mtu mzima anayeogopa mwanga au mtoto anaye ogopa giza". Kuwa masikini ni kweli tu masikini, kwamba tutatoka katika umasikini hilo halina mjadala. Wengi wetu ni watoto wenye milango sita ya fahamu, na ule mlango wa sita unatufanya kwenda mbele akiwapo yeyeto kama kizingiti tutapita tu wala hatuzuii kwa lolote. Moyo uko thabiti katika hilo, tunajua inawezekana wala hatuitaji kuambiwa na EL wala nani. Maisha yamekuwa na yatakuwa magumu kutokana na bajeti ya uchumi unaopaa hilo halina mjadala. Maamuzi yanapitishwa kwa Uccm na sio wananchi wanataka nini hilo halina mjadala. lakini mwisho wa siku mafanikio yetu ni dhahiri hakuna atakaye simama mbele yetu. Sisi sote ni ndugu hilo halina mjadala, tunakamdamizana halina mjadala, wapo wakandamiza na wakandamizaji hilo halina mjadala, wataendelea kuwepo sina hakika.
 
Hiyo ATC yenyewe inashindwa kupaa sasa nchi itapaeje? Kweli bongo usanii mtupu!!!!

FD,
Watendaji hawawezi kutoa bila yeye kutoa baraka zake. The way article ilivyoandikwa kama kuna matatizo nani atawajibika? Unafikiri ni nani aliyewambia kuwa alikuwa najaribu kudesa kutoka kwa Walter Rostow kama siyo yeye mwenyewe????
 
Guys, sasa tunaanza kuwa na woga wa kitoto. Katika majibu ya ofisi ya waziri mkuu hakuna vitisho vyovyote. Yale ni majibu tu ya kihoja. Kama kuna vitisho sio katika ile statement, labda mseme ametumiwa message pembeni nje ya ile statement. Mambo yote aliyoandika mwanakijiji yanajibika kihoja; vilevile majibu ya PM yanajibika kihoja.

Mbona tunaanza kujitisha wenyewe? Jamani uanaharakati sio kazi rahisi,tukiamua kuifanya tujue tumeamua kufanya kazi kubwa na ngumu! Sasa sisi tunajitisha tena tukiwa nje ya nchi, halafu tunawalaumu wananchi waliopo nchini kwamba ni waoga?
 
Bi Senti 50...Mimi ni mama .Count me out kwenye huo uwasilishaji!
....SOTE TUTAKUFA TU KAMA NDIO TUNAKOKUOGOPA ZAIDI. SO LET US DIE FOR A GOOD CAUSE!

TUNASONGA MBELE....

Nipo pamoja nawe Mama Lao. MKJJ Endeleza mapamabano, uskikatishwe tamaa. David Vs Goliath. Utashinda tu.
 
Jamani baada ya kufurahi kuwa sasa tumeanza kupata na majibu ya upande wa pili, tunafikiria jinsi ya kutishana wenyewe. kijiwe hiki kimekuwepo kwa muda mrefu sana na tumekuwa na hoja nyingi ambazo hazina majibu toka kwa wahusika.
Kwa mtazamo wangu sasa ndio wakati wa kupeleka hoja moja baada ya nyingine kwa sababu tutapata tu majibu kutoka kwa wahusika,ndio changamoto tunaloitaji ili tuweze kufikia muwafaka ktk hoja zetu.
muda wa kupiga porojo umekwisha,tuna mambo mengi tu ya kuhoji ktk ofisi ya waziri mkuu maadam wamejitokeza wapambe wake kujibu,basi sasa huu ndio wakati wake.
Kuhusu waandishi wa PM, hivi ni nani asiyejua kazi za bongo zilivyo wewe ni bwana shamba lakini umeajiriwa idara ya uhasibu,au wewe ni mhandisi lakini unafanya kazi ya uandishi wa habari yote hiyo ili mkono uende kwa kinywa.
Mmjj sasa tumefika mahala tulipokuwa tunapatafuta kwa muda mrefu,nikupongeze kwa hilo,sasa tutapata majibu ya baadhi ya maswali yetu hata kama yatakuwa ni ya kihiyo.
 
Natoa Salaa toka hapa Dodoma ambapo Zitto amekandamiza kisawasawa , majibu ya waziri Mkuu hayana mvuto kwa Mzee MKJJ.Napita tu
 
hivi mara ngapi wanataja hilo jina la "mwanakijiji".. naanza kuogopa.

Mzee MKJJ...fear can paralyse you....
YOU HAVE NOTHING TO FEAR HOJA ZAKO NI ZA MSINGI NA MAELFU YA WATU TUKO NYUMA YAKO.
Naona sasa the Devil is tempting you via BI 5O CENT....SHE HAS COME TO INSTILL THE FEAR IN YOU.
UAMUZI NI WAKO ....
 
Jamani, niliposema "naogopa" sikuwa na maana nimetishika. NIlikuwa na maana msisitizo wa majibu yao ulikuwa ni kumjibu mtu ajiitaye "mwanakijiji" ambaye wanadai ana "uelewa mdogo". Badala ya kuonesha upuuzi wa hoja zangu na kutetea Tanzania yao inayopaa, wamechukua mistari kadhaa to do ad hominemn attacts. Hata hivyo nimeshawajibu. Na nimewajibu kwa point nikipangua kila hoja waliyokuja nayo hadi "mfano wa Mpwapwa" mahali ambako nimewahi kuishi. Ndugu zangu, tunachoshuhudia ni mgongano wa kifikra, kati ya fikra za watu wanaotaka Tanzania ya zamani ambapo wakubwa wakikohofa tunatetemeka, wakinuna tunadondoka na wakicheka basi tunapata neema! Fikra za wale ambao kwao Tanzania ni ya "kwao" na sisi wengine ni wapangaji tu katika nchi yetu. Fikra hizo zinagongana na fikra za watu wanaoamini kuwa Tanzania yenye neema na yenye mafanikio siyo tu inawezekana bali pia tunaistahili. Ni fikra zinazosema viongozi wanatoka kwa watu, na ni watu ndio wenye mamlaka ya mwisho. Haya ni mapambano ya kifikra na natumaini si ugomvi!!

Ndugu zangu wale waliotamba kuwa kelele za mlango haziwakoseshi usingizi inaonekana ndani ya wiki moja wameanza kushtuka shtuka... kwani zile kelele za mlango zimeanza kutiwa nguvu na kelele za madirisha, mapazia, kenchi na paa! Vinginevyo, kwanini bodi ya mikopo itumia kurasa nne kujibu hoja za "mzushi"? kwanini Ofisi ya Waziri Mkuu watumie muda wao kujibu hoja za mtu mwenye "uelewa mdogo"?

Kuna sababu moja tu, kuna madhara ambayo yameanza kufanyika. Nilipoandika makala ya kwanza ya "Anguko la CCM, unabii utatimia" mbona walinipuuzia, ingawa walishtuka? Ninapata wapi mawazo haya yote, ni hapa Jambo forums, hoja nyingi ninazotoa zinatokana na mjadala wetu humu na kutokubaliana kwetu humu na ndio maana ninawapenda wale wanipingao na kunisahihisha kwa sababu they sharpen my minds and show my flaws in my arguments.

Ni kwa sababu hiyo ndugu zangu, tusirudi nyuma! Nchi ni yetu sote na hakuna mtu mwenye haki zaidi na Tanzania kuliko mwingine, hata kama mtu huyo ni kiongozi shujaa, hodari, mahiri aliyetamba Bungeni.

Kwenye gazeti hilo la "Kulikoni" kuna makala yangu nyingine ambayo inasema "TUWAACHIE NCHI?". Nitaibandika kwenye hoja kuu.
 
Mh. Lowassa ni msomi wa development Studies kwa hiyo alipokwa anazungumza bungeni alijua anazungumza kitu gani... lakini tatizo moja ni kwamba.. hadhira yake (wabunge wengi) hawaelewi lolote kuhusu Political Economy wana Development Studies
(Najaribu kupiga picha jinsi John Komba na washkaji zake walipokuwa wanamshangilia Wziri Mkuu)!

W.W Rostow alitumia lugha ya picha kufafanua Theory yake ya Modernization (Rostow's Stages of Growth) against ile ya Karl Marx!

Mh. Lowassa akatumia tena lugha ya picha kujenga hoja yake bungeni!

M.M Mwanakijiji akatumia lugha ile ile ya picha kujibu hoja ya Mh. Waziri Mkuu!

Nakumbuka niliwahi kukutana na mchoro uliokuwa unaonyesha Rostow's Stages of Growth kwa kutumia picha ya ndege ya abiria!

Kinachonishangaza ni hiki:

Mh Waziri Mkuu anasema Serikali ya awamu ya pili ilikuwa kwenye Rostow's Second Stage of Growth ambayo ni Preconditions for take-off. Hizi preconditions kwa kauli nyepesi zaidi ni uenezaji wa misingi ya kiuchumi kwa jamii nzima... id est kuunda tabaka la wawekezaji/wajasiriamali na kuhakikisha ushamiri wa benki zenye nguvu zitazowezesha tabaka hili kustawi! Na hii process si ya siku moja, inaweza kuchukua hata miaka 50 kama sio mia!
Kama serikali ya awamu ya tatu ilifanya yote haya.. basi ni kwenye makaratasi.. ila kivitendo waliuza njia kuu za uchumi kwa wageni.. tena kwa bei ya kutupa na hivyo kujitupa mbali kabisa na Rostow's Second Stage of Growth .. na si kama Mh. Waziri Mkuu alivyowaburuza wabunge na uma wa Watanzania!

Serikali yetu ya awamu ya nne haijafikia bado hatua ya tatu ambayo ni Take Off.
Labda nimuulize Mh. Waziri Mkuu kwa kutumia Lugha ya Picha:

Utawezaje ku-Take Off gizani wakati matairi yamechomolewa, Runways zimeota nyasi, mvua inanyesha na giza linaingia?
Hiyo Take-Off ina-sound kama ile ya Mfalme Njozi!
 
Ofisi ya PM kwa kweli inatatizo la kimantiki kabisa .
Tafuteni vijana na wazee wenye uwezo wa kujibu hoja za ofisis yake badala ya kujidhalilisha na majibu ya namna hii kwa kweli .
Duuh kweli REDET mnafanya kazi mliyotumwa kisaswasawa. leo napitaq tu kwani nilikuwa nipo safarini tangu awali.

Nitarudi hapa kuja kujibu hoja baadhi .
 
Back
Top Bottom