Majibu rasmi ya Mwanakijiji kwa Waziri Mkuu

NAKUHAKIKISHIA HATA HAO WANAOWATUMIKIA HAO MAFISADI, Nikiwa na maana watumishi wa kina BALALI na KINA MSOLA na wengineo hawana imani na mabosi zao na wanapigana bega kwa bega na kina Mwanakijiji, ujue fika ndio maana ahata hizo taarifa za serikali utaona zinaandikwa kisanii ili kuzidi kuwakandamiza wenyewe..

Mwanakijiji tuko nyuma yako wengi... Hata hivyo vitisho wahusika kama Balali na wenzake hawana ubavu wa kujitokeza hadharani na kufanya madhara, watakachofanya ni kutuma watu ambao hawapo kwani hakuna MTANZANIA ambaye hajui kinachoendelea, hata hao MAPOLISI, USALAMA na kadhalika, hawaridhiki na hali iwayo
 
Hivi REDET anayosema ndiyo ile taasisi ya wanamtandao inyoongozwa na Professor Lwekaza Mukandala?

Huyu Mukandala mbona sasa naye amejiingiza kutumiwa kisiasa hata kwa kuleta data zisizokuwa za kweli, jambo ambal ni baya sana kitaaluma huku yeye akiwa ni mkuu wa chuo kikubwa sana kitaaluma hapa nchini. Ameona zile picha za Maggid Mjengwa alizotoa huko vijijini?
singidakinampanda.jpg

singidafamilia.jpg

kshambakokoto.jpg

Je anasema kuwa hata hao watu wa vijijini wameridhika na maendeleo. Kama Viongozi wetu wanatafsiri maendeleo namna hiyo basi tuna njia ndefus sana ya kwenda
 
Ebwana eeh....wait a minute. Kwani Mwanakijiji katishiwa maisha..? Mbona watu mna mchecheto hivyo? Mimi binafsi sidhani kama wanamuhofia Mwanakijiji namna hiyo. Kwanza sitashangaa kama wanamjua kwa jina lake alilopewa na wazazi wake. Mwanakijiji haishi kisiwani peke yake bali anaishi na watu huko aliko na si vigumu hata kidogo kujua yeye ni nani na anafanya nini. So long as hayuko CCM na hana madaraka yoyote watamwacha kama alivyo. Mtikila (mfanya kweli) mpaka leo bado anapeta. Linganisheni aliyoyafanya Mtikila na Mwanakijiji. Mnataka kuniambia ya Mwanakijiji yanashinda ya Mtikila? I don't think so. Kwa hiyo hamna haja ya Mwanakijiji kubabaika na majibu ya ofisi ya waziri mkuu hadi kufikia kuhofia maisha.
 
Hakuna mtu atakaye ondolewa na hawa wakoloni weusi na wala hatutishiki na hao waganga wao wa kienyeji. Mwanakijiji is bigger than hizo tisha toto zao. Mapambano Bado Yanaendelea.
 
very serious! kwani analipwa? wote tunamtia hamasa hapa mzee wa watu wakati yakimkuta tutabakia kusikitika tu. Kaka, achana nao hao, nakuomba sana kwa niaba ya kina mama wote. Waache wale nchi yao, usijifanye una uchungu kuliko walioko Tanzania wenyewe.

asante.

Kuna mama mmoja bungeni alishika tama na kumwambia marehemu AC "mtoto wewe?"
 
Hakuna mtu yeyote Duniani awezaye kuongeza au kupunguza maisha yake hata sekunde moja kwa Woga.

Kila mtu hapa duniani ataishi maisha yake, muda ukifika anaondoka.
Hapa Duniani kuna kuishi tu hakuna kuishi zaidi ya muda wala kuishi chini ya muda.

Kwa hiyo ninyi CCM msilete vitisho vyenu hapa mtandaoni magazetini au mahali pengine popote. Komeni.

Kazi aliyotumwa mtu kuja kuifanya Duniani ikiisha ni lazima aonje mauti arudi katika asili yake.

Kwani imeandikwa kila nafsi hai itaonja mauti.

Mjue fika huu ndiyo mwanzo wa mwisho wenu.

Kuendelea Kutumia silaha yenu ya enzi zote (Vitisho)kwa mara nyingine tena haisaidii.

Kwa miaka 46 mlitugubika kwa Blanketi la Woga na mlifauru sana.

N ikweli silaha yenu ya kuwatia hofu Watanzania iliwahi kufanya kazi enzi zile lakini sasa hivi imekosa umaarufu.

Kundi linalo tishika na vitisho vyenu linapungua, muda si mrefu litatoweka kabisa na huo ndiyo utakuwa mwisho wa mwisho wenu.

Viroho vinawadunda na mimacho inawatoka hamuamini akili zenu

"Hata akina M.M. Mwanakijiji wanatuambia ukweli???"

Mkipatacho sasa hivi ni upepo wa baridi hata manyunyu hajaanza kudondoka.

Ikishuka masika, umoja wenu haramu utasambaratika.

Nchi ya Tanzania si mali ya CCM kila mmoja wetu ajue hilo. CCM hawajakopeshwa wala kuazimwa Tanzania,ila wamepewa dhamana tu(Mandate).
Tanzania ni ya Watanzania wenyewe na Watanzania hao ni sisi.

Mnakumbuka niliwaambia andikeni na kutoa vielelezo bila hofu?
Serikali ya watu waovu sikuzote inaogopa kusemwa na watu wa kawaida kuliko kitu chochote kile.

Janja yetu inafanya kazi wenyewe wamejileta kilingeni na majibu ya kubuni.

Watanzania tuendelezeni mapambano popote pale tulipo tusikubali CCM watugawe.

Eti kuna wa Tanzania wa Ughaibuni na wale wa Tanzania!

Kuwagawa Watanzania kwa mtindo wowote ule ni kufilisika Kisiasa ni mtindo uliotumika na Jasusi (Karl Peters).
 
bi thumni umenisikitisha, na umemuaibisha mama yangu, kwani ww ni alama wa unaewakilisha mama zetu ambao kwa kukabili mapambano na kuwa tayari kufa ndio kulikotufanya tuwepo.

mapambano juu ya haki dhidi ya dhulma lazima yaendelezwe, la zima tuseme "ukweli ni huu" (kuusuta uwongo) yaani ukweli ubainishwe na uwongo usiwe na nafasi.

nnaamini hakuna mtu anaeweza kumchafulia mwenziwe maisha, ikiwa hilo halijaandikwa na kuna msemo unasema "when God close one Door he open another".

msemo huo unatufunza kwanza mwenye mamlaka ya kufunga mlango wa rizk na mengineyo ni MUumba, na akiifunga hukufunguliwa mwengine.

watu wengi walijitolea, kila chao mpaka maisha yao kwa ajili ya kunusuru maisha ya wenzao, na ndio maana kila tukikaa huwa majasiri kwa kuamini kuna wengi tu walipenda kuishi kama sisi lkn kwa kuona kuwa maisha yao hayana thamani ikiwa dhulma haijaondoshwa na walipambana hadi kuishinda au kuondoka duniani wakiwa hai na uhai wa milele

Martin Luther king yu hai na hatokufa, Gandhi yu hai na hatokufa na wengine tele.

basi na mkjj endelea uwe hai milele, milele ushukuriwe na uwe mfano wa kuigwa hata ikiwa ushatangulia mbele ya haki.

pia mimi na ww senti hamsini na wengine tukubali aidha kuwa na wapigania haki au na na wapigana na haki
 
Bi senti 50.

Acha mambo yako hayo ya kukatisha tamaa na kuturudisha nyuma, ebu tueleza jambo gani mnalotaka kumfanya mkjj? kama ni kuhisi kwako tu funga domo lako
 
Ebwana eeh....wait a minute. Kwani Mwanakijiji katishiwa maisha..? Mbona watu mna mchecheto hivyo? Mimi binafsi sidhani kama wanamuhofia Mwanakijiji namna hiyo. Kwanza sitashangaa kama wanamjua kwa jina lake alilopewa na wazazi wake. Mwanakijiji haishi kisiwani peke yake bali anaishi na watu huko aliko na si vigumu hata kidogo kujua yeye ni nani na anafanya nini. So long as hayuko CCM na hana madaraka yoyote watamwacha kama alivyo. Mtikila (mfanya kweli) mpaka leo bado anapeta. Linganisheni aliyoyafanya Mtikila na Mwanakijiji. Mnataka kuniambia ya Mwanakijiji yanashinda ya Mtikila? I don't think so. Kwa hiyo hamna haja ya Mwanakijiji kubabaika na majibu ya ofisi ya waziri mkuu hadi kufikia kuhofia maisha.

Wakati Mwanakijiji mwenyewe anasema: "Hoja hujibiwa kwa hoja" au labda haikutakiwa kujibiwa nini!!
 
Wakati Mwanakijiji mwenyewe anasema: "Hoja hujibiwa kwa hoja" au labda haikutakiwa kujibiwa nini!!

Yep!! Its funny how Mwanakijiji is now suddenly draping himself in false victimhood if he was cavalier enough to challenge the Prime Minister in the media.

Kwa vyovyote vile, sioni mahali ambapo "Mwanakijiji" au "Chris Alan" wametolewa maandishi ya vitisho kwenye majibu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Ninachoona ni watu wanatumia "emotions" kumtetea visivyo wakati mwenyewe amekaa kimya huku aki-enjoy new found status as imaginary victim badala ya kutetea msimamo aliotoa kwenye makala yake gazetini.
 
Wananchi wenyewe, kama walivyofanya katika ujenzi wa shule kwa kuibua miradi hiyo na wao wenyewe pia kuchangia, licha ya msaada wa serikali, wako tayari kwa kazi hiyo! Hawajaka tamaa wala kuikimbia nchi yao na kwenda kuishi ughaibuni kama alivyofanya M.M. Mwanakijiji!

Ofisi ya Waziri Mkuu imeboa kweli kweli. Katika busara zao zote wameona kuwa hili nalo ni jibu la kuandika gazetini? Sijaamini kuwa hii ilikuwa ni sehemu ya jibu la waziri mkuu au limeongezewa na mhuni mmoja wa mitaani asiyehusika kabisa na ofisi ya waziri mkuu.

Nakumbuka kuwa mwaka 1995 katika kinyang'anyiro cha urais, Mwalimu alimwabia Lowassa point blank kuwa alikuwa hafai kuongza nchi. Mimi nilikuwa mmjawapo wa shabiki wakuu wa Lowassa niliyekatishwa tamaa sana na msimamo huo wa mwalimu, kwani Lowassa alikuwa ndiye role model yangu ya uongozi kutokana na popularity yake aliyojipatia pale wizara ua ardhi. I think Mwalimu was right.

Kama kweli hiyo ilikuwa ni sehemu ya jibu la waziri mkuu, ukichanganya na jibu lote kwa jumla (nitaliongelea muda mwingine) utaona kuwa huyu mtu ni mfupi sana wa mawazo. Analodai hapa ni kuwa mtanzania yeyote ama anayesoma au kufanya kazi nchi za nje hana haki ya utanzania. Kama huo ndiyo mwongozo wenyewe, basi wabongo wote mlioko ughaibuni nadhani mmeipata. Acheni "kujipendekeza" kwenye balozi zenu na wala "msijipendekeza" kwa viongozi wa bongo wanapokuja nchini mnakofanyia kazi kwa vile "mmeshapoteza haki zenu za utanzania." Msizungumzie lolote kuhusu Tanzania na viongozi wake kwa vile "mmeshapoteza haki zenu za utanzania."

Ni matumaini yangu kuwa Waziri mkuu ataikana statement hiyo.
 
tutajuaje, inawezekana wamegundua kwamba Mwanakijiji amejilipua. lol!
 
Viongozi wetu wamezoea kumiliki vyombo ya habari basi wanaweza kuandika kitu wanacho kitaka kwa wao mimi sioni cha ajabu majibu yaliyo toka ofisi ya waziri mkuu akuna cha kusha ngaza wengi wetu tuna jua hilo ni kuvumilia kura zenu zi ishe muda wake,2010.
 
Hiki kimya cha "Mwanakijiji" ndicho kile cha "Ukiona kobe kainama..." au?

Vinginevyo bandugu tafadhali wacheni kumtetea "Mwanakijiji" kwa hoja zisizohusiana na yaliyomo kwenye majibu yaliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Acheni ajibu mwenyewe kipengele kwa kipengele, tena kwa takwimu na ushahidi mwingineo kama ikiwezekana. Nani alisema kazi ya Uandishi wa habari ni masihara? Tunataka "objectivity and truth" na siyo "fiction and anecdotes".
 
Takwimu? Tanzania? Simple: Look, Sh billion moja za wajasiliamali kila mkoa, mkoa wetu wa Tabora una idadi ya wakazi 1,717,908 kwa hiyo kama wote wanataka kufaidika na hizo hela ambazo Lowassa anatuambia zinaondoa umaskini, kila mmoja atapata Sh 582.11, ambayo ni kama nauli ya daladala kwenda na kurudi kutoka mjini, je hiyo inaondoa umaskini? Na je takwimu hiyo inatosha kukuonesha kuwa Lowasa anapiga domokaya tu?
 
Hapo umechukulia kuwa wakazi wote wa Tabora ni wajasirimali siyo? Lakini kwa vyovyote nakubali kuwa bilioni moja kwa kila mkoa ni kiasi kidogo sana kwani hata kama zingegawanywa kwa nusu ya hao wakazi milioni 1.7 zingekuwa ni sawa na pesa za njugu tu.
 
Lakini si philosophy ni maendeleo kwa watanzaia wote? Kwanini wanyamwezi wengine waachwe?

Unajua hawa jamaa hawafai kabisa kuongoza nchi masikini kama Tanzania kwani wanataka watanzania wote wawe wamachinga au mama nitilie vile.

We said before, the main enemy that must be got rid of before we talk of any development is ignorance in all dimensions. But, they are putting forward Tsh 1bn per region as their bail against poverty, and the PM is boasting of that decision. Come on!!
 
Back
Top Bottom