Kidogo chetu
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 1,432
- 993
Sie kwetu KAWE maji ni 24/7 pamoja na umeme, tukikosa jua ni tatizo kubwa na zito la kitaifa .Ni zaidi ya wiki mbili na kama sijakosea itakua ya tatu kumetokea jambo ambalo ni la kustaajabisha kidogo katika jiji hili.
Hapa ninapokaa (Ubungo Msewe) hapo awali kuona maji yanatoka katika mabomba ilikuwa nadra sana. Sasa kila siku maji yanatoka tu, imenilazimu sana ninue shower bafuni.
Nauliza tu ni huku Ubungo pekee au ni Dar nzima? na nini kimetokea? hatujazoea mambo haya.
Kama hali ikiendelea hivi ajira za watu zitakuwa mashakani .
yaani sie kuogea kwenye ndoo na makopo tushasahahu, mambo yoote kwa shower tuu