Maji yanatoka mfululizo Dar, inashangaza sana

Maji yanatoka mfululizo Dar, inashangaza sana

hongera kwao,hata huku kwetu maji yanatoka deile yakikatika ni mara mojamoja sana.
Umeme pia umekuwa haukatikikatiki mara kwa mara kama zamani
 
Ni zaidi ya wiki mbili na kama sijakosea itakua ya tatu kumetokea jambo ambalo ni la kustaajabisha kidogo katika jiji hili.

Hapa ninapokaa (Ubungo Msewe) hapo awali kuona maji yanatoka katika mabomba ilikuwa nadra sana. Sasa kila siku maji yanatoka tu, imenilazimu sana ninue shower bafuni.

Nauliza tu ni huku Ubungo pekee au ni Dar nzima? na nini kimetokea? hatujazoea mambo haya.

Kama hali ikiendelea hivi ajira za watu zitakuwa mashakani .

Kweli Watanzania tumezoea shida.
 
Hapa ninapokaa (Ubungo Msewe) hapo awali kuona maji yanatoka katika mabomba ilikuwa nadra sana. Sasa kila siku maji yanatoka tu, imenilazimu sana ninue shower bafuni.

Nauliza tu ni huku Ubungo pekee au ni Dar nzima? na nini kimetokea? hatujazoea mambo haya.

Kama hali ikiendelea hivi ajira za watu zitakuwa mashakani .
Kwa wiki mbili mfululizo dereva anayeniletea maji alikuwa ananitumia text kuwa maji yanaisha lini aniletee? Nikamchunia ila jana nikabidi nimwambie ukweli kuwa sasa hivi tunapata maji ya DAWASA... Nadhani kimoyo moyo kasikitika sana kupoteza mteja wa uhakika...
 
Ni kazi ya serikali kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana, ni kazi yako pia kulipa kodi na bili ya hayo maji.. Serikali imefanya kazi yake...bado ihakikishe inatimiza majukumu yake kila pahala watanzania wote wapate huduma hii muhimu..
 
Hongera Mh Rais wetu mpendwa kwa kufanya kz kwa vtendo co porojo ukisaidiwa na Mkuu wako wa Mkowa wa Dar wasio wapenda watafute nchi ya kuishi kwa muda muda wenu wa uwongizi ukiisha wtarudi
[HASHTAG]#Viva[/HASHTAG] Magufuli
[HASHTAG]#Hapa[/HASHTAG] kzi tu
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] kwanza majungu baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunzeni kuzoea mambo mazuri yawazoee, sasa kama kila siku mnalia shida tu kwanini zisiwaandame mpaka mshangae maji kutoka kwenye bomba.

Huo ni mwanzo tu wa matokeo ya utendaji wa awamu ya 5.
 
Sijuti kuwa Raia wa Nchi inayoongozwa na Mstahiki Mheshimiwa Amiri Jeshi Mtu wa Watu Dkt John Pombe Joseph Magufuli!

Pamoja na kupoteza Pato kwny Kisima changu Kikongwe kwa dhati ya Moyo wangu nampa hongera sana Ndugu Rais kwa uchapakazi usiomithilika tangu kuumbwa kwa Ulimwengu huu!

Kama Si kikwazo cha Katiba nami ningetamani Dkt Magufuli atawale Milele Tanzania!
 
Nashauri Temeke nayo iungwe katika bomba la Ruvu, maana mahitaji yameingezeka na chanzo cha maji cha mtoni hakikidhi mahitaji, maji ni shida kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ndiyo ya muhimu sasa...
Sasa jingalao na stroke wamekuja kwa speed baada ya kusikia jamaa yao kasifiwa,,mweeeee
Jifunzeni kuzoea mambo mazuri yawazoee, sasa kama kila siku mnalia shida tu kwanini zisiwaandame mpaka mshangae maji kutoka kwenye bomba.

Huo ni mwanzo tu wa matokeo ya utendaji wa awamu ya 5.
 
Back
Top Bottom