KERO Responded Mwanza: Changamoto kubwa ya maji, mamlaka ziseme ukweli

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Lyetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
1,388
Reaction score
3,718
Kumekuwa na changamoto kubwa ya maji mkoa wa Mwanza haswa wilaya za Nyamagana na Ilemela. Baadhi ya maeneo hayajapata maji kwa wiki mbili na mamlaka kupitia idara yao ya huduma kwa wateja zinasema kuna upungufu wa umeme kwenye vituo vya uzalishaji na usambazaji wa maji.

Kwapicha halisi ya changamoto ni vituo vyote vya uzalishaji na usambazaji vimeathiriwa na huo upungufu wa nishati kwasababu maeneo mengi hayapati maji na mengine yanapata kidogo.

Mamlaka (TANESCO, MWAUWASA) zitoe ufafanuzi zaidi, tunachangamoto ya upungufu wa umeme nchini au kwa baadhi ya mikoa?

Kama ndio, huu upungufu wa umeme nchini au kwa baadhi ya mikoa umesababishwa na nini?

Kama hakuna changamoto, huu upungufu wa nishati kwenye vituo vya kuzalisha na kusambaza maji mkoa wa Mwanza unasababishwa na nini?

Pia soma: MWAUWASA: Kukosekana kwa huduma Uzalishaji na Usambazaji wa Maji Mwanza imetokana na hitilafu ya umeme
 
Katika majiji ambayo hayakupaswa kuwa na ukosefu wa maji ni pamoja na Mwanza. Kibiashara ni eneo muhimu kwa nchi, uwingi wake wa watu, sekta ya kilimo na mwisho wanaziwa na chemchem nyingi.
 
hayo maeneo umetaja kutoka ziwani ni meter au km chache sana ila hayana maji miaka hii 6 tangu Uhuru kwa mjibu wa Dr. Mollel aliesema tanzania ina miaka 6 tangu ipate Uhuru!!! sasa fikiria sehemu ambazo hazina Ziwa!! ukweli mimi naona baada ya kifo cha Magufuli tumerudi nyuma sanaaa uongozi ni dhaifu sana hakuna anaejali kazi zake wala kuwa na uwajibikaji kwa kazi!! imebakia ni kupiga dili kuuza Open space zote, kuuza rasilimali zote za nchi na kujenga majumba Dubai!!
 
Tuisome namba tu hakuna namna.
Uzuri hata mbogamboga hayo maji hawayaoni.
 
Siasa hizo!!

Kahama na Shinyanga maji ni 24/7 kutoka ziwa Victoria au ni vituo tofauti na hivyo vya MWAUWASA?
 
Kumekuwa na changamoto kubwa ya maji mkoa wa Mwanza haswa wilaya za Nyamagana na Ilemela. Baadhi ya maeneo hayajapata maji kwa wiki mbili na mamlaka kupitia idara yao ya huduma kwa wateja zinasema kuna upungufu wa umeme kwenye vituo vya uzalishaji na usambazaji wa maji.

Kwapicha halisi ya changamoto ni vituo vyote vya uzalishaji na usambazaji vimeathiriwa na huo upungufu wa nishati kwasababu maeneo mengi hayapati maji na mengine yanapata kidogo.

Mamlaka (TANESCO, MWAUWASA) zitoe ufafanuzi zaidi, tunachangamoto ya upungufu wa umeme nchini au kwa baadhi ya mikoa?

Kama ndio, huu upungufu wa umeme nchini au kwa baadhi ya mikoa umesababishwa na nini?

Kama hakuna changamoto, huu upungufu wa nishati kwenye vituo vya kuzalisha na kusambaza maji mkoa wa Mwanza unasababishwa na nini?

Pia soma: MWAUWASA: Kukosekana kwa huduma Uzalishaji na Usambazaji wa Maji Mwanza imetokana na hitilafu ya umeme
Ningekua Rais ningewafukuza wakurugenzi wa Mwanza

Lwa jinsi Mwanza ilivyo na changamoto za maji, umeme, barabarayani sioni umuhim wa serikali kwenye jii hili
 
Back
Top Bottom