Maji ya kujaza kwenye battery ya solar

Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,280
3,345
Wajumbe heshima yenu, tafadhali msaada kwenye tuta, maji ya betri ya solar yanapoisha, ni maji gani sahihi ya kuyaweka kama replacement ya maji ya mwanzo?

Je ni maji makali? Au maji baridi? Maana nilishauriwa kuwa mwanzo kuwa maji ya kwanza makali yanapoisha basi maji ya pili yanapaswa kuwa ya baridi unayamwaga yote ya kwanza kisha unajaza ya baridi, nimefanya hivyo kwenye battery langu la kwanza la n 100 la binslum ila ndo likaisha nguvu kabisa kiasi cha usiku linadumu na nguvu kwa muda wa dk 30-50 tu, hvyo sasa nimenunua battery lingne na sitaki kukosea hivyo naombeni muongozo? Pia ni upi utaratibu sahihi wa kubadilisha au kuongeza maji mapya?
 
Kwa ninavyoelewa:
Battery ya solar ni Dry , Sealed lead acid battery. Battery za namna hii iwe ni ya solar au ya gari huwa haziongezwi maji. Ndio maana zinaitwa SEALED LEAD ACID BATTERY. Inamaanisha kwamba battery hii iko SEALED na kuifungua ni kuibomoa na kuiharibu.

Kama kweli battery yako ni DRY basi itakuwa na indicator ya life ya battery ambayo inakuwa na kioo chenye rangi kwa ndani, battery ikiwa nzima indicator inakuwa na rangi Kijani, na ikiwa Nyekundu basi battery imefikia mwisho wa maisha, ingawa indicator hii sio ya kuiamini sana.
 
Usisubiri maji ya betri yaishe ndipo uongeze ila kuna alama zipo mbili kwenye betri, Upper na Lower, hivyo maji yanapokuwa kwenye mustari wa Lower unatakiwa kuongeza maji baridi kwa sababu unakuta bado mle ndani ya betri kuna acid ya maji makali yaliyowekwa kabla ya matumizi.
 
Usisubiri maji ya betri yaishe ndipo uongeze ila kuna alama zipo mbili kwenye betri, Upper na Lower, hivyo maji yanapokuwa kwenye mustari wa Lower unatakiwa kuongeza maji baridi kwa sababu unakuta bado mle ndani ya betri kuna acid ya maji makali yaliyowekwa kabla ya matumizi.

Sent from my cupboard using mug

Nimeipenda "Sent from my cupboard using mug"🤣🤣🤣😂😂
 
Tumia maji baridi, Distiled water. Maji makali ni mara ya kwanza tuuu au ukifanya maintenance kubwa
 
Back
Top Bottom