Maji ukiyatumia vizuri haina haja ya KIOO..

Maji ukiyatumia vizuri haina haja ya KIOO..

G nako is the best,fid q na Joh
Hahah.. Hao ni wanafanya hiphop ila sio [HASHTAG]#Actual[/HASHTAG] Hiphop.. U knw y?

Hawana skendo ya kufungiwa nyimbo zao kwa sabab wanaimba hiphop isiyogusa MAISHA ya MTANZANIA kwa namna moja au nyingine.. Wao ni entertainers mfano huyu FID Q.. zamani alikuwa katika ILE core yya actual hiphop ila kwa sasa anazid kupoteza loyalty.. Soo sad.. G nako nae.. Hana tofaut na Ben pol tu..

[HASHTAG]#myVIEWS[/HASHTAG]
 
Lyrics:1
Nilikuwa kituoni nikingoja daladala/
Nikamuona manzi mmoja akivuka barabara/
Viatu mchuchumio na Ana mdomo ka chuchunge/
Nikaona kwanza nivunge ningoje mpaka avuke/
Mkononi Ana mkoba mwekundu bastola nundu/
Sikuwa na mapepe nilikuwa nimepoa kizungu/
Hakuna aliyenishuku kituoni sikuwa mwendaji/
Kumbe mwendawazimu Mission Town Mbumba Mpigaji/
Nimenyuka nimevunja duka mavazi/
Mfukoni mboli imetuna kizushi kumbe makadi tu/
Na attitude /
Ya utanashati ili mradi tu/Udwanzi mtupu na siachi MTU/
Nikamgusa bega la kulia/
Wakati huo kushoto amegeukia/
Unajua nini ilifuatia/
Nikamnyang’anya alichoshika/
Akapiga kelele za mwizi umati ukaitika/
Wengine na vitofa vishoka vigoda/
Sauti za tumuue tumuue zikasikika pamoja/
Akatokea jamaa si ndo akahoji kwanza kisa/
Nikawaambia Mi sio mwizi ila mwizi ni huyu sista/
Lyrics:2
Haikuwa rahisi kueleweka/
Wananchi wenye hasira wanahisi kunifyeka kuniteka kuniSILA/
Nikiwa nimemshika mkono asiponyoke/
Jazba kibao natusi kizungu japo ndo broken/
Nikawaambia wazee kwanza naomba mtulie/
Huyu dem hamfahamu ngoja story niwapatie/Ilikuwa Mombasa nyamaza Dada usilie/
Siku ile beach na wenzako mkaniomba niwanunulie/
Mitungi na misosi na swimming niwalipie/
Muogelee mpige picha kwa Insta mkazitupie/
Baada ya bata ndefu nikaomba uniachie /
Namba yako nikitoka baadae nikupigie/
Nikupitie tukalegeze chaga we na mie/
Kipi kilikufanya shetani likuingie/
Baada ya mapenzi dawa ya usingizi unipulizie/
Uniibie Mali zangu na kisha unikimbie/
Mtoto mzuri Kama Wewe unafaa hata kuwa mbunge/
Unaishi kwa utapeli maisha mguu ndani mguu nje/
Najilipa hii pochi simu na pesa zake/
Zote alizonazo nasepa na asinifuate/
Lyrics:3
RAIA wakashusha zana zao zote chini/
Ghafla wakamchenchia yule Dada wa watu maskini/
Kwa kuwa niliongea kwa hasira na kujiamini/
Wakamponda sista duu mzima na kimini/
Unajitia mjanja umeibia mtoto wa mjini/
Ya mwizi ni siku moja siku hizi si arobaini/
Mwana kakuchaisa na kisha kaingia mitini/
Oya jama tuondokeni alie analia nini/
Ukweli ni kwamba hakuniibia/
Ule ni mchezo tu ambao nilimpangia/
Ukiniona mtaani kaa mbali/
Nitakupora hiyo SAA ya mshale/
By @nikkimbish 2018
 
Back
Top Bottom