Hakuna ubishi kwamba maji ni muhimu. Labda swali kwa Mh. Zitto ni kwamba, analysis hiyo ya gharama ya maji kwa watu wa vijijini, ni kweli kwamba wananchi hao wanacho kipato cha kiasi hicho? Kama maji tu gharama yake ni hiyo, je, mahitaji mengine yanagharimu kiasi gani na kwa kipato kipi?
Aidha, tunapaswa kujiuliza, ni kwa nini vyanzo vya maji vilivyokuwa vinatiririsha maji siku za nyuma vimekauka na kupelekea kuzuka tatizo la maji vijijini?
Kuhusu miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji ni muhimu pia kwa vile kutokuwa na ubora unaotakiwa, muda wa uzalishaji na namna ya kufikia masoko huathirika.
Hebu fikiria, kwa mfano; kuna kipindi watu walilalamikia foleni ya magari jijini Dar es Salaam kwamba ilikuwa inatia nchi hasara kwa vile muda mrefu ulikuwa ukitumika kwenye safari badala ya uzalishaji.
Inashangaza na kusikitisha mtu anapokebehi jitihada za kupunguza msongamano wa magari kwa jiji kama la Dar es Salaam.
Cha msingi, nafikiri, ni kuhakikisha kwamba tunatunza vyanzo vya maji na kuhakikisha kwamba miundo mbinu inayojengwa na serikali au wadau wengineo wa maji inajengwa kwa viwango na kulindwa na watumiaji wa maji na wananchi kwa ujumla. Namna nyingine ni kujenga utamaduni wa kuvuna maji ya mvua.
Kama wananchi wa vijijini wanao uwezo wa kutumia kiasi hicho kilichosemwa na Mh.
Zitto kwenye kukabiliana na tatizo la maji, iweje wasiwe na uwezo wa kujenga au kununua matenki ili wayatumie kuvuna maji ya mvua? Au iweje halmashauri za Wilaya zisiwe na mkakati wa kujenga mabwawa ili kuvuna maji ya mvua vijijini?