Chanzo Mafuriko ya Rujifi ni Wananchi kuvamia mkondo wa maji na sio Bwawa la JNHPP

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,375
50,177
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Tanesco ni kwamba kilichosababisha Mafuriko huko Rufiji ni Wananchi waliovamia mkondo wa Maji na Sio Bwawa la Nyerere.

Mhandisi huyo mbobezi amenukuliwa akisema mwaka 1974 kiwango Cha maji mtonrufiji kiliwaho kufikia MITA za ujaza 13,000 Kwa sekunde na hakuna Mafuriko yaliyotokea ,Sasa iweje maji ya Sasa ya MITA za ujaza 8,000 yasababishe Mafuriko? Alihoji bwana huyo.

View: https://www.instagram.com/p/C5iznPzozWe/?igsh=MTR4cXM5cnUwdmxkMQ==

My Take
TANESCO na Serikali acheni kucheza na maisha ya watu,watendeeni kama binadamu Kwa kuwahamisha kwenye mkondo wa Maji yenye Kasi kubwa kutoka bwawa la Nyerere badala ya kuleta kejeli na dhihaka.

View: https://twitter.com/HabariLeo/status/1777699272433025434?t=VjVJUYaoj42IiGKm1-QNaQ&s=19
 
View: https://www.instagram.com/p/C5iybKwIpf1/?igsh=aHR6c3djbDJxbjNi

Huyo mhandisi sna akili mbovu sana.
 
Serikali imenukuu baadhi ya watu humu Jf, ambao pia walikuwa wanasema wananchi eti ndo wamevamia njia ya maji,

Hii nchi ina laana hatupendani sisi kwa sisi, yaani mtu bora akomolewe mwananchi mwenzie ili yeye atetee chama au serikali tu,

Hapo kuna watu wanatamani sasa hao wana rufiji waondolewe hata mia wasipewe iyo kwao ndo furaha kuu,tena mwingine anachanganya na udini kbs, kwa laana tuliyonayo ndiomaana hata mitimu yetu ya mpira haifiki popote kimataifa ,hadi litimu la taifa,

Angalia walichofanyiwaga watu wa kimara kuvunjiwa nyumba zao na yule ibilisi, tumelaaniwa sana
 
Uongozi wa CCM unajaribu kutumia kila njia kuonyesha hili tatizo halijasababishwa na Bwawa la Nyerere. Wanasiasa sasa ndio wamekuwa mainjinia wa kutoa ufafanuzi, na mainjinia wako kimya. Wenye akili wote wanajua kwamba tatizo ni kwamba Bwawa la Nyerere lilijazwa maji kupita kiasi, na walipogundua hili wakaamua kufungulia maji mengi kulinusuru bwawa na kuepuka mafuriko makubwa hata zaidi ambayo yangeleta maafa makubwa sana. Lakini hawataki kukiri hili na kusema ukweli. Mbaya zaidi, wanawalaumu wananchi ambao wamewasababishia haya matatizo. Hawa ni viongozi wauaji na wanastahili adhabu ya kifo.

Tunajua kuna wahandisi kama huyu, kwa sababu tu ya kulinda ugali wao, wamekubali kutumika kisiasa, kama tu karatasi ya chooni inayotumika mara moja na kutupwa. Tunawaelewa, lakini wanapaswa pia kuelewa wanashiriki dhambi ya wanasiasa. Tunatumaini dhamiri zao zitawishitaki.

Sasa kila mtu mjinga na akubali maelezo ya wanasiasa ambao wala sio wataalamu wa maji, lakini maelezo yao hayabadili ukweli kwamba mafuriko yanayotokea Rufiji ni upumbavu wa viongozi wa kisiasa kujifanya wanajua kuliko wataalamu wetu.
 
Jina la muhandisi wapi?
Kuna watu wanafikiri kila mfanyakazi wa Tanesco ni Mhandisi. Maelezo kama haya ya kisiasa yatakuwa yametolowa na mtu ambae wanajua hajui kilichosababisha mafuriko na atasema kama alivyoelekezwa aseme. Kama kweli ni mhandisi, labda ndio maana hata jina hawakuonyesha, asije akasutwa na wahandizi wenzake wanaoelewa kilichotokea
 
Kuna watu wanafikiri kila mfanyakazi wa Tanesco ni Mhandisi. Maelezo kama haya ya kisiasa yatakuwa yametolowa na mtu ambae wanajua hajui kilichosababisha mafuriko n atasema kama alivyoelekezwa aseme. Kama kweli ni mhandisi, labda ndio maana hata jina hawakuonyesha, asije akasutwa na wahandizi wenzake wanaoelewa kilichotokea
Na mimi nimehisi hivo. Mtu mwenye taaluma yake kuongea hayo duh. Kwanza ni nje ya field yake kabisa. Hayo ilibidi yasemwe na mtu wa Bonde la Wami Ruvu
 
Watanzania sio wajinga.
Watanzania wajinga ni wengi sana, ndio maana wanasiasa wanajua watakubali huu utumbo wanaoutoa kuhusu kitu gani kimesababisha mafuriko. Bwawa hili limekuwa na maamuzi mengi ya kisiasa ili CCM wapate ujiko. Sasa wanatapatapa kusema nini kimeleta mafuriko, na hawataki kusema ukweli. Kwanza mvua nyingi. Pili wananchi wenyewe, bado kidogo watasema ni wanasiasa wa upinzani wamelihujumu bwawa la Nyerere na kusababisha mafuriko. Wakisema hivyo, kuna Watanzania wataamini.
 
Alisema moja ya adui wetu ni ujinga.

Halikwepeki hilo.
Sawa kabisa, na ujinga mwingi upo katika viongozi wanasiasa walio madarakani, na kwa watu wanaowaweka katika hizo nafasi. Haya makundi mawili ni adui zetu wakubwa sana. Lakini angalau wana akili ya kuwaogopa diaspora kuleta mawazo mbadala nchini ya kuwatoa wananchi toka mental slavery walipowaweka. Ndio maana wanasema dual citizenship ni hatari kwa usalama wetu - usalama wao!
 
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Tanesco ni kwamba kilichosababisha Mafuriko huko Rufiji ni Wananchi waliovamia mkondo wa Maji na Sio Bwawa la Nyerere.

Mhandisi huyo mbobezi amenukuliwa akisema mwaka 1974 kiwango Cha maji mtonrufiji kiliwaho kufikia MITA za ujaza 13,000 Kwa sekunde na hakuna Mafuriko yaliyotokea ,Sasa iweje maji ya Sasa ya MITA za ujaza 8,000 yasababishe Mafuriko? Alihoji bwana huyo.

View: https://www.instagram.com/p/C5iznPzozWe/?igsh=MTR4cXM5cnUwdmxkMQ==

My Take
TANESCO na Serikali acheni kucheza na maisha ya watu,watendeeni kama binadamu Kwa kuwahamisha kwenye mkondo wa Maji yenye Kasi kubwa kutoka bwawa la Nyerere badala ya kuleta kejeli na dhihaka.

View: https://twitter.com/HabariLeo/status/1777699272433025434?t=VjVJUYaoj42IiGKm1-QNaQ&s=19

Maelezo haya ni dharau kubwa kwa wananchi inayofanywa kwa maksudi na viongizi wa serikali.

Wanasema eti wananchi walivamia mkondo wa maji mara tu walipoanza kujaza bwawa na maji kupungua ktk maeneo ya mkondo ndipo wananchi wakajenga na kufanya shughuli nyinginezo za uzalishaji, huu uongo ni mkubwa Sana.

Ushahidi wa wazi dhidi ya uongo huu tumeushuhudia katika vyombo vya habari tukiona nyumba zenye bati zilizochakaa Sana kwa kutu kudhihirisha kuwa nyumba hizo zilijengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita kabla ya mradi huo kujengwa. Leo hii kiongozi mpumbavu asiye na huruma, utu, wala ubinadamu anaona fahari kuhujumu uhai na haki nyingine za raia na ufunika uovu huo kwa uongo mkubwa kiasi hiki .

Hakika hili halivumiliki katika mioyo ya wananchi , na kwa kuwa limeelezwa kisiasa basi wanasiasa wa upinzani wafike eneo la tukio kuuona ukweli nao waihabarishe jamii yaliyo ya kweli yanayofichwa na serikali. Hii ni kwa sababu hata baadhi ya vyombo vya habari kwa sasa vipo chini ya kibano kikali ktk kutoa habari kamili
 
Back
Top Bottom