Maji ni Mtego wa Umasikini (poverty trap)

Maji ni Mtego wa Umasikini (poverty trap)

Sawa, Bunge liko wapi katika hili? naamini unasukumwa kusema hivi kwa sababu majimbo mengi yaliyorudiwa uchaguzi chama chako kimepoteza nafasi.
Wazee wa ndioo Bunge ni akina nani?

Wabunge wengi ni wa Chama gani?

Kwa nini hao hao wabunge ambao wana nguvu kupitisha mambo wanashindwa kukemea haya mambo ya kipuuzi?

Hata kama chama chochote cha upinzani kingeshinda hasara ni ileile, Serikali badala ya kujikita kufanya miradi mbali mbali kama hili suala la maji vijijini yenyewe inajikita kwenye marudio ya uchaguzi.

Hivi kweli tuna nia na nchi ya Viwanda na uchumi wa kati ilihali kuchimba visima vya maji imetushinda? Tuko serious kweli!!

Serikali inatakiwa ikubali juu ya matatizo muhimu kama haya na kuyapatia ufumbuzi kuliko na kuhangaika na mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na tija kwa Taifa.
 
Mkuu unajua vijijini kuna watu wananunua Maji ya dumu la Lita 20 kwa shilingi mia tano, una jua kuna sehemu watu wamevuta mabomba lakini unapita mwezi Maji hayajatoka?

Vijijini hali ya upatikani ni mbaya sana na wananchi wake ni masikini.
Uko sahihi mkuu
 
Tangu mwaka huu uanze leo ndio umezungumza jambo la maana.

Tunataka viongozi wa kisiasa waikosoe na kui-challange serikali kwa hoja za msingi na sio kuleta hoja za kuchochea chuki, udini, ukabila, kuhamasisha maandamano yasiyokuwa na tija na mwisho wa siku wanaokuja kuumia ni wananchi masikini na sio nyie ambao mmeanzisha uchochezi.
 
Udhaifu na kutokuwa na kipaumbele kwa viongozi wetu ndiyo tatizo.

Jimbo la Hanang limeongozwa na Waziri Mkuu, hajawafanyia chochote wana Hanang hawezi kusingizia chochote alikuwa ni kiongozi mkubwa serikalini. Baada ya hapo likaongozwa na Waziri wa siku nyingi mh Dr naye hajawafanyia chochote wana Hanang kwenye nyanja za maendeleo, kama maji, barabara, afya na elimu.

Leo hii Waziri Mkuu huyo wa zamani anawinda madaraka atufanyie nini?
 
Mnyalu pekee unayeburuzwa na Mbowe
Kwa sababu mtaji wenu ni umasikini kwa watu vijijini, sasa mkisikia watu wanalisema hili jambo mnatokwa mapovu maana mnajua mumeingilia ulaji wenu.

Mkumbuke pia kuna bomu mnaliandaa wenyewe likijakuwalipukia msije kusema hatukuwaambieni
 
Kutokuwa na vipaumbele vinavyogusa maisha ya wananchi hasa wa chini ni TATIZO kubwa kwa serikali..

Maji ndio UHAI wa Mwanadamu..

Popote pakishakuwepo na maji, Mwanadamu ataishi..

Unajiitaje Kiongozi wa wanyonge wakati hauwajali katika suala la muhimu kama maji??

Unanunua mindege kwa pesa cash halafu unatamba, mnyonge gani ana uwezo wa kupanda ndege..??

Upofu.

Kuna jamaa wengine wanaandaa maandamano ya kutetea siasa badala ya kutetea uchumi
 
Tolea maelezo hii barua Zitto
e9ea720a2230d6f8228d989a162c4e94.jpg

b9ac483f7765593dde14e79e7c79dddb.jpg
 
Wazee wa ndioo Bunge ni akina nani?

Wabunge wengi ni wa Chama gani?

Kwa nini hao hao wabunge ambao wana nguvu kupitisha mambo wanashindwa kukemea haya mambo ya kipuuzi?

Hata kama chama chochote cha upinzani kingeshinda hasara ni ileile, Serikali badala ya kujikita kufanya miradi mbali mbali kama hili suala la maji vijijini yenyewe inajikita kwenye marudio ya uchaguzi.

Hivi kweli tuna nia na nchi ya Viwanda na uchumi wa kati ilihali kuchimba visima vya maji imetushinda? Tuko serious kweli!!

Serikali inatakiwa ikubali juu ya matatizo muhimu kama haya na kuyapatia ufumbuzi kuliko na kuhangaika na mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na tija kwa Taifa.

Wingi wa wabunge siyo sababu ya kupitisha hoja za hovyo hovyo bungeni, nadhani wewe unazungumzia bunge la awamu ya mzee Pius Msekwa na siyo hili bunge la mzee wa viwango(R.I.P) na mama makinda.

Mkuu unaongea nini hiki, tafuta dodoso la sheria za uchaguzi soma. serikalini hakuna siasa, siasa ziko kwenye vyama huku. serikalini ni utendaji tu kwa kufwata kanuni na taratibu za nchi.

Mkuu, October, 2011 chama chako kilipokea msaada wa kuchimbiwa visima 200 nchi nzima na mzee Sabodo kwa kila jimbo lililotoa mbunge wa chama chako, nikuulize swali la kipuuzi tu, Hivyo visima viko wapi katika hayo majimbo ya wabunge wako?

Tuache mahaba na ushabiki, serikali kuu haiwezi kukufanyia kila kitu. Wewe kama Mtanzania umewajibika kiasi gani kuhakikisha mtaani/ kijijini kwako kuna kisima cha maji? Tuna madiwani wa itikadi tofauti na watendaji wa serikali za mitaa wa itikadi tofauti.

Ukiwa Mtanzania mwenye mahaba na nchi yake, mwenye kujiskia raha kuitwa Mtanzania na Mwenye makuzi ya kitanzania. Hupaswi kuongea maneno ya namna hiyo. Hivyo huna budi kutengua kauli yako. "kuhangaika na mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na tija kwa Taifa"

Shukrani!
 
Ama kweli ni nchi yenye mataifa mawili tofauti.

Kuna kipindi nilienda sehemu moja huko wilayani Chemba kijijini kina mama wanachota maji kwenye kisima kirefu kweli. ngazi yenyewe mti halafu ukiwaangalia umri nao kikwazo kwao lakini lazima watumie maji. Wanahangaika sana kuyapata maji na ukiangalia uhalisia wa maisha yao haikuhitaji utumie hata elimu ya astashahada kujua umasikini wao. They are a true definition of poverty. Wako trapped deeply in cycle of poverty.

Sijajua kuhusu magonjwa ya tumbo huko Kwamtoro, Chemba ila sidhani kama wako salama.

Hali inafanana sana nchi hii {kwa maeneo ya vijijini}, na ndiko umasikini ulikoshamiri.
 
Ukiacha siasa hili tatizo la maji ni fursa sana marehemu mama yangu aliwahi niambia kuwa
"popote penye shida kubwa basi ni fursa kwako badili mtazamo wako juu ya hili tatizo" niliishi Tanzania sehemu yenye shida kubwa sana ya maji.

Baada ya kurudi home nilijichanga nikachimba kisima kikubwa now ninapata faida ya 100k per day. Sasa imajini kwa mwezi napata sh ngapi? Na ninauza maji kwa shilingi 100 tu kwa ndoo na 100 kwa ng'ombe na 50 kwa mbuzi. Na mengine nimevuta kwenye shule mbili sasa

So nia yangu sio kuwaambia nini napata katika project hii ila ni kuwabadili mind set na kuchngamkia hii fursa jamani.

Hatuwezi kaa na kuilaumu serikali kila siku wakati sie tumekaa. Kumbukeni kuwa kufanya ni vigumu sana kuliko kukosoa.

Sasa, hima amkeni ingieni vijijini jichangeni mfanye huu mradi utaniambia kama utasikia vyuma.

"REMEMBER ALWAYS BE THE PILOT OF YOUR OWN DESTINY AND LET NO ONE THINK ON YOUR BEHALF."
 
Aisee kumbe mnasikiliza ushauri eeeeeeeeeeeh hivyo ndivyo inavyotakiwa mnawainvolve wanajamii kwenye mambo ya maendeleo,na wao hawatawaangusha kwenye kura.sio mnaibuka tu from nowhere siku za uchaguzi.
 
Hiyo ni tafakari nzuri, siku nyingine weka video au audio, umeandika maneno mengi sana. Watu wetu wanashida nyingi sana na ramli nyingi sana zinapigwa lakini ukweli ni kwamba watu wetu hawajaelimika.

Ni hivi, hata wale walioenda shule mpaka wakapata PhD lakini hawajaelimika. Sehemu kubwa ya urabuni ni jangwa lakini wao wameendelea, muheshimiwa tafakari upya hypothesis yako.
 
Tatizo huwa ukiandika unakimbia bila kujibu michango ya wengine
 
Serikari ya mweshimiwa magufuri ikae ichunguze kwa makini , njia gani itasaidia kupeleka maji safi vijijini, ni aibu sana kijiji kikawa na mto km 10 /15, lakini kikakosa maji ya bomba., kama ilivyofanya usambazaji wa umeme kupitia REA , basi hata maji wafanye hvyo.
 
Ukiacha siasa hili tatizo la maji ni fursa sana marehemu mama yangu aliwahi niambia kuwa
"popote penye shida kubwa basi ni fursa kwako badili mtazamo wako juu ya hili tatzo" niliishi Tanzania sehemu yenye shida kubwa sana ya maji.
baada ya kurudi home nilijichanga nikachimba kisima kikubwa now ninapata faida ya 100k per day. Sasa imajini kwa mwez napata sh ngapi?? na ninauza maji kwa shilingi 100 tu kwa ndoo na 100 kwa ng'ombe na 50 kwa mbuzi. na mengine nimevuta kwenye shule mbili sasa

So nia yangu sio kuwaambia nini napata katika project hii ila ni kuwabadili mind set na kuchngamkia hii fursa jamani.
hatuwezi kaa na kuilaumu serikali kila siku wakati sie tumekaa
kmbukeni kuwa kufanya ni vigumu sana kuliko kukosoa.

sasa hima amkeni ingien vijijini jichangeni mfanye huu mradi utaniambia kama utasikia vyuma.

"REMEMBER ALWAYS BE THE PILOT OF YOUR OWN DESTINY AND LET NO ONE THINK ON YOUR BEHALF."
Nimekuelewa vema mkuu namna ulivyo weza tatua changamoto ya maji na kuwa fursa ya kiuchumi kwako.

Ukipata muda nikuombe utuchanganulie gharama zake na mambo gani ya muhimu kuzingatia.
Ahsante.
 
Ni aibu sana kwa taifa lililo na mazingira kama yetu kuwa na tatizo la maji. Aibu kwa watawala kuishi katika kila aina ya privilege wakati hawataki kutoa nafasi angalau ya watu wengine kutoa mawazo yao kuhusu mustakabali wa nchi yetu.
Ni aibu sana.
 
Tunashindwaje kuchimba visima kila ward ikiwa tuna pesa za kununulia Vichwa vya treni visivyokuwa na mwenyewe?
 
Kutokuwa na vipaumbele vinavyogusa maisha ya wananchi hasa wa chini ni TATIZO kubwa kwa serikali..

Maji ndio UHAI wa Mwanadamu..

Popote pakishakuwepo na maji, Mwanadamu ataishi..

Unajiitaje Kiongozi wa wanyonge wakati hauwajali katika suala la muhimu kama maji??

Unanunua mindege kwa pesa cash halafu unatamba, mnyonge gani ana uwezo wa kupanda ndege..??

Upofu.
Tatizo sio Rais, tatizo viongozi wengi wa Halmashauri sio wabunifu

Tatizo lipo kubwa sana kwa viongozi wetu, Mie nahisi viongozi wengi wa Halmashauri sio wabunifu, wanashindwa kabisa kuziona changamoto za wananchi na kuzitatua zinapotokea, sina budi kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, anajaribu kuonesha kidogo ubunifu, basi hata wilaya nyingine hawana budi kuiga.
 
Back
Top Bottom