• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Maji ni Mtego wa Umasikini (poverty trap)

Zitto

Zitto

MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Messages
1,473
Points
2,000
Zitto

Zitto

MP Kigoma Urban
Joined Mar 2, 2007
1,473 2,000
Changamoto ya Maji inachangia sana kuwashikilia watu wa vijijini kwenye dimbwi la umasikini na kuongeza tofauti ya kipato Kati ya mijini na vijijini na kati ya wenye nacho na wasio nacho. Gharama za maji ni kubwa mno maeneo ya vijijini kiasi kwamba zinazidi wastani wa pato la mtu mmoja ( per capital income) kwa siku nchini Tanzania.

“Pato la Taifa mwaka 2016 lilikuwa shilingi milioni 103,744,606 kwa bei za mwaka husika. Aidha, idadi ya watu Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa watu 48,676,698 mwaka 2016. Hivyo, Pato la wastani la kila mtu lilikuwa shilingi 2,131,299 mwaka 2016 ikilinganishwa na shilingi 1,918,897 mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 11.1. Pato la wastani kwa kila mtu katika Dola za Marekani liliongezeka kutoka Dola 967.5 mwaka 2015 hadi Dola 979.1 mwaka 2016 ikichangiwa na kupungua kwa kasi ya kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. Mwaka 2015, shilingi ya Tanzania ilipungua thamani dhidi ya dola ya Marekani kwa asilimia 16.8 ikilinganishwa na asilimia 8.8 mwaka 2016.” Hali ya Uchumi wa Taifa Juni 30, 2017. Kwa kutumia takwimu hizi za Serikali Ina maana kila Mtanzania ana kipato cha wastani wa shilingi 2.1 milioni Sawa na USD 980 kwa mwaka.

Hanang wanatumia kipato chao kikubwa kununua Maji

Mwananchi wa kijiji cha Gehandu Huko Hanang Mkoa wa Manyara ananunua maji pipa moja la lita 200 kwa shilingi 7000 na familia moja inahitaji angalau pipa moja kwa siku kwa matumizi ya kujibana kabisa ya maji. Kwa hiyo mwananchi huyu atahitaji takribani shilingi 2.5 milioni kwa mwaka kwa ajili ya Maji tu ya kutumia yeye na familia yake. Kwa familia ya Watu 6, huu ni wastani wa 16% ya kipato cha kila mwanafamilia hata mtoto mdogo wa siku 1 kutumika kununua Maji.

Hivyo familia moja inatumia wastani wa kipato cha mtu mmoja kwa mwaka kwa ajili ya Maji tu. Lazima familia hii iendelee kushikwa kwenye mtego wa umasikini. Mwananchi mmoja kijijini Gehandu alitueleza kuwa bajeti yake yote inaishia kwenye maji wakati wa kiangazi. Alieleza kwa uchungu sana namna anaamka saa 10 alfajiri kufuata Maji kilometa 20 kutoka nyumbani kwake na huko huchukua muda mrefu kwani foleni ni kubwa sana. Hanang hutumia sana Punda kubeba Maji na hubidi wakati mwengine kuyafuata mpaka mkoa jirani wa Singida.

Mijini ni tofauti

Miji mingi nchini kwetu hupata maji kutoka mamlaka za Maji safi na salama. Wastani wa bei ya maji kwa pipa la lita 200 kwa mamlaka za maji nchini ni shilingi 300 tu. Mwananchi wa Uzunguni jijini Arusha au Mikocheni jijini Dar es Salaam au Shanty Town Manispaa ya Moshi au Capri Point jijini Mwanza hutumia wastani wa shilingi 108,000 kwa mwaka kama gharama za Maji kwa familia yake. Ikumbukwe kuwa maji yanayosambazwa na Mamlaka za Maji Mijini ni masafi, yana madawa ya kuua wadudu wanaosababisha magonjwa kama kuhara nk. Mtu wa mjini haoni mzigo mkubwa wa matumizi ya Maji kwenye kipato chake kwani ni chini ya 1% ya wastani wa kipato cha familia ( wastani wa familia 1 watu 6 ). Wakati kule Hanang familia itatumia kipato chote cha mwanafamilia mmoja kununua maji ya familia nzima, Arusha au Dar es Salaam familia itatumia 4% tu ya kipato cha mwanafamilia kugharamia maji ya familia nzima. Hii ni nchi moja yenye mataifa mawili!

Ni zaidi ya Maji

Kwa kuwa maji yanayotumiwa na watu wa vijijini si safi na salama, Wananchi hao hutumia fedha nyingine nyingi zaidi kwenye matibabu kutokana na magonjwa kama kuhara, kichocho, typhoid, amoebae na kadhalika. Serikali inaingia gharama kubwa kununua madawa ya kutibu magonjwa haya kwa watu wa vijijini pale ambapo dawa hizi zinapatikana. Lakini pia nguvu ya kufanya kazi za uzalishaji hupungua kwa sababu ya Watu kuwa na siha duni na hivyo mzunguko wa umasikini kuendelea kuzunguka. Kwa nchi ambayo haina Mfumo madhubuti wa Bima ya Afya kwa Wananchi wake, gharama za Afya kwa masikini ni kubwa mno.

Tufanye nini?

Serikali yeyote makini lazima ijikite kwenye kuboresha hali ya maisha ya Wananchi wake kwa kuwaondolea vikwazo vya Maendeleo na kuvunja mitego ya umasikini ( poverty traps ) inayowashika na kuwadidimiza kwenye umasikini. Maji safi na salama kwa gharama nafuu yaweza kuwa ni hatua kubwa ya kuwaondoa Wananchi kwenye mtego mmoja wapo wa umasikini ( water poverty trap ). Hivyo Serikali iwekeze vya kutosha kwenye usambazaji wa Maji vijijini.

Miradi ya Maji sio miradi rahisi sana hivyo kunahitajika fikra mpya Katika kupata fedha za kujenga miradi ya Maji, kutunza vyanzo vya maji na kuendesha miradi ya Maji. Katika kata ambazo ACT Wazalendo ina madiwani tumeona tufanye majaribio ya ushiriki wa Wananchi kupitia Jumuiya za watumiaji Maji na sekta binafsi Katika kusambaza maji na kuendesha miradi ya Maji. Tunafanya majaribio haya kata za Tomondo Morogoro, Gehandu Hanang na Sumbugu Misungwi. Kupitia majaribio haya tutaweza kuboresha na kushawishi sera ya Taifa ya Maji kutokana na ushahidi kwenye kata hizi.

Ni vizuri Serikali kutazama upya vipaumbele vyake vya kimaendeleo. Kwa mfano kuna tija kujenga barabara ya Morocco - Mwenge Kwa shilingi 80 bilioni wakati Wananchi wa Tomondo, Morogoro wanakunywa Maji na mifugo?

==========​
 
For the English Audience
ZITTO KABWE: WATER IS A POVERTY-TRAP

Economic Analyst and a Member of Parliament for Kigoma town, Zitto Kabwe, shares some useful insight on how the basic need, water, has been acting as a poverty-trap to people living in villages, sighting example of Hanang village in Manyara region.

In his remarks, Zitto says that Water shortage in Tanzania has been a problem for decades now; the problem being even bigger in rural villages. He says the challenge contributes in dragging rural communities down to poverty and widening the gap between urbaners and villagers, as well as the haves and the have-nots.

According to researchers and statistics, availability of Water in rural areas is much more costly compared to the situation in towns in terms of price and accessibility. He also notes that, contrary to urban areas, water supply in villages is very scarce and expensive due to poor infrastructures, hence the price gets higher because of high demand as per law of demand and supply.

Ironically, clean and safe water is adequately available in towns and cities at a cheaper price while in villages people buy contaminated water at a very high price with more expenses to be used in treating diseases like cholera, typhoid, amoebae etc derived from such untreated water.

Zitto advises the Government to collaborate with stakeholders and upgrade its strategies in dealing with the problem.

SOCIAL MEDIA VIBES WITH ZITTO

Originating from JamiiForums.com as posted by Zitto himself, users from other social networks such as Twitter and Facebook, picked the subject and brought it to the wider platforms for discussion.

The government is urged to improve people's lives especially those living in rural areas, so that they can afford paying for clean and safe water.

Others say Water must be prioritized ahead of other unnecessary developmental projects there may be. For instance, someone wondered how comes the government spends huge cash to purchase 7 air crafts at once, while there are people dying for lacking safe water?

"People can survive living without boarding planes, but not lacking water. We must set our priorities right", he insisted.

In a nutshell, Clean and Safe Water at a fair price, could play a big role in unlocking the poverty-trap in the villages, since the natives will not be spending a lot of money to access water. It is easy to accomplish this, only if the government will invest greatly in water supply to the rural areas.
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2015
Messages
4,226
Points
2,000
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined May 28, 2015
4,226 2,000
Ni sahihi sana, haiwezekani serikali ikawekeza ama kuanza na vipaumbele ambavyo havina manufaa kwa kiasi kikubwa kwa taifa. Na badala yake kusahau sekta muhimu kama ya maji.

Hata mheshimiwa Lema ashawahi kuliongea hili na kuishauri serikali, kuhusu umuhimu wa maji na kusema kuwa maji ni bidhaa muhimu, hivyo serikali inatakiwa ifanye bidii kufikisha maji maeneo mengi ya nchi yetu ili wananchi wasipate adha ya kufata maji umbali mrefu, na badala yake wajikite katika uzalishaji zaidi.
 
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
35,377
Points
2,000
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
35,377 2,000
Umerejea karibu, sehemu kwenye democracia
 
The CIA

The CIA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Messages
480
Points
500
The CIA

The CIA

JF-Expert Member
Joined May 5, 2017
480 500
Ukweli utaendelea kuwa ukweli.

Hakuna sababu ya kununua ndege nyingi na kwa mbwembwe, zikaishia kushikiriwa wakati wananchi hawana maji, barabara, elimu,umeme etc.
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
18,642
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
18,642 2,000
Zitto,

Tija ya kujenga barabara wewe huioni? Bora ungesema ile midege isiyo na tija au ile SGR isiyo na tija yoyote..
 
O

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2012
Messages
976
Points
500
O

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2012
976 500
CCM wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. Hela zimeelekezwa kwenye chaguzi za marudio na kununua madiwani na wabunge.
 
N

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
7,322
Points
2,000
N

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
7,322 2,000
Mheshimiwa Zitto, ungeanza na sisi hapa Ujiji maana kimsingi hatupaswi kulilia maji zile posho unazogomea Bungeni tumia kutuletea maji BURE toka hapo Tanganyika, utakuwa mbunge wetu milele.
 
L

lebabu11

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2010
Messages
1,939
Points
2,000
L

lebabu11

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2010
1,939 2,000
Utawala wa CCM umelaaniwa.

Wewe angalia maeneo ya Temeke, Mbagala, Mkuranga kuna shida kubwa ya maji lakini toka Mbagala hadi mto Rufiji ni kama kilometers 100 tu, lakini serkali za CCM zimeshindwa kuvuta maji toka mto rufiji kuja mkuranga, Mbagala na Temeke.

Watu maeneo hayo wanakunywa maji ya visima vya mavi, lakini mamilioni ya lita za maji ya mto Rufiji yanamiminikia baharini kila siku.

Bomba la gesi limeweza kutoka Mtwara hadi Dar wanashindwaje kuchukua maji Rufiji kuleta Dar?
Kujenga bomba la maji sambamba na lile la gesi kwa wakati mmoja na kutumia mkandarasi huyo huyo kungepunguza gharama sana.

Tatizo kubwa serikalini wanapanga jambo moja moja na huchukua muda mrefu kutekeleza, pengine hata technology hubadilika kabla ya utekelezaji.
 
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
1,138
Points
2,000
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
1,138 2,000
Mh. Zitto, kama ulivyo hitimisha kwa swali zuri. Tatizo la hii nchi ni priority!! (vipaumbele!), katika suala la maji hii nchi tumelaliwa kuwa na vyanzo vingi lakini ni kama hatuna macho.

Mfano, Mji wa dodoma na wilaya zake zingeweza kupatiwa maji kwa kujenga mabwawa badala ya kufikiria kusafirisha maji kutoka ziwa victoria. Tuna hazina kubwa ya maji ya chini ya ardhi! Lakini hayatumiki ipasavyo. Mimi nakuunga mkono kwamba tukiboresha huduma za upatikanaji wa maji hasa vijijini tutajikwamua kama nchi kutoka wenye umaskini japo kwa kiasi fulani.
Ni vyema unapotoa hoja uwe unaweka tarakimu.

Mfano. Hiyo akiba kubwa ya maji chini ya ardhi ni kiasi gani na ipo maeneo yapi? Na je yana ubora upi? Umewahi kuyatumia maji ya visima maeneo ya Dar. Dodoma na Manyara? Ubora wake ukoje?

Je. Dodoma wajenge mabwawa eneo gani yaani kwenye mto upi na bwawa litakuwa na uwezo wa kutoa maji kiasi gani?

Hasara ya kutoa maji ziwa victoria badala ya kujenga mabwawa kwa ajili ya mji wa dodoma ni ipi?
 
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
1,138
Points
2,000
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
1,138 2,000
Everything is a trap in this country.
Lack of water is a trap....lack of electricity is a trap....poor roads is a trap....poor healthcare is a trap.....don't even mention the education system!
All one vicious cycle designed to keep us perpetually deprived
Kwahiyo ni sahihi kuanza kuondoa mtego wa barabara kabla ya hiyo mitego mingine ikiwemo maji elimu umeme nk.
 
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
1,138
Points
2,000
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
1,138 2,000
Huwa nashangaa sana Tanga jiji kupata maji toka Muheza mto Zigi,cha ajabu pale Muheza maji yanakotoka kuna shida ya maji ni balaa,nadhani tumekosa vipaumbele kama nchi.
Hili ni tatizo la kimfumo. Kwamba katika kugawa maji kunakuwa na mamlaka za mijini ambako maji yanauzika, na mamlaka za vijijini ambako maji hayana bei.

Kama mradi wa kupeleka maji Tanga mjini ungezingatia maeneo yote ya jirani kusingeanzishwa mradi mwingine wa kupeleka maji muheza.

Mhe. Zito mweleze waziri wa maji aache kuwa na discrete projects kwa kila eneo. Nchi hii ni kubwa inahitaji miradi mikubwa ili kusambaza maji kila mahala kwa gharama nafuu.

Mfani ni mitadi kama ya kuleta maji jijini Dar iliyozingatia miji ya Kibaha na Bagamoyo. Na miradi ya kitaifa kama ule wa mugango au wa wang'ing'ombe. Mambo ya vidima kila kijiji ni siasa.
 
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Messages
1,271
Points
1,250
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2012
1,271 1,250
Serikali yetu vipaumbele vyake having mantiki na inataka ionekane kuwa INA uwezo wakati wananchi ndio tunaumia. Mfano kila siku inajisifu kununua bombardier wakati hatuna Maji. Bombardier moja ingeweza kuwekeza miradi zaid ya 1000 ya maji
 
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Messages
1,271
Points
1,250
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2012
1,271 1,250
Tija ya kujenga barabara wewe huioni? Bora ungesema ile midege isiyo na tija au ile SGR isiyo na tija yoyote..
Barabara zina tija ila sio kutumia million 80 kujenga barabara ya Morocco to Mwenge, eneo hilo tayali lina barabara nzuri
 
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
1,138
Points
2,000
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
1,138 2,000
gfsonwin,

Pole kwa kuchoka.

Sera ya maji ya mwaka 2002 imeainisha vipaumbele vya kugawa maji. Kwanza ni maji kwa ajili ya binadamu yaani kunywa kuoga msalani kupikia nk. Pili ni maji kwa ajili ya MAZINGIRA na mwisho ni MATUMIZI MENGINEYO yaani matumizi ya kiuchumi.

Hapo kwenye matumizi mengineyo ni kwamba wadau wanatakiwa wakae pamoja wagawane maji yaliyobaki baada ya maji ya binadamu na mazingira kutengwa pembeni kutoka kwenye chanzo husika.

Bodi za maji za mabonde ndizo zenye jukumu la kuyagawa maji hayo na kila mtumiaji anatakiwa awe na KIBALI CHA KUTUMIA MAJI.
 
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
1,138
Points
2,000
E

Eudorite

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
1,138 2,000
Tunashindwaje kuchimba visima kila ward ikiwa tuna pesa za kununulia Vichwa vya treni visivyokuwa na mwenyewe?
Siyo kila ward ina maji chini ya ardhi.
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
18,642
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
18,642 2,000
Barabara zina tija ila sio kutumia million 80 kujenga barabara ya Morocco to Mwenge, eneo hilo tayali lina barabara nzuri
Hujawahi kukutana na msongamano wa pale wewe, yaan unaweza kusema magari yote Tanzania yapo hicho kipande, halafu haikuwa milioni 80, ilikuwa bilioni 2 nadhani.., na japo barabara zilikuwa nzuri ila zilikuwa nyembamba hivyo wakaona wapanue..
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
18,642
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
18,642 2,000
SGR ina tija kuliko barabara
TAZARA ilikuaje kwani? Wafanyabiashara wanaona tija kutumia barabara kuliko reli, nyinyi mnalazimisha na hilo li-SGR, unajua ni kwanini malori yanafurika Zambia highway ilihali TAZARA ipo?
 
M

mtoto wa mjini

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2010
Messages
1,758
Points
2,000
M

mtoto wa mjini

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2010
1,758 2,000
Watu vijijini wafundishwe kuvuna maji ya mvua
 
Buswelu

Buswelu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2007
Messages
2,008
Points
1,225
Buswelu

Buswelu

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2007
2,008 1,225
chambimagaka,

Wale jamaa hata uvute maji toka ziwa victoria, mto kirumi bado watakata mabomba....pale Nyamongo walivutiwa maji toka mgodini usiku wanakata mabomba wanaenda kuuza Kenya. Baadae mwekezaji akaweka water tanks points akawa anapitisha maji asubuhi anajaza kwenye tanks hizo kwa matumizi ya binadamu...ili wana Nyamongo waje wachote bado wale jamaa wakawa wakimaliza kuchota wanaiba koki za maji....wao walikuwa wanataka waachiwe sehemu wakavune dhahabu sio huduma za kijamii.

Pili....Ruzuku anayo toa mwekezaji....ingekuwa inatumika vyema Tarime ingekuwa na maji toka 2008. Matumizi mabaya ya ruzuku ni changamoto....zile hela zingetumika kwanza na vipaumbile kama hivyo tatizo hilo lingekuwa historia kwa sasa na pengine na matatizo mengine mengi yangekuwa historia....tatizo ni culture ya watu wale.

Ila kwa sasa naona mambo yamebadilika baada ya umeme kufika nyamongo....ustaarabu umeanza kuwaingia....na udhibiti mkubwa uliowekwa wa kuchukua mchanga wa dhahabu umefanya vijana kuanza kuwaza njia mbadala ya kupata kipato.

Mwita Mwita.
 

Forum statistics

Threads 1,403,288
Members 531,177
Posts 34,419,811
Top