Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,668
- 11,333
Upeo wa mtu unajulikana kutokana na matendo yake, sasa hapa ni picha tu bila maandishi mtu anakuja juu, lakini tujifunze kitu kwa aina hii ya wabunge.
Wmchome moto kwani yeye ni mchawi?Huyu jamaa mimi simuelewi ukiangalia hiyo picha kwa makini unaona kabisa anachosema si kweli, kama alikuwa na Vincent iweje aonekane anamuangalia Nassari! na anasema Nassari alikuwa anaamlisha vijana wa Chadema wamchome moto, kwa mazingira ya kawaida mtu anayetishiwa kuchomwa moto angekuwa na sura ya kutishika maana usalama wake ungekuwa hatarini lakini tofauti na yeye anavyoonekana kwenye picha akiwa na furaha sana,ina maana alikuwa anafurahia tishio hilo! haya ndio matatizo ya waganga wa kienyeji kuwa wana siasa!mbona sasa hatishii kulishitaki na Tanzania Daima maana nalo lilipandika picha hiyo!
Huyu ela zinamuwasha aende ili na mawakili wapate ulaji.
Kwani kuna kosa gani kuwa jirani na Nassari mbona sijamwelewa ama amesahau nani alikuwepo, labda wamemtisha waliomweka madarakani akaona kuna kuwekwa pembeni. Awe wazi tu!!
Nassari ni mtoto wa mchungaji so kuwa karibu nae mapepo yake yanakosa furaha, amani na utulivu.
Majimarefu Asema Picha Imetengenezwa
Amemaliza maongezi na wakili maarufu jijini kuiburuza CHADEMA na MWANANCHI Mahakamani Jumatatu kwa kumchafulia jina na heshima yake ndani ya chama na jamii kwa ujumla
"Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa jana ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.Vilevile ukurasa wa kwanza gazeti la Tanzania Daima.
Maji marefu wewe ni msomi uliyebobea mpaka kufikia hadhi ya kuwa profesa, wanafunzi wako wa chuo kikuu wakiona hii habari hawataipenda kabisa.
mkuu jimbo analoliongoza linahitaji nguvu ya ziada, wapiga kura wake asilimia kubwa ni wajinga wajinga kama yeye.Naona kajaribu kutumia matunguli "kuiadhibu" CHADEMA akashindwa sasa mbio mahakamani........ngoja na yeye tumpelekee mahakama ya kura 2015
mkuu jimbo analoliongoza linahitaji nguvu ya ziada, wapiga kura wake asilimia kubwa ni wajinga wajinga kama yeye.