Majeshi ni kwa ajili ya form 4 failure tu

Majeshi ni kwa ajili ya form 4 failure tu

Ukisikia akili mtopea ndiyo hii. Kwamba una experience ya miaka 10, labda hilo jeshi ni la nyumbani kwenu. Kwa hiyo madaktari walipogoma Muhimbili ni form 4 waliofundishwa na mshua wako walioenda kuthibiti hali? Au walipogoma uwanja wa ndege ni hao ndugu zako walioenda? Je, waliojenga daraja la msata lilipobomoka? Haya, umechunguza ni idadi gani ya wanajeshi, polisi, magereza, usalama wa taifa, n.k walioko ktk kila chuo cha elimu ya juu nchini? Nenda kwa huyo sangoma akakuoshe tena!

Uliza pale muhimbili kipindi cha mgomo walifanya nini? Propaganda zitawapoteza. Ulimwengu wa Leo madaraja ya chuma na mbao yanafundishwa chuo gani? Njoo huku kwetu mufindi hayo madaraja tunayajenga kuvushia magogo yetu hatujioni kama wasomi
 
Nyie bishaneni tu, mi cha 4 changu msharaha mkubwa, ninanyumba,gari na watoto wangu nasomesha shule nzuri na nimeridhika na maisha
 
huyo jamaa sio mwanajeshi wala hakupitia jeshi lolote bali anajikanyagakanyaga hapa kwa maneno ya kusikia vijiweni na kama ukitimba utatokea kwa askari yoyote mwenye degree ni ujinga wake tu wa kushindwa kufuata sheria na kanuni mbalimbali za majeshi pia graduate huwezi kukaa muda mrefu jeshini bila kuwa afisa.

hivyo mtoa mada anapiga fix tu kama vipi aje tena kwa mahojiano hapa.

Tupe tofauti yenye mantiki kati ya mwanajeshi na afisa na mchango wa kila mmoja ndani na nje ya jeshi.
 
So ukiritimba gan unaozungumziwa.Maana huku jeshin wasomi ndio hao wanapigiwa salute,wanalipwa mishahara mizuri,wanavyeo

Salute na mishahara vina msaada gani kwa nchi? Ningependa nitambuliwe kwa mchango wangu ktk nchi na sio salute. Salute inamaana sana kwa wajinga
 
Uliza pale muhimbili kipindi cha mgomo walifanya nini? Propaganda zitawapoteza. Ulimwengu wa Leo madaraja ya chuma na mbao yanafundishwa chuo gani? Njoo huku kwetu mufindi hayo madaraja tunayajenga kuvushia magogo yetu hatujioni kama wasomi

Any way uko hapa kujifurahisha, siye tuko hapa kupata na kutoa elimu ya jamii.
 
Acha ujinga ww mawazo mgando hayo ivi unajua kama kuna watu hawalali ili we uishi kwa amani na usalama waki kila.siku afu eti hawana elimu....na uende ata toi boya kweli ww

Wasomi wa kweli wanastahili kulala. Na asipolala kunajambo la kukumbukwa analigundua. Kwa anayejitambua hawezi kufanya kazi ya jeshi. Jeshi special kwa wavivu wa kufikiri.
 
Wasomi wa kweli wanastahili kulala. Na asipolala kunajambo la kukumbukwa analigundua. Kwa anayejitambua hawezi kufanya kazi ya jeshi. Jeshi special kwa wavivu wa kufikiri.

kulala ama kutokulala kwake wewe inakuhusu nini? mbona huyo girlfriend ulinaye kuna baadhi ya ndugu na rafiki zako wanasema ulikua na uvivu wa kufikiri ndio maana ukaishia kumpata huyo, wanaenda mbali nakusema hukuona mzuri zaidi ya huyo? Wakati wewe unaona umefanya best choice kwao wanaona ulikua na uvivu wa kufikiri ndio maana ukaishia kumpata huyo uliyenae. Hapa lazima utabisha tu. Nachotaka kusema ni kwamba hakuna perfection at all kwa binadamu wote yani haitokuja kutokea watu wote wakaliona jambo fulani kuwa ni sawa muda wote lazima watatoa kasoro tu ndio maana wakati wewe unaona ni sawa kua na huyo girlfriend ulinaye kuna watu wanakudhihaki huku nyuma tena bila sababu za msingi za kukuona hufai kua na girlfriend ulinaye. HUU TUNAUITA NI UBINADAMU. Ivyoivyo kwa majeshi wakati wewe unaona si sawa kwa wasomi kutokwenda huko kuna wasomi wenzako tena wenye MASTERS DEGREE wanaona fahari kwenda huko. Sio unakaa hapa unabishabisha wakati kuna watu wanakukosoa hata wewe kwakukuona ulifanya makosa katika kuchagua huyo girfriend ulinaye.
 
Salute na mishahara vina msaada gani kwa nchi? Ningependa nitambuliwe kwa mchango wangu ktk nchi na sio salute. Salute inamaana sana kwa wajinga

wanalinda mipaka ya nchi dhidi ya uvamizi mpaka wewe unapata muda wakutoa fikra zako zenye akili iliyotukuka hapa JF huo ndio mchango wao mkubwa kwa nchi yetu. KULE KUNA UTII NA NIDHAMU YA HALI YA JUU. Nazani ofisini kwenu hivi vitu vipo kwa hiyo na NYINYI NI WAJINGA? NA JE HESHIMA ZENU NI UJINGA KWA MBOSI WENU? ndio maana unafanya kazi kwa maagizo ya bosi wako hujipangii kazi ya kufanya ukifika ofisini . Kama ungekua huwaheshimu usingefika hapo ulipofika sa iv. Jeshini saluti ni heshima kwa watu waliokuzidi cheo NI SAWASAWA NA WEWE UNAVYOWAHESHMU MABOSI WAKO hakuna tofauti. KAMA HESHIMA IMEKUA IMEKUA UJINGA SIKU KWA MABOSI BASI HAYA NI MAENDELEO YA HALI YA JUU SANA, ANYWAY THANKS ULIMWENGU WA DIGITALI KUFANYA HESHIMA KWA WATU WALIOTUZIDI CHEO KUA UJINGA SIKU HIZI MAOFISINI.
 
Mkuu sina elimu kubwa sana ila elimu yangu ya kidato cha nne inatosha kabisa kuelewa maana ya division of labour na mwalimu wangu wa history form 2 alinifundisha kuwa division of labour inaangalia umri(age) jinsi(sex) na ujuzi au ubobezi(specialization) je unadhani majeshi yetu hasa Polisi na magereza yanawatumia wasomi kulingana na ujuzi waliosomea.

Una elimu kubwa umeshindwa tofautisha division of labour and specialisation, ungesoma economics form 5&6 ndo ungejua kuwa hapa umehara. Comeback to the topic jeshini kuna watu wenye elimu zao za maana na cio ww ya kwako ya magumashi 1stly u have downstairs.
 
Salute na mishahara vina msaada gani kwa nchi? Ningependa nitambuliwe kwa mchango wangu ktk nchi na sio salute. Salute inamaana sana kwa wajinga

Sasa we msomi unataka ufanyiwe nini na jeshi ili uone umethaminiwa? Inaelekea unastress za kutoajiriwa na ndiyo maana husomeki unataka nini? BASI KAMA WEWE MSOMI GUNDUA KITU UHESHIMIKE UNAJIITA MSOMI KWA ELIMU ZA KIBONGO AMBAZO MWISHO WAKE KWENYE SIASA ZA KUCHAFUANA.
 
Una elimu kubwa umeshindwa tofautisha division of labour and specialisation, ungesoma economics form 5&6 ndo ungejua kuwa hapa umehara. Comeback to the topic jeshini kuna watu wenye elimu zao za maana na cio ww ya kwako ya magumashi 1stly u have downstairs.

Mkuu mimi nimesema sina elimu kubwa sana nimeishia form 4 nikashindwa kuendelea na masomo nilichokiandika nime refer notes za mwalimu wangu wa history form two na sio kila mtu ajue kile unachokijua wewe.
 
Kwa experience yangu ya kufanya kazi katika jeshi moja hapa nchi kwa miaka 10 nimegundua kuwa kazi za majeshi(jw,polisi,magereza) zinawafaa watu wenye elimu ndogo tena form 4 failure maana kuna kila aina ya ukiritimba na urasimu ambao msomi hawezi kuvumilia na kama akivumilia ataishia kujilaumu kwa uamuzi wake.

Hivi na wewe ni MSOMI aiseeee hv hzo degree zenu za NYUKI zinawasumbia hv bongo kuna WASOMI
 
Kiasi kikubwa kuna ukweli ktk madai ya mleta mada. Siku zote jeshini wanatakiwa wasomi wachache na wasiosoma wengi maana kazi za jeshi nyingi ni manual. Ni kazi na mazingira ambayo yanahitaji watu wachache wenye IQ kubwa kuwaongoza wengi wenye IQ ndogo. Ndio maana huwi taught bali trained. Tukubali tukatae majeshini division alizo taja mleta mada ni ukweli na ushahidi ulio wazi japo wasomi kweli wapo kwa uwiano mdogo.
 
Inaelekea unastress za kutoajiriwa.

Wasiojielewa tu ndio huona fahari kuajiriwa, nilishachana na huo mtazamo.

Wanajeshi wengi wanasingizia kufurahia kazi yao but in real sense hawapo hivyo.
 
hahaaaa!!! kuna kaukweli hapa,

nina ma friend mwanajeshi, anayoyaongeleaga kwakweli mmmh!!

mtoa mada mm nimekuelewa japo mie naona km watu wamepanik na kugoma kuelewa lile la msingi uliloliongelea.

ATOTO, Nakubaliana na ww, wachangiaji wengi hawajamsoma, wanafikiri ameyaponda majeshi yetu kuwa hayana wasomi. Anachokiongelea mtoa mada ni kwamba unaweza kuwa na elimu nzuri tu, Diploma, degree, masters etc lkn kupanda cheo kulingana na elimu yako kuna ukiritimba mkubwa sana hasa kama huna god father na hujui kujipendekeza kwa maafande.
 
Back
Top Bottom