Majeshi ni kwa ajili ya form 4 failure tu

Majeshi ni kwa ajili ya form 4 failure tu

Naunga mkono mada, jwtz ndo wasomi halali lakini wengine hakuna elimu Kwa wengi, wamefoji vyeti vya ndugu zao Kwa hilo wasikatae.
 
Huyu mtoa post hajatumia ubongo wake kwa ufasaha na ndiyo maana ameshindwa kufikiri hadi akafikia kudharau kazi za watu.Kama wao ni form four failure kinakuuma nini? Isitoshe hujafanya research kwenye majeshi yetu wapo wasomi wengi na wanatenda kazi zao vizuri.Siku zote elewa wengi Wa waTz tunafanya kazi vide profession
 
Kwa experience yangu ya kufanya kazi katika jeshi moja hapa nchi kwa miaka 10 nimegundua kuwa kazi za majeshi(jw,polisi,magereza) zinawafaa watu wenye elimu ndogo tena form 4 failure maana kuna kila aina ya ukiritimba na urasimu ambao msomi hawezi kuvumilia na kama akivumilia ataishia kujilaumu kwa uamuzi wake.

Jeshi ni kazi ya kitume maana imeandikwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Majeshi!
Wewe utakuwa Mwanasheria tu maana ndo wanaongoza kuacha kazi!
 
Naunga mkono mada, jwtz ndo wasomi halali lakini wengine hakuna elimu Kwa wengi, wamefoji vyeti vya ndugu zao Kwa hilo wasikatae.

huna unalolijua bora ukae kimya mkuu.. jwtz ndo inachukua darasa la saba mpaka leo + vyeti vya ku forge.. sasa sijui elimu unayoizungumzia ni ipi???
 
huna unalolijua bora ukae kimya mkuu.. jwtz ndo inachukua darasa la saba mpaka leo + vyeti vya ku forge.. sasa sijui elimu unayoizungumzia ni ipi???

Ila Jeshi la Polisi wamezidi kuzoa zoa vilaza...

Ndio maana adabu ya jeshi hilo imepungua mno...

Jeshi la wananchi walau miaka ya karibuni wameanza kuwa makini na ajira zao...
 
Kwa kukusaidia mtoa mada kama kweli umesoma utakuwa unajua kitu kinaitwa division of labour, hata ktk taasisi kubwa za kielimu mfano UDSM sio wafanyakazi wa pale wooote ni maprofesa NO. Katika majeshi yetu pia sio wooote hawana elimu ya kutosha kama unavyodhani (Hapa nazungumzia elimu iliyopo kwenye mfumo rasmi yaani msingi, sec na vyuo) wanayo kubwa tuu!!!! In adition watu hawa hupewa elimu ya kijeshi ambayo haitolewi ktk tasis nyingine na katika mgawanyo wa majukumu hayo kila mtu anafit sehemu yake na ndio maana wewe na wenzio msio na shukrani mnalala na kuendesha maisha yenu bila wasiwasi.
 
Ila Jeshi la Polisi wamezidi kuzoa zoa vilaza...

Ndio maana adabu ya jeshi hilo imepungua mno...

Jeshi la wananchi walau miaka ya karibuni wameanza kuwa makini na ajira zao...

Jeshi la Polisi ndo jeshi lenye wasomi wengi kuliko majeshi yote hapa nchini na ndio maana nidhamu haipo sababu kila mtu anajiona yuko juu. kijana kaajiriwa na ka degree chake chenye GPA mbaya lakini anadharau kazi akitumwa anajiona yeye msomi hivyo hastahili kufanya kazi hiyo huku akisahau wakati wa usaili alivyosugua gaga kuitafufa. mpaka leo jeshi la wananchi wa Tanzania ndo jeshi lenye askari wenye nidhamu ya hali ya juu sababu wajiriwa wake wengi ni darasa la saba.. over!!!
 
Wasomi wanataka waishi jeshini kama wako wako ofisi za BOT..Wakati jeshini ni sehemu ya ukakamavu na kugangamala....na sio lelemama....
 
msomi ni mtu wa aina gani??? we ulifanyia jeshi la nchi gani hilo??? nakushauri research yako uanze upya kwa kufanya hivi... kila majeshi yanapotangaza nafasi za ajira, basi nenda siku ya interview ukawahoji watahiniwa wanaowania hizo nafasi wana shule gani then utarudi na majibu mkuu..
Huyu nahisi atakuwa kwenye lile jeshi letu hapa zenji linalo fanana na jkt- bara ila tofauti huku vijana watiifu wa "sisiem" hukusanywa kutoka maskani na kupelekwa kwenye jeshi hilo.jeshi ambalo wakifanya road work marching/jogging wengi wao hukatiza chochoro na kusubiri troop yao kwa mbele kuelekea kambini!
 
Kwani ww una elimu gani??, ukute una ka degree kamoja tu, wakati wenzako wana masters+doctorate+cpA(T), na wanakula maisha jeshini, ww kwanza hujawahi ht fanyia kazi kwny jeshi lolote hapa bonge, utawadanganya wajinga wajinga km ww.
Wewe! kijijini kwao kufika form six ni elimu kubwa sana wewe unamtajia degree? unadhani mwenye degree hata ya ovyoovyo tu anaweza kwa miaka kumi ya experience na uchunguzi akaja na hitimisho la kipuuzi kama hilo?
 
Upo sahihi mkuu! Japo wengi hawakukuelewa. Uzowefu wa 10years unaongelea unachokijuwa. Majibu ya wachangiaji hayaendani na mada yako.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
Sasa wewe kwa ufahamu wako unadhani mleta hoja kaongelea chochote au katupa hitimisho la uchunguzi na uzoefu wake tu? Na tutakuwa wapuuzi tukikubaliana nae bila ya yeye kudadavua kwa mifano ikiwezekana madhira yanayowakumba wasomi kama mleta hoja jeshini.
Kutokueleweka ni tatizo la mleta hoja kwa kushindwa kuitambulisha hoja yake ,hatupigi ramli hapa ,leta hoja inayojitosheleza katika suali pana kama hili!eti msomi halafu unaleta habari kama uko kwenye kijiwe zembe!
 
Wasomi wanataka waishi jeshini kama wako wako ofisi za BOT..Wakati jeshini ni sehemu ya ukakamavu na kugangamala....na sio lelemama....

uko sawa kabisa mtani.. ndo maana hawahitajiki wengi jeshini maana wanaharibu nidhamu iliyokuwepo
 
Na wasomi wengi wanakimbilia jeshini baada ya mitego yote kubuma kitaa na kusugua benchi sana...
 
Na wasomi wengi wanakimbilia jeshini baada ya mitego yote kubuma kitaa na kusugua benchi sana...

unatumia kinywaji gani mkuu??? mwezi Dec nilikua Dar.. ungewaona wakiwa na route za chuo cha Polisi kwenye usaili ungewahurumia ila subir watoke chuoni ndo utawajua njema...
 
Sasa wewe kwa ufahamu wako unadhani mleta hoja kaongelea chochote au katupa hitimisho la uchunguzi na uzoefu wake tu? Na tutakuwa wapuuzi tukikubaliana nae bila ya yeye kudadavua kwa mifano ikiwezekana madhira yanayowakumba wasomi kama mleta hoja jeshini.
Kutokueleweka ni tatizo la mleta hoja kwa kushindwa kuitambulisha hoja yake ,hatupigi ramli hapa ,leta hoja inayojitosheleza katika suali pana kama hili!eti msomi halafu unaleta habari kama uko kwenye kijiwe zembe!

Wewe ndo hujaelewa unajua maana ya ukritimba na urasimu.
 
Wewe ndo hujaelewa unajua maana ya ukritimba na urasimu.
Usituletee misamiati hapa,sema ukiritimba upi na urasimu upi ulioko huko mpaka ukahitimisha vile! na ni kweli sijakuelewa chochote ndio maana sikubaliani nawe na hufanyi juhudi zozote ili watu tukuelewa msingi wa madai yako zaidi ya hints za "usomi" form 4 failures"ukiritimba"na "Urasimu"ukitaraji wasomaji wako tujazie nyama katika hili ilhali wewe umeshafanya uchunguzi na una first hand experience, sasa unaona ugumu gani kufunguka yaliyopo huko ili sisi raia wakawaida tukuelewe?
 
Kama huelewi maana ya maneno hayo kaa kimya au tafuta kamusi.
 
Kama huelewi maana ya maneno hayo kaa kimya au tafuta kamusi.
Mkuu acha maarifa mafupi kwa kujifanya mjuzi wa lugha,hebu nikuulize kwa kipimo cha akili yako -maana tukijadiliana kama watu wazima hatuelewani.
Mimi ni raia wa kawaida tu,nahisi jeshini asilimia 99 wanafanya au kutimiza majukumu yao kwa kufuata amri si utashi wao,sasa utakapo amriwa kufanya kazi fulani ni ukiritimba gani au urasimu gani unakuzuia kutimiza wajibu wako?
 
Back
Top Bottom