"MAJERUHI"... Based on a true story...

kuna mtu kasema kuwa ati nimeandika mambo mengine kwa undani sana hivyo ipelekwe kwa watu wazima.... kweli?
 
Wife anapenda sana kusoma hadith. Hiki kitabu kikiwa tayari ntamnunulia, then ntampatia siku nakwenda long trip.
Naamini kitampa kampani sana.

Nimekukubali MM, uko very universal brother. kitakuwa store by when?
 
Wife anapenda sana kusoma hadith. Hiki kitabu kikiwa tayari ntamnunulia, then ntampatia siku nakwenda long trip.
Naamini kitampa kampani sana.

Nimekukubali MM, uko very universal brother. kitakuwa store by when?

Inshallah kitaweza kupatikana kwenye mitandao na tukipata publisher wa uhakika nataka kiwe tyari kabla ya holidays! Kinaweza kuwa zawadi nzuri kwa marafiki na familia!
 
iko poa ila attachment umerudia ulichoandika,ungeweka hata sura ya 11

Watu wengine walikuwa hawawezi kudownload attachment ndio maana ya kuweka stori hapo juu... na wengine hawana muda sana kuwa online so wanadonload tu attachment
 
SURA YA 11.. (INTRO)

Siku ya Alhamisi Alex hakutokea kazini kabisa. Ijumaa hakutokea vile vile. Erica hakutaka hakuulizia wala kufanya nini. Alijaribu kupiga simu mara mbili kumjulia hali lakini simu ilikuwa imezimwa; akajua kweli Alex amemkasirikia na kwa kweli hakumlaumu. Katika hisia zake Alex alikuwa tayari ni historia na alikuwa anaangalia maisha yake ya mbeleni. Siku ya Jumamosi ilipofika majira ya saa kumi za jioni alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wa benki na kuulizwa kama amepata habari za Alex. Moyo wake ulimshtuka na kumlipuka.

“Habari gani?” aliuliza katika hali ya shaka kuu. Alikuwa ameingia tu nyumbani kutoka kufanya manunuzi Kariakoo. “Hujasikia?”alikuwa ni mmojawapo wa marafiki wa Alex pale ofisini aliyeitwa Jovian akimuuliza. “Kusikia nini Jovian?” “Dah! Sijui nianzie wapi!” “Sema basi unataka nizimie? What happened to Alex?” aliuliza kwa hamasa akiombea katika mioyo yake yote yaani labda iwe ni ajali na amepelekwa Muhimbili au kakoswakoswa na kitu kibaya. Masikio yake hayakuwa tayari kusikia sentensi iliyofuatia....
 
Back
Top Bottom