"MAJERUHI"... Based on a true story... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"MAJERUHI"... Based on a true story...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 28, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kutokana na kisa cha kweli

  SURA YA 10
  Kutoka mwanzo....

  Kutwa nzima moyo wa Erica ulikuwa ukimwenda mbio na kumshtuka shtuka. Alikuwa na wasiwasi wa aina yake lakini ulikuwa ni wasiwasi ulioendana na kukosa subira. Alikuwa akijua kuwa siku aliyokuwa ameisubiria na kuipanga kichwani mara nyingi ilikuwa imefika. Pale kazini alionekana mwenye mawazo sana na alikuwa akijishughulisha kiasi kwamba wafanyakazi wengine walijua haikuwa siku ya kwenda kumuuliza uliza maswali. Alifanya kazi sana na hata chakula cha mchana aliagiza tu chips zikaletwa pale. Ilikuwa ni karibu miezi miwili tangu aanze penzi lake la wizi na Imma huku akiendelea na penzi jingine na Alex. Alijua wakati ulikuwa umefika kufikisha mahusiano hayo kwenye ukomo wake na siku hiyo ilikuwa ndio siku yenyewe.
  Alipofika nyumbani baada ya kazi aliingia bafuni kujimwagia maji na alipotoka huko alivaa gauni jepesi fupi jekundu inayong'ara lililombana mwili kama kumng'ang'ania asikimbe. Miguu yake iliyonawari vyema ilitulia kwenye viatu vidogo vya mchuchumio. Kifua chake kilibanwa vizuri na gauni lakini kikifichua matiti yake na kuachilia yaonekane kwa juu katika hali ya kudokeza tu uzuri wake. Alikuwa ameziachilia nywele zake ambazo zilikuwa zimewekwa relaxer mabegani mwake. Moyo bado ulikuwa unamdunda na viganja vyake vilikuwa vikishikwa na unyevu mara kwa mara. Alikuwa anamsubiria Imma kufika pale nyumbani.

  Kwenye majira ya saa mbili kasorobo Imma alimpigia simu. "Hey baby nimefika!" Imma alisema mara aliposikia sauti ya Erica upande wa pili wa simu. "Karibu" alielekea mlangoni. Alipopanda ghorofani Imma aliwaza ni jinsi gani amejaribu kujinasua kutoka katika mikono ya Erica na kushindwa. Upande mmoja nafsi yake ilimsuta na kumkemea lakini hisia zake na mwili wake ulimpigia kelele kuitikia. Alijitahidi kujizuia kuondoka ofisini na kuelekeaa kwa Erica lakini kwa kadiri alivyokuwa anajiambia kuwa akomeshe uhusiano huo ndio kumbukumbu kama taswira za kwenye luninga zilicheza kichwani mwake na kuamsha ashki hadi kwenye vidole. Aliendelea kujipa moyo kuwa kwa kadiri ya kwamba mke wake - mama mapacha wake - hajui basi hakukuwa na ubaya sana. Ila alikuwa na uhakika siku akija kujua mambo yangeweza kuwa makubwa sana. Kale kashetani kwenye bega lakekaliendelea kumnong'oneza ‘asilolijua halimuumizi'. Alipanda ngazi huku moyo ukimdunda.


  Alipofika mlangoni alibonyeza kitufye cha kengele kilichokuwa upande wa kushoto wa mlango na sekunde chache tu baadaye komeo la juu la mlango lilijiachia na kitasa kikazungushwa chini, mlango ukaachia. Erica alikuwa amesimama mbele yake akiwa katika utufuku wake wa kike na vazi lakelile jekundu likifichua uzuri wake wa asili. Hakuwa na vipodozi vingi na hivyo vidogo alivyokuwa navyo alivitumia vizuri sana na hivyo kuyaangaza macho yake zaidi na mashavu yake kuonekana kama ya picha ya Mona Lisa.


  "Mbona unataka kunipa ugonjwa wa moyo Erica" Imma alisema huku mguu wake wa kushoto ukivuka kizingiti. "Hahahah kwa lipi tena acha vurugu, mambo dear" "Pouwa, umependeza sugar pie"


  "Asante" Sauti yake ililegezwa kidogo. Macho ya Imma yalikuwa yametulia kifuani kwa Erica na hakuyaamini macho yake kwani gauni alilovaa Erica lilifichua kuwa chini yake hakukuwa na sidiria kwani chuchu za Erica zilizikuwa zimechorwa vyema na kuumbika kama za sanamu wa kuchongwa juu ya gauni lile jekundu. Erica hakujali ila moyoni alijisikia raha tu kuwa kijana huyo kwa kweli alikuwa amenasa. Alimkaribisha ndani hadi sebuleni upande wa kulia wa pango lakelile.
  "Dear jisikie uko kwako ngoja niandae meza"


  "Asante" pembeni ya mlango mkubwa wa sebule kulikuwa na sehemu ya kuvulia viatu na Imma alifanya alilokwisha zoea kwa kuvua viatu na kubakia na soksi zake za rangi nyeusi zikiwa na michirizi ya rangi nyekundu, nyeupe na bluu kwenye shingo zake. Aliweka funguo ya gari lakekwenye jaketi na kulivua jaketi hilo kisha akalitundika kwenye kabati dogo la makoti upande wa kushoto wa sebule. Aliketi kwenye kochi kubwa la rangi ya maziwa ambalo liliangalia luninga kubwa ya nchi 52 ambayo wakati ule ilikuwa inaonesha muziki wa Afrika. Kabla hajatulia Erica alirudi kutoka jikoni. Alikuwa amejifunga kanga kiunoni bila kuibana ni kama kuishikiza tu.


  "Unataka kinywaji chochote?""Maji tu nina kiu ile mbaya"


  "Ok" Erica alielekea jikoni kwenda kumchukulia glasi ya maji. Alivyogeuka nyuma ilikuwa ni kama kwa makusudi tu kwani Imma hakuweza kuyaondoa macho yake kumwangalia Erica mgongoni. Kuanzia shingoni hadi miguuni lakini macho yake yalijikuta yanaangalia kwa kukazia kiuno chake. Alijua jambo jingine kuwa licha ya kuwa Erica hakuwa amevaa sidiria ushahidi wote wa kimazingira ulionesha kuwa hakuwa na kitu kingine chochote chini ya gauni lile.


  "Usihangaike ngoja nije kuchukua mwenyewe" alijikuta anasema na kuinuka kutoka kwenye kochi na kuelekea jikoni akimfuata Erica nyuma. Erica aliuma midomo yake akitamani kucheka kidogo lakini alijizuia.


  "duh harufu tamu hii" "Hahaha umeanza, umefuata maji chukua kwenye friji" Erica alijibi kiutani."Kama ingekuwa ni maji tu mbona ningeendelea kukaa sebuleni""Ala! kumbe umefuata nini kingine jikoni kusaidia kupika? hehehehe" alicheka Erica."Nimekufuata wewe nilikuwa na swali""Ehe uliza""Nilikuwa nashangaa" akaanza lakini asijue jinsi ya kuendelea."Unashangaa nini Imma?""Forget it wacha nijuchukilie maji" aliamua kuahirisha swali lake. "Ha! haya wee!" Erica alisema bila kutaka kumsukumiza aulize."Miye ntauliza bwana anyway!" Wote wawili waliangua kicheko.


  "Haya mara ya mwisho!" Erica alisema akiwa amesimama mbele ya Imma pembeni ya jiko na meza ya kukatia vitu pale jikoni. Jiko la Erica halikuwa kubwa sana na liliendana hasa na ukubwa pango lakelote. Lilikuwa jiko dogo lakini la kisasa. Kuta zake mbili za upande wa kulia na kushoto zilikuwa zimepakwa rangi ya mchanga uliofifia na ukuta wa katikati ulikuwa ni wa rangi ya nyeupe. Mbele ya ukuta huo wa katikati ndio miundombinu ya jikoni ilikuwa imepangwa vizuri. Kulikuwa na friji kubwa la rangi nyeusi upande wa kushoto, likifuatia chini yake jiko la gesi la rangi nyeusi vile vile, sinki la kuoshea vyombo lilifuatia na upande wa kulia vyote vikiwa vimelingana kulikuwa na mashine ya kuoshea vyombo na kabati dogo la vyombo. Vyote vikiwa vya rangi nyeusi vile vile. Kabati la vyombo na mashine ya kuoshea vyombo vilikuwa vimeunganishwa juu na ubao mnene wa marumaru uliotengeneza meza hivi ambapo mtu angeweza kuweka vyomo baada ya kuviosha - kama hakutaka kutumia mashine. Juu yake kulikuwa na kabati dogo pamoja na mashine ya umeme ya kupashia moto vyakula.

  Mbele ya vyote hivyo kulikuwa na meza ya mstatili ya rangi nyeusi chini na juu ikiwa ni marumaru nyeupe ikifanana na ile marumaru iliyokuwa juu ya mashine ya vyombo na kabati. Chini yake kulikuwa na milango ya makabati ya kuwekea vyombo mbalimbali. Ukuta wa upande wa kulia ulikuwa na shefu moja iliyoshikizwa vizuri ukutani ndani yake kukiwa na vyombo mbalimbali vya glasi. Vyombo vingine vya bati vilikuwa chini ya meza na vile vya udongo na maglasi mbalimbali vikiwa kwenye kabati kubwa pembeni ya sebule.


  "Nilikuwa nashangaa kama chini ya hilo gauni kuna kitu kingine chochote" alisema bila haya wala woga. Mikono yake ilimsaidia kwani alimvuta Erica aliyekuwa amesimama akikoroga mchuzi wa samaki jikoni wakati akiupasha moto. Mikono ya Imma ilizunguka kiuno cha Erica kwa kutokea nyuma na kumvuta kidogo huku Erica akijitahidi kuushika mwiko vizuri. Erica aliweza kumhisi Imma kuwa alikuwa katika hali gani kwani miili yao ilikuwa imegusana kabisa.  "Hahaha kuna njia moja tu ya kujua!"


  Imma aliteremsha mikono yake chini na kulivuta gauni la Erica kwa kupapasa mapaja yake huku akiileta juu. Ilipofika kiunoni alikuwa na uhakika na dhana aliyokuwa nayo kichwani.


  "Toba baby, ndio maana chakula chako kinakuwa kitamu sana" alimbonyezea busu la shingoni huku akiliachia gauni limfunike tena Erica.


  "Shindwa!" alisema Erica huku akitikisa kiuno chake na kumbamiza Imma kidogo na kumfanya amuachie kidogo. Imma alikuwa amezama kwenye majaribu. Erica alifunika sufuria na kuweka mwiko pembeni na kumgeukia Imma ambaye alikuwa katika kila kipimo taabani. Macho yake yalikuwa yakiita tamaa. Alimsogelea na kujiachilia mikononi mwake naye Imma hakuchelewa kumpokea kwa busu la taratibu lililouvuta kidogo mdomo wa chini wa Erica. Imma alizungusha mikono yake kiunoni mwa Erica na kumvuta karibu huku Erica naye akizungusha mikono yake. Walibusiana kwa dakika chache huku wakigusana kimahaba. Erica alikuwa hoi na Imma alikuwa hoi bin taabani.


  Imma alishindwa kujizuia na kwa nguvu ya ajabu alimnyanyua Erica na kumkalisha kwenye ile meza ya katikati. Alifungua zipu ya Erica mgongoni na kumsaidia kutoa mikono yake. Gauni likaajiachia tu hadi kiunoni na kukiachilia kifua cha Erica wazi. Kidani cha Erica na hereni ndivyo vitu pekee vilibakia mwilini. Erica alifungua zipu ya Imma na kuachanisha mkanda ulioshikilia suruali na vyote vilianguka kwenye sakafu. Wakati Erica anashughulikia kufungua suruali Imma alikuwa anafungua vifungo vya shati lake. Erica alifungua miguu yake na Imma alisimama katikati yake.Midomo yao ilikuwa bado imeshikana mikono yao ikipapasana mgongoni.


  "Tukisi kwanza dear hakuna haraka" Erica alimnong'oneza Imma ambaye aliitikia na kuhakikisha hampi nafasi nyingine ya kuzungumza.  Erica alianza kuhesabu muda ulivyokuwa unapita, raha aliyokuwa anaipata na kuweza kusikia mapigo ya moyo yalivyokuwa yakizidi kuongezeka. Imma alimsahau kabisa mkewe, alisahau kila kanuni aliyojiwekea katika maisha na kwa dakika chache zile alikuwa katika pepo ya mahaba ya aina yake. Kabla ya Erica hakuwahi kukutana na mwanamke mwenye kutoa ushirikiano wa mapenzi namna ile, kwa namna ile, na bila unyimi wa aina yoyote. Alikuwa ni binti aliyejua kutoa kama alivyojua kupokea. Alifikiria ni vipi atamuacha mke wake ili awe na Erica milele. Raha ilimpanda hadi kwenye ncha za nywele zake.  NUSU saa kabla yake Alex anawasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Afrika ya Kusini mbako alikuwa ameenda kwenye kongamano la kikazi jijini Durban. Alikuwa Afrika ya Kusini kwa wiki moja ambapo pamoja na kufanya utalii kidogo alikuwa na muda wa kufikiria sana mahusiano yake na Erica. Alijua kwa kweli ni wakati wa kutoa pendekezo la ndoa. Mapema siku hiyo alimuambia Erica jinsi alivyokuwa amemkosa sana na alivyotamani kufika nyumbani kumweka machoni pake. Kwa kweli mawazo yake yote yalikuwa kwa Erica. Alinunua zawadi nyingi tu kama hereni, bangili na na nguo kwa ajili ya mpenzi wake. Alex alikuwa ameshaamua kuutuliza moyo wake na kwa hakika alijua hata Erica alikuwa ametulia kwake. Haikuwa hamu ya kumuona tu Erica lakini alikuwa na hamu ya kumfurahia katika kitanda cha mapenzi. Kama ulikuwa ni ukame basi ulizidi, ulikuwa ni usongo.

  Alipoondoka uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere hakutaka kwenda kwake alitaka kwenda moja kwa moja kwa Erica kumshtukiza kwa zawadi mbalimbali. Alifikiria kumpigia simu lakini akaona itaondoa utamu wa kumshangaza. Alikumbuka kuwa hakuwa na haja ya kufanya hivyo kwani mapema siku hiyo alikuwa amekwisha mwambia Erica kuwa hata kama angeenda nyumbani baada ya kutua uwanja wa ndege basi ingekuwa ni kwenda kutua mizigo tu lakini angeenda kwake hata kama ni usiku wa manane kwani alikuwa amemmisi kupita kipimo.

  Aliamua kwenda tu moja kwa moja kwa Erica hasa kwa vile kesho yake hakuwa amepanga kwenda kazini mapema hadi mchana wake. Gari ya shirika ilikuwa imeegeshwa katika eneo la jipya la kuegeshea magari ambapo alitakiwa kwenda kujitambulisha na kukabidhiwa ufunguo. Baada ya kukamilisha taratibu zote za kutoka uwanjani alichukua barabara ya Nyerere kwenda nayo hadi barabara ya Mandela na kutoka hapo kuelekea nayo hadi alipoipita barabara ya Morogoro ambapo barabara ya Mandela iligeuka na kuwa barabara ya Sam Nujoma. Uchovu wote ulikuwa unamuishia kwa jinsi adrenalini ilivyokuwa ikichemka mwilini. Kwa kadiri alivyokuwa anakanyaga mafuta ndivyo mwili wake ulivyozidi kuwaka tamaa, hamu na matamanio vilikuwa vimemzidia.

  Karibu dakika hamsini baadaye alifika kwenye lango la majumba ya Mivuleni. Alichomoa kadi yake na kuinyoshea kwenye chombo cha kupitishia funguo za kadi na mara taa ndogo iliyokuwa inamulika mulika rangi nyekundu ikageuka kuwa rangi ya kijani na geti likajiachia. Erica alikuwa amempa ufunguo wa geti na wa nyumba yake na hivyo vyote vilichangia imani yake kuwa yeye na Erica walikuwa wanaelekea zaidi ya kuwa wapenzi. Alikata kona upande wa kulia na kupita maghorofa matatu hadi alipofikia ghorofa la Erica. Mbele ya ghorofa kulikuwa na maeneo ya kuegesha magari ya aina mbili. Kulikuwa na sehemu ambayo ilikuwa na paa la bati ambapo magari ya wakazi yaliegeweshwa na upande mwingine ulikuwa na eneo lililochorwa chorwa alama za sehemu za kuegeshea magari ambapo wakazi na wageni waliweza kuegesha magari yao. Aliegesha gari lakeupande wa wageni.


  Giza lilikuawa limetanda kama mwamvuli lakini kwenye eneo la majumba ya pale Mivuleni lilipunguzwa na taa kubwa ambazo zilikuwa zimepamba mitaa ya eneo hilola makazi ya watu wenye kipato cha kati. Ujenzi na ramani ya majumba hayo ulinakili kwa kiasi kikubwa majengo ya Whispering Willows Apartments ya nje ya Jiji la Columbus, Ohio Marekani ambako mmiliki wake aliishi wakati anasoma Chuo Kikuu cha Ohio kampasi ya Columbus. Pembeni ya maghorofa yote pale na kulifanya eneo zima liwe na mwanga wa kutosha sana.


  Alex alienda nyuma ya gari na kufungua boneti na kuchukua kisanduku kidogo ambacho kilikuwa kimesheheni zawadi mbalimbali. Alikiweka chini huku akirudisha kufunga boneti. Akiwa mwenye furaha alielekea kwenye mlango wa kupanga ghorofa kuelekea maskani ya Erica. Alikuwa anatamani kucheka kwa furaha na hamu ikimzidia kwa kila hatua aliyopiga kupanda ngazi.


  Alipofika mlangoni kwa Jessica alitaka kubisha hodi lakini alisita - kwanini abishe hodi kwake. Hata hivyo aligonga mara ya kwanza na mara ya pili bila kujibiwa. Alisikia tu sauti ya TV kwa mbali na akajua Erica alikuwemo ndani labda yuko mbali na sebuleni. Aliamua kujaribu kuufungua mlango kabla hajachukua simu yake kumpigia ndani. Kwa bahati nzuri mlango ulikuwa haujafungwa. Alifurahi kwani kama Erica alikuwa bafuni anaoga basi angeenda kumshtukiza huko. Alipoingia ndani aligundua ni kweli sauti ya TV ilikuwa juu na harufu ya mapishi ilimkaribisha. Tumbo lilimsokota kwa njaa ya ghafla.


  Alifunga mlango nyuma yake kilichomshtua mara moja ni sauti ya mgumo wa mapenzi. Ulikuwa ni mgumo wa sauti ya kike iliyokuwa imenogewa katika mapenzi. Hakujua mara moja kama ilikuwa inatoka kwenye TV au jikoni, aliangalia TV upande wake wa kushoto lakini hakukuwa na kitu chochote kinachohusiana na mapenzi zaidi ya muziki. Alitembea taratibu kama kwa kunyata, hatua chache kuelekea jikoni. Kengele zote za tahadhari zilimuambia kitu ambacho hakuwa tayari kukiamini. Alikuwa anaoembea katika akili zake kuwa amkute Erica labda anajipa raha mwenyewe au kitu kingine kuliko alichokuwa anakihofia.  "Ericaaaa!!" Ndilo neno pekee aliloweza kulisema kwa sauti iliyojaa kilio, hofu, uchungu na maombolezo ya moyo. Sauti yake ingeweza kusikika kama mwangwi. Erica alikuwa amekumbatiwa juu ya meza, mgongo wake ukiwa wazi na mbele yake kijana wa makamu kiasi akiwa kifua wazi ambaye naye mikono yake ilikuwa imemshikiliza vizuri kabisa Erica na kutokumuachia. Walikuwa wamezama katika mapenzi, miili yao ikiwa imeloa jasho na harufu ya mahaba ikichanganyika na harufu ya chakula.


  Erica aligeuza shingo yake na macho yake kuyakutanisha na ya Alex, Imma alikuwa hajui achomoke au afanye nini kwani alikuwa amekaribia kufika kileleni. Erica alimsukuma Imma kumuondoa, Imma aliinama chini na kuanza kuhangaika kuvaa suruali yake. Hakujua kama amefumwa au ndio kafumania. Alex alikuwa ameacha mdomo wazi akitafuta neno la pili kusema. Alipatwa na kigugumizi cha ghafla. Uchungu aliousikia ulipenya kwenye ngozi, mishipa na kujikita hadi kwenye supu ya mifupa yake. Alijihisi kuishiwa pumzi, moyo ndani yake ulikuwa karibu upasuke. Alihisi kizunguzungu cha ghafla na kichefuchefu ambacho mtu anaweza kukipaa akiwa angani kwenye ndege. Alitaka kutapika lakini hakuweza.


  "Mungu wangu Erica unafanya nini" alifanikiwa kutoa sentensi ya pili. Alishindwa hata kupiga hatua moja mbele. "Ooh Mungu wangu!" Erica aliweza kusema kwa haraka huku akivuta gauni lakekifuani. Ambaye alikuwa amechanganyikiwa ni Imma. Hakujua afanye nini mara moja."Mbona hukuniambia kuwa una mume Erica?" Imma alifanikiwa kusema na kwa hivyo kujichongea.


  "Huyu ni nani Erica?" Alex alisema kwa sauti ya juu kama baba akimgombeza bintiye. Sauti yake ilinguruma ndani ya nyumba utadhani simba aliyewekwa zizini. Erica alikuwa amesharuka kutoka kwenye meza na mwili wake akiwa amuhifadhi. Imma alikuwa anatetemeka pembeni yake akijitahidi kuvaa shati lakekwa haraka. Wote wawili hawakujua Alex atafanya nini maana hasira iliyokuwa inawaka kutoka kwenye macho yake ingekuwa ni radi basi ingewararua na kuwaunguza hadi wawe majivu.


  "Kwanini umefanya hivi Erica, si ungeniambia kwamba una mtu" Imma aliuliza huku akijitahidi kuchomekea shati lake. Alikuwa bado na soksi zake miguuni.


  "I'm sorry, I'm sorry, I'm sorry" ndilo maneno pekee ambayo yaliweza kutoka kwenye kinywa cha Erica na wala hayakuwa wazi kama yaliekezwa kwa Imma au kwa Alex. Alikuwa amegeuka akiwa upande kidogo anamuelekea Alex ambaye alikuwa amesimama karibu na eneo la jikoni na Imma aliyekuwa amesimama kati ya meza na jiko. Alex alikuwa anatembea kwa kuzunguka zunguka huku kashika kiuno chake kwa mkono mmoja, kichwa chake akitikisa na kuguna kwa hasira.


  "Erica kwanini umefanya hivi?" Alisema kwa kunung'unika kulikojaa uchungu kutoka moyoni, uchungu ambao Erica aliweza kuisikia katika maskio yake lakini akikataa kuuruhusu upenye moyo wake. Erica alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.
  Imma alikuwa amemaliza kuvaa.

  "Kaka samahani sana, sikujua kabisa kuwa Erica ana mtu; nisingeanza naye kabisa" Alianza kuondoka. Aliamuangalia Erica wakati anampita Alex pale kizingitini "Erica umefanya vibaya sana, please don't call me" Alisema huku akitoka. Alikuwa na uchungu moyoni, uchungu ambao aliulewa maana yake. Alikuwa tayari kumuacha mke wake kwa penzi la kudanganywa. Alijisikia vibaya na hatia, alijiona mjinga kupita kiasi. Kwani kwa karibu wiki mbili nyuma alikuwa ameanza kuonesha dalili ya kutomjali mkewe wala kusaidia katika maisha ya mapacha akisingizia kutingwa na kazi zaidi. Alikuwa hajamgusa mke wake kwa mwezi mzima. Alipochukua ufunguo wake na jaketi alilokuwa amelitundika kabatini aliondoka bila kuaga tena. Alimuonea huruma Alex zaidi kwani alionekana ni mtu mzuri na asiyestahili jambo lile. Alijaribu kujiweka katika nafasi ya Alex na mara moja alielewa ule uchungu. Je akifika nyumbani na kumkuta mke wake kwenye sita kwa sita na mtu mwingine angejisikiaje? Aliuma midomo yake hadi kujisikia angeweza kuipasua na kuapa kutotoka tena kwenye ndoa yake kwani malipo yake katika maisha ya watu yanaweza kuwa makubwa kweli.


  Alex alikuwa anashindwa kumuangalia Erica. Hakutaka kusema lolote. Mawazo yake yalikuwa yanazunguka kama upepo wa tsunami. Alikuwa amechanganyikiwa kwani maisha yake yote yalikuwa yameanza kuzunguka kwenye maisha ya Erica. Hakutarajia usaliti wa aina ile. Uchungu uliokuwa moyoni ulikuwa ni u chungu uliomfanya ahisi mbavu zinambana.


  "Erica mbona nilikupenda sana" Erica alikuwa kimya. "Niangalie!" Alifoka. Erica aliyainua macho yake na ya kuyagonganisha na yale ya Alex. Hakukuwa na maneno kwa sekunde chache. "How long umekuwa naye huyu?" Kimya. "Talk to me!!!" Erica alishtuka na kusogea hatua moja nyuma. Aliangalia kushoto kulikuwa na chano cha visu. "How long?" aliuliza tena. "Wiki chache" alijibu kwa unyonge na kwa sauti ya kunong'ona. Alex alisogea karibu. Kati yao kulikuwa na ombwe la aina yake. "Erica, I really loved you I surely did!" kwa sauti ya taratibu, iliyojaa uzito, hasira, uchungu na kukerwa kwa daraja ya kwanza Alex alisema. Alikuwa anatikisa kichwa chake na kusonya huku akifyonza.


  "I'm sorry Alex" alisema. Maneno yake hayakuwa na ushawishi, macho yake yalikuwa makavu. Alikuwa anamuangalia Alex alivyokuwa anasogea karibu. "Nimeumia sana Erica, natamani ningefanya kitu kibaya hapa leo lakini its not worthy it" Alex alisema huku akimnyoshea kidole cha kutuhuma Erica. Hakutaka hata kumsogelea tena. Machozi yalikuwa yameanza kumlenga taratibu. Alimuangalia Erica ambaye naye alikuwa anamuangalia machoni kama kwa kumuibia hivi.

  Erica alikiona. Alikiona kile alichokuwa anakitafuta. Kilikuwa kimefichika ndani ya macho ya Alex lakini kilijitokeza pale aliposogea karibu. Macho ya Alex yalikuwa yamejaa huzuni, kukata tamaa, hasira na kinyongo cha kusalitiwa. Erica alimuangalia Alex jinsi mikono yake ilivyokuwa inatetemeka kwa hasira na sauti yake ilivyokatika katika. Alex aligeuza na kuanza kuelekea nje.

  "Alex I'm sorry" alijaribu kumwambia. Alex aligeuka alipofika mlangoni. "I"m more than sorry, najuta kukufahamu na kukupenda" Alex alisema akifunga mlango nyuma yake na kuacha ombwe la hisia za penzi lililosalitiwa.


  Erica alikuwa amesimama pale pale alipoachwa na Alex. Hisia zake zilikuwa kinyume kabisa na ambavyo ingetarajiwa. Hisia ya joto la kufanya mapenzi lilikuwa limechanganyika na hofu ya kufumaniwa na vile vile furaha ya kuona amefanikiwa kumfanya mtu mwingine asikie uchungu wa kusalitiwa. Alienda na kuufunga mlango na makomeo yake yote. Hakujisikia vibaya wala kujuta. Alijisikia zaidi ahueni kuwa amefanikiwa katika jaribio lakehilo la kwanza. Alikuwa ameachana na wanaume wote wawili na alikuwa mtu huru tena. Alikuwa ameshikwa na hasira, hasira ya kwanini alifikishwa katika nafasi kama hiyo. Sam aliwaza.


  Alielekea bafuni kwenda kuoga. Alipoingia na kujichojoa nguo alianza maji ya mvua yaumwagikie mwili wake na kumsafisha na uchafu wote wa Alex na Imma. Akili yake ilikuwa mbali kabisa. Alikuwa anawaza ni nani ataingia tena kwenye anga zake na kuonja tamu ya kisasi chake. Wanaume wangemkoma alijiambia moyoni. Alimlaani tena na tena - labda kwa mara ya milioni - Sam. Alipotoka bafuni baada ya muda kidogo alienda kujipashia chakula na kula taratibu pale pale jikoni na baadaye kujilaza chali sebuleni kwenye kochi kubwa akiwa anaangalia TV. Mawazo yake hata hivyo yalikuwa mbali kabisa. Alikuwa anafikiria itakuwaje watakapoonana tena ofisini na Alex.


  Usingizi ulianza kumchukua taratibu. Bustani.


  Barafu ya bustani yake ilianza kuwa ya rangi ya kijivu. Vipepeo nao walianza kutoweka. Moyo wake ulikuwa unazidi kuwa wa baridi. Alijiambia moyoni jinsi gani mapenzi ya mwili yalivyokuwa matamu bila kuutoa moyo wake. Aliguna kidogo alipojitambua uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kuweza kumfanya mwanamme ampende upeo bila yeye mwenyewe kufungua hata sentimita moja ya moyo wake. Wanawake wamekuwa wakifanya hivi kwa maelfu ya miaka, wanaume hawajui tu - alijiambia. Usingizi ulimpitia taratibu huku akiota kuwa amegeuka kuwa njiwa wa kijivu akiruka kwenye bustani yake. Alisikia kwa mbali wimbo wa Tina Turner - What love's got to do with it. Alitabasamu. Its only a second hand emotion. Njiwa aliruruka akikataa kutua kwenye barafu.

  Inaendelea...

  .... Kama unafikiri umewahi kusoma simulizi la mapenzi basi hujasoma kisa cha Erica Lugo....

  soon in bookstore near you.. don't mind the file name..
   

  Attached Files:

 2. Imany John

  Imany John Verified User

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  mwandishi ni nani?
  Da anajua sana kukoleza.
   
 3. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Inakataa kuachia!!
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  dah hongera Mwanakijiji hadithi nzuri sana ..keep it up ...ila mwisho imeniikitisha
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Au imeng'ang'ania?
   
 6. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  nini hiyo?mia
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hongera mkuu,ni story nzuri ila mwisho wake mmmh!
   
 8. N

  Ndomse New Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah Anajua kupenda!!!!!
   
 9. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  mbona sura ya kumi?
   
 10. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  imma alipofika alimkumbatia erica kwa mahaba ya dhati,,,..... tutaendelea kesho
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Unaonjeshwa...ukipenda unanunua kabisa kwa raha zako!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna sura tisa nyuma yake na nyingine mbele yake. Itakapofika mwisho nashauri uwe na box la tissue maana hata mi mwenyewe nilishindwa kujizuia
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160

  Ukiona Mtu mzima analia basi ujue yamemkuta
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Wakati anamkumbatia alikuwa anajisikiaje?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Taratibuu naona wengine wamelalamika wanashindwa kudownload... so nimeposti sura nzima kwenye posti ya kwanza kwa wale wanaosoma kwa kutumia simu
   
 16. Imany John

  Imany John Verified User

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Mtunzi ni nani?mbona kimya mkuu?
   
 17. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  rahaaaa utamu raaaaa utaam
   
 18. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  umepotelea wap wewe?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mimi mwenyewe...
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mbona huo siyo mwisho? ni mwisho wa hiyo sura tu... hata mchezo wenyewe kwa kweli bado haujaanzaa... fikiria kama ni mechi basi ni half time... unayefikiria kafungwa aweza kuwa siye anayeshinda pambano kipenga cha mwisho kikilia..
   
Loading...