Majeraha ya paja yamuondoa Mo Salah AFCON, kurejea Liverpool kwenda kutibiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Uongozi wa Timu ya Taifa ya Misri umethibitisha kuwa mshambuliaji wao Mohamed Salah (31) amerejea katika klabu yake kupatiwa matibabu zaidi baada ya kuumia misuli ya paja katika mchezo dhidi ya Ghana kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Salah au Mo Salah ataukosa mchezo wa leo Januari 22, 2024 dhidi ya Cape Verde na kama Misri itafanikiwa kuendelea na michuano kuna uwezekano wa kurejea kuendelea kuitumikia Timu yake katika michuano ambayo itafikia tamati Februari 11, 2024.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wamemrejesha klabu kwa kuwa si kawaida ya Salah kupata majeraha hayo na ndio maana wameongeza umakini katika matibabu yake.
 
Kweli uongo kipaji.

Na mleta mada umebarikiwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom