Majarida haya na watunzi wake:wako wapi?

Teh Teh Teh Umenikumbusha kina Kaboka mchiz, Zena na Betina, madenge cjui usitake nicheke na Yule Mzee kifimbo cheza Mzee wa kurekebisha Kiswahil, mambo ya digital yameharib kila kitu,cjui google, yutube,iPad,iPhone,imarc,Facebook,twitter, instagram etc wiz mtupu kila kitu Watu wana google tu cku iz,hakuna tena kusoma vijarida wala novel Aya tutaanzia wap kumgoogle Zena na Betina cye analogy..?hatar sana

Wewe siyo wa analog ni digitali hebu angalia hizo red.
 
Usilinganishe jarida la sani na yale ya tabasamu na bongo la sani kitambo sana enzi za toto tundu, mpingo, pimbi, prof ndumilakuwili,kipepe,zumo,obi,ole,linda,mzee profesa,zena na betina,kifimbo cheza,madenge,kipepe,mwinyi mpeku,mzee sani mwenyewe,na ile makala ya jambo limezua jambo, Je unaikumbuka stor ya kisiwa cha kitintale? Ebana huo mzigo miaka ya90 duh.

mkuu sikatai kuwa Sani lilikua ni kongwe,ila ninachosema mimi majarida ya Bongo na Tabasamu yalileta ushindani mkubwa sana kwa sani,na yalipendwa sana watu.unakumbuka majina ya kikosi cha Bush stars ndugu.
 
madenge,mzee meko,kipepe wengine endelea mwenyewe
 
Vijana mnisamehe kwa uwazi huu. Akili za watoto tuliowazaa zina mambo mawili tu kwa sasa. Wanawaza ngono na viloba, basi. Ukitaka kujua we angalia tu humu JF. Angalia Forum za MMU kuna post ngapi, na Forum za Biashara kwa mfano, kuna post ngapi... Server zimejaa ushauri wa ngono wakati biashara hata robo ya post za MMU haifiki.

Unganisha dots hapo

hapo chacha! wananikera mpaka basi!!!!
 
Ninavyojua john kaduma ndiye alikuwa mchoraji mwanzilishi wa SANI, na haya mengine yalifuata baada ya john kununuliwa
 
Kuna mchora katuni wa enzi hizo alikuwa akijulikana kama Nicco ye Mbajo. Ni jina lililokuwa likinifurahisha sana. Sijui yuko wapi siku hizi. Mchoraji mwingine wa enzi hizo ninayemkumbuka ni Deo Babili.
 
mzee unakumbuka vizuri.Ukurasa wa 'darasa la mapenzi' ulikuwa ukipendwa sana na wasomaji wa gazeti la HEKO.Ni kweli mmiliki wa gazeti hilo Ben Rashid mtobwa alikuwa akiandika lakini si hadithi zote,zingine ziliandikwa na waandishi mbalimbali.Mimi ni mmojawapo niliyekuwa naandika ukurasa huo.Moja ya darasa tamu aliloandika BEN nakumbuka ni 'siku niliyokufa kifo kidogo' huyu jamaa ni muandishi aliyekuwa na uwezo kuchezea na lugha namna anavyotaka.Alikuwa fundi ambaye sikumpatia mfano wake hapa TZ.Ndiye mtu aliyenifanye nipende sana kuandika hadithi na kujifunza uandishi
Darasa la Mapenzi ilikuwa hadithi inatoka kwenye Heko. Na mwandishi (au niseme Mwalimu wa hilo Darasa) alikuwa mmiliki wa gazeti mwenyewe, Ben R. Mtobwa. Katangalia mbele ya haki sasa; hayupo.
 
Unakumbuka mtoto Vicky, alikuwa mzuri sana na alikuwa ameolewa na mzee mwenye mihela wao walikuwa watu wa matanuzi tu shopping Geneva, Paris London, likini ndani hakuwa na raha.

Hadithi ilitungwa na Said Mbwana Makatta Bhawji. Ilikuwa inaitwa maji Mazito (Jina la Jambazi Kapuko wa Kapuko).

Umesahau 'FAHARI' kiboko cha majarida. Mtunzi alikuwa Freddy Jimm Mdoe.

Da umenikumbusha mbali. Nakumbuka FAHARI lilikuwa gazeti la kawaida na jina lake lilikuwa la mwandiko mwekundu.

Nani anakumbuka Busara lilikuwa jarida la miaka ya 80. Lilikuwa mpinzani wa Sani wakati ule kati ya 1981-1985. Haya niiteni 'mzee'.

Nakumbuka Busara. Marehemu Mzee Hammie Rajab amepta kuandika humo. Hata character "Power Mbulumundu" aliyekuja kuchorwa na John Kaduma nadhani katika Tabasamu kwa jina la Power Mbulumbundu alitokea katika jarida la Fahari. Vituko vya Mbulumbundu/Mbulumundu vilifanana na Baba Ubaya aliyeanzia katika Jarida la KIU.

Kulikuwa na Mcheshi pia miaka ya 80, wanawake wa Mcheshi walikuwa wanachorwa na mahips, miguu chupa ya bia!!

Well, niseme nini hapa!!!!!?? Honestly nimelog in ili nirespond kwa sentensi hii. Kwanza asante kwa kunikumbusha Jina la Mcheshi. Nilikuwa nawaza hawa wanawake wenye mahipsi, mapaja yanayong'aa, macho yaliyolegea, nywele za Afro na mashavu yanayomeremeta nilikuwa nawaona katika jarida gani. Heshima sana kwako "mzee" Sky Eclat.

Naomba nikuzawadie Vicky, Omari Kisila na Mzee Mkongwe.... Maji Mazito. Respect!!

SANI 2b.jpg
 
mzee unakumbuka vizuri.Ukurasa wa 'darasa la mapenzi' ulikuwa ukipendwa sana na wasomaji wa gazeti la HEKO.Ni kweli mmiliki wa gazeti hilo Ben Rashid mtobwa alikuwa akiandika lakini si hadithi zote,zingine ziliandikwa na waandishi mbalimbali.Mimi ni mmojawapo niliyekuwa naandika ukurasa huo.Moja ya darasa tamu aliloandika BEN nakumbuka ni 'siku niliyokufa kifo kidogo' huyu jamaa ni muandishi aliyekuwa na uwezo kuchezea na lugha namna anavyotaka.Alikuwa fundi ambaye sikumpatia mfano wake hapa TZ.Ndiye mtu aliyenifanye nipende sana kuandika hadithi na kujifunza uandishi

nimefurahi kusikia ulikua ni mmoja kati ya waandishi katika majarida yale,labda nikuulize kitu kimoja;KWANINI MAJARIDA YALE YAMEPOTEA ILIHALI YALIKUA YANAPENDWA SNA
 
mzee unakumbuka vizuri.Ukurasa wa 'darasa la mapenzi' ulikuwa ukipendwa sana na wasomaji wa gazeti la HEKO.Ni kweli mmiliki wa gazeti hilo Ben Rashid mtobwa alikuwa akiandika lakini si hadithi zote,zingine ziliandikwa na waandishi mbalimbali.Mimi ni mmojawapo niliyekuwa naandika ukurasa huo.Moja ya darasa tamu aliloandika BEN nakumbuka ni 'siku niliyokufa kifo kidogo' huyu jamaa ni muandishi aliyekuwa na uwezo kuchezea na lugha namna anavyotaka.Alikuwa fundi ambaye sikumpatia mfano wake hapa TZ.Ndiye mtu aliyenifanye nipende sana kuandika hadithi na kujifunza uandishi

Ben alikuwa mtu wa vipaji vingi, ingawa watu wengi hawakuwa wanajua. Alikuwa na kichwa cha mahesabu na sayansi sana pia. Miaka ya mwishoni mwa miaka ya 70, kile kipindi cha vita ya Idd Amin ben alikuwa Dar tech. Sielewi kitu gani kilimtuma kuanza uandishi kwa sababu taarifa zinasema hakufeli masomo Dar tech.

Nakumbuka kitabu chake cha kwanza kilihusu maisha ya DR. REmy Ongala. Alianzia hapo akapata vihela baadae nikasikia kesha kuwa mwandishi mkubwa kabisa na mambo ya sayansi kaachana nayo. Ni jambo la kusikitisha alipata kifo kikubwa baadaye na mungu kamchukua.
 
Hadithi ilitungwa na Said Mbwana Makatta Bhawji. Ilikuwa inaitwa maji Mazito (Jina la Jambazi Kapuko wa Kapuko).

Da umenikumbusha mbali. Nakumbuka FAHARI lilikuwa gazeti la kawaida na jina lake lilikuwa la mwandiko mwekundu.

Nakumbuka Busara. Marehemu Mzee Hammie Rajab amepta kuandika humo. Hata character "Power Mbulumundu" aliyekuja kuchorwa na John Kaduma nadhani katika Tabasamu kwa jina la Power Mbulumbundu alitokea katika jarida la Fahari. Vituko vya Mbulumbundu/Mbulumundu vilifanana na Baba Ubaya aliyeanzia katika Jarida la KIU.

Well, niseme nini hapa!!!!!?? Honestly nimelog in ili nirespond kwa sentensi hii. Kwanza asante kwa kunikumbusha Jina la Mcheshi. Nilikuwa nawaza hawa wanawake wenye mahipsi, mapaja yanayong'aa, macho yaliyolegea, nywele za Afro na mashavu yanayomeremeta nilikuwa nawaona katika jarida gani. Heshima sana kwako "mzee" Sky Eclat.

Naomba nikuzawadie Vicky, Omari Kisila na Mzee Mkongwe.... Maji Mazito. Respect!!

View attachment 95485

Well said.
 
Nakumbuka ndani ya SANI kulikuwa na mtunzi mahiri anaitwa Amri bawji,jamaa alikuwa ananikosha sana kwa hadithi zake kama Love story tanganyika na unguja,
Na mtunzi flani alikuwa gazeti la lete raha anaitwa Beka mfaume, namkubali aliachia hadithi miaka ya nyuma yaitwa mzee beka niliikubali, vipaji vipo sana bongo ila ndo hivyo
Hiyo Love Story-Tanganyika na Unguja ilitengenezewa movie, sina uhakika kama ipo madukani. Nilishawahi kuiona Channel 10 miaka kama 10 iliyopita. Ni nzuri sana.

nikianza kuwataja akina kaduma na ibra washokera nitaonekana babu humu,hebu ninyamaze.

John Kaduma ni marehemu, ila Ibra Washokera bado anachora katuni kupitia gazeti la Mwananchi, ukurasa wa mwisho kabisa (Bwana Chezo)
 
Hadithi ilitungwa na Said Mbwana Makatta Bhawji. Ilikuwa inaitwa maji Mazito (Jina la Jambazi Kapuko wa Kapuko).

Da umenikumbusha mbali. Nakumbuka FAHARI lilikuwa gazeti la kawaida na jina lake lilikuwa la mwandiko mwekundu.

Nakumbuka Busara. Marehemu Mzee Hammie Rajab amepta kuandika humo. Hata character "Power Mbulumundu" aliyekuja kuchorwa na John Kaduma nadhani katika Tabasamu kwa jina la Power Mbulumbundu alitokea katika jarida la Fahari. Vituko vya Mbulumbundu/Mbulumundu vilifanana na Baba Ubaya aliyeanzia katika Jarida la KIU.

Well, niseme nini hapa!!!!!?? Honestly nimelog in ili nirespond kwa sentensi hii. Kwanza asante kwa kunikumbusha Jina la Mcheshi. Nilikuwa nawaza hawa wanawake wenye mahipsi, mapaja yanayong'aa, macho yaliyolegea, nywele za Afro na mashavu yanayomeremeta nilikuwa nawaona katika jarida gani. Heshima sana kwako "mzee" Sky Eclat.

Naomba nikuzawadie Vicky, Omari Kisila na Mzee Mkongwe.... Maji Mazito. Respect!!

View attachment 95485

Hadithi za Mlima Kolelo kwenye gazeti la Busara, R.I.P Hammie Rajabu.
 
Mkuu umenikumbusha stori za profesa ndumilakuwili, kuna siku moja alienda kumuibia dokta love pimbi wakati pimbi akiwa amesafiri, alikata bati la nyumba ya dokta kwa mkasi akapitia darini, akakomba kila kitu akafungasha kwa kutumia shati lake lililotengenezwa na mtaliano. Kuna stori ya 'Damu nzito kuliko maji' hii nafikiri ilikuwa ya miongoni mwa hadithi za mwishomwisho.

Kwenye gazeti la bongo nakumbuka stori ya 'anga za wenyewe' na 'msako wa mr x'

kama walivyosema wachangiaji wengine Sani lilikuwa kongwe zaidi ya tabasamu na bongo.

Siku hizi kutokana na mabadiliko ya teknolojia na ujio wa vifaa vingi vya teknolojia, imekuwa rahisi mno kwetu kupata burudani katika vifaa hivi kuliko kusoma vitabu/majarida/magazeti

Muda ambao majarida yalianza kufifia (mwanzoni mwa miaka ya 2000) ndiyo muda ambao watu wengi walikuwa wanaweza kupata tv, tamthilia/filamu/miziki ya ndani na nje ilipata umaarufu katika jamii, na matumizi ya kompyuta/internet kuongezeka hivyo kama ilivyo hulka yetu watanzania tukamezwa na burudani za nje na zile zenye muundo huo, mathalani mwishoni mwa miaka ya 80 ungeweza kukuta vijana wanaazimana majarida ya sani, magazeti au riwaya(novels kama za JH Chase) lakini baada ya mwaka 2000, huwezi ukakuta vijana wanamwamko wa kusoma au kuazimana vitu hivyo, muda huo utaonekana ni ushamba, ujanja/ukisasa ni kuwa na cd za nyimbo/filamu za nje na vifaa vingine vya elektroniki.

Lakini kikubwa ni kwamba watanzania ni wavivu mno wa kusoma, kuna watu unaweza hata kupita mwezi mmoja hawajasoma gazeti.

Kama waandaaji wa haya majarida watasoma hapa watangaze utaratibu wa kuuza zile kopi za zamani kwani wapenzi wa hayo majarida tupo wengi
 
kaka umechangia vizuri sana,palipo nivutia zaidi ni hiyo paragraph ya mwisho kwamba wanaweza kuanza kutuuzia majarida yale ya zamani,hta mm nitakuwa wa mmoja wapo katika kuyanunua,swali ni je watakua na kumbukumbu za copy zile ili waweze kuzi-reproduce?
 
Katika visa vilivyokua na wapenzi wengi ni mechi ya watani wajadi Bush Stars na Born Town. Mtangazaji alikua ni Sukununu.

Bush Stars walikua na mtu anaitwa Mapungo, huyu jamaa alikua tishio sana katika ufungaji kiasi cha kupewa hadi mke kwa ile heshima aliyowapa Bush Stars.

Kuna mechi moja mapungo alipewa pasi ya mwendo kisha kumuacha beki wa Born town nakuachia shuti Kali lilogonga mwamba na kurudi mpaka golini kwao kisha kuingia na refa kusema ni goli.....vurugu zilizuka kwa kina mapungo kukataa sio goli na kufanya pambano kuvunjika.

Kuna game nyingine Born town walifunga goli kwa tikitaka....lakini Bush Stars waligoma sio goli eti mtu hawezi funga goli kwakua kalipa kichogo!
 
hahaa nimecheka sana mkuu,unakumbuka Mapung'o alishachezea hadi manchester united?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom