Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,787
Kila zama na kitabu chake...kwa ambao tumezaliwa vijijini tulipata bahati ya kujua robo ama nusu kabisa ya yaliyokua yanajiri mjini kutokana na watunzi na masanii mahiri wa zama za nyuma kidogo..Nimekuwa mpenzi wa muda mrefu sana wa majarida tajwa hapo juu na hakika pamoja na kutokuwa na kipato wakati huo ila nilijidunduliza na kuhakikisha kila mwezi najinunulia nakala tatu kwa maana ya Sani,Bongo na Tabasamu...
Kwa kua inspired na kazi za watunzi waliobobea kama kina John Kaduma (R.I.P) E.P. Ndoda,Abrahman Dohu,4T Ndila,Dikwe Ndoto,Katembo na wengine kwa wingi wao leo najivunia matunda ya msukumo nilioupata...Mungu azipe pumziko la heri roho za wasanii na watunzi wa hadithi,riwaya na tamthiliya ambao walitupa nuru wakati digital ikiwa mapumziko ughaibuni...