Majangili Wakichina Ndani Ya Serengeti

Majangili Wakichina Ndani Ya Serengeti

Nairobian

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
873
Reaction score
2,283
-Wakuu hizi ni habari za uhakika kutoka kwa ndugu ambao wanaishi ndani ya hifadhi ya Serengeti. Habari zenyewe ni kwamba, kuna wachina wanaotembea na magari mawili aina ya Landcruiser za kusafirisha watalii na NOAH (yenye vioo vyeusi) wanaingia ndani ya hifadhi na kuwaua Tembo.

-Wakazi na Vijana wanaoishi na kuchunga ng’ombe ndani ya hifadhi wamewaona Wachina mara kadhaa. Ila majuzi (Jumapili) Wachina kama watatu wakisindikizwa na watu waliovaa sare za askari wa wanyamapori, wakiwa na silaha nzito, waliingia ndani ya Serengeti na kuiua familia ya Tembo tisa na kuwanyofoa pembe zao .

-Inasemekana hichi kitendo kilifanyika chini ya lisaa. Ina maana hao tembo waliuwawa na meno yao kunyofolewa chini ya lisaa limoja. Hawa vijana baada ya kusikia milio ya Bunduki, walilazimika kujificha huku wakiangalia kitendo kizima na hatimaye meno ya tembo kupakiwa ndani ya Landcruiser . Vijana hao waliogopa kuomba msaada wakidhania wangeuawa na hao majangili hao.

-Hawa wachina uonekana siku za Jumapili au jumamosi tu.Wachina wanapanda Noah huku wale (weusi) waliovaa sare za Askari wanyama pori wanatembea na Landcruiser ya Kijani yenye nembo ya TANAPA. Siku zote Landcruiser ndio utangulia, na mara nyingi wanatoka ndani ya hifadhi kuelekea Mugumu
 
Hii itadharauliwa na kupuuziwa kama story tu, lakini ijulikane ni kila siku Tembo kadhaa wanadondoshwa, kwa pace hii iloyoko sasa hivi baada ya miezi miwili Serengeti, Ngorongoro na Tarangire zitakuwa hazina Tembo hai tena, ni harufu tu ya mizoga.


Tupige Vita ujangili.

iWorry.
 
Hawa Wachina Watatulia Tukiwahukumu Kunyongwa Hadi Kufa
 
hii mortality rate ya tembo inasiktisha.lakini kinachosikitisha zaidi ni pale unapokutana na masikini mwenzangu anashabikia mauaji ya wanyama hawa akidai haoni faida zake.
 
Hawa Wachina Watatulia Tukiwahukumu Kunyongwa Hadi Kufa Lakini Nina Mashaka Ni Wale Waliokuja Juz Kat Na Meli Na Kupokelewa Na Mwamunyange
 
Waziri wa hii wizarakwa sasa ni nani kwani?
 
Nairobian. Hii ni kweli kabisa! Nawashangaa askari wa TANAPA pamoja na mishahara minono lkn bado wanadanganyika kwa wachina?! Tuseme nn kwa wale wengine wa GAME ambao vimshahara ni vidogo! Shame on them~TANAPA SERENGETI.
 
Ngoma Droo:
Wachina wanaua Tembo wetu; Wabongo tunaruhusiwa kupeleka Sembe China.
 
mkuu mleta mada,huoni kama unachonganisha Tz na China?hizi nchi ni marafiki na hata ccm na chama cha huko ni marafiki.
pia mchina kaahidi kutulinda kwa garama yeyote!
 
Hii yote nishauri ya kuwa na serikali legelege. Tutaimba sana lakini watatupuuza!
Halafu baadae watapanda kwenye majukwaa kunadi sera za kijinga kwa kanga, tshirt na kofia za kijani na njano! Poor you CCM shame on you JK!
 
Wangetoa hata namba za hayo magari labda ingesaidia kuwabaini.

Next time waambie warecord namba, muda na siku ya tukio
 
Kwa hapa tulipofika bora waishe tusahau kabisaa na ibaki stori ya Tembo..
Wachina endeleeni hadi waishe tubakie tu Mlima wetu Kilimanjaro. Na huo mkiupenda ubebeni pelekeni kwenu sisi hapa niwakulima tutalima tu hatutakufa njaa.
 
Umesema hizo gari zinaonekana mara kwa mara sasa inakuwaje vijana wameshindwa hata kusoma namba maana rangi wamezitambua na sio mara moja.
 
Yani natamani ningechukua nafasi ya hao wananchi huko serengeti alaf niwe na haka kamchina kangu nirekodi tukio zima
 
Back
Top Bottom