Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,008
Mwanakijiji ,
Nnachoshindwa kuelewa ni kitu kimoja , nimesoma comments zako kwenye hii issue na kitu ambacho ninachoweza kusema ni kuwa tayari umeshawahukumu hawa polisi . Statement ulizotumia kama kumpiga mtu risasi tena akiwa amegeukia nyuma au mauaji ya wazi ni mauaji ya wazi yanathibitisha hilo .
Swali langu kwako kwa nini unakuwa mwepesi kuwahukumu hawa polisi ? Na jee una hakika gani kwamba haya majambazi yalipigwa risasi kwa nyuma ? Inakuwa ni vigumu kwangu kukubalina na lile unalolisema wakati inaonekana dhahiri you have preconceived opinion katika hii issue.
Rufiji.. unachukulia vitu nje ya context. maswali yangu yote ninayoyauliza ninayauliza kutokana na habari ambazo tayari ziko hadharani. Sijawahakumu Polisi ila ninahoji kuwa taarifa pekee za tukio hilo zimetolewa na watu pekee waliohusika na tukio hilo. Kuna ubaya gani kupata external opinion ili kuthibitisha maneno hayo ya Polisi? Kama Polisi hawakufanya lolote kinyume cha sheria si wawe wa kwanza kuiita tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora?
Hadi hivi sasa, nina wasiwasi na stori nzima ya Polisi na hayo ninayoyauliza kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari na Polisi wenyewe ndiyo vitu vinavyohitaji kuchunguzwa. Maoni yangu mimi hayana thamani yoyote ile ila maswali yangu ndiyo ya msingi.
Zaidi ya yote nina taarifa ambazo zinanifanya nihoji mambo haya...kwani POlisi wanafahamu kuwa watu wengi hawafahamu kilichojiri jioni ya tukio. Bahati mbaya... kuna watu waliokuwa karibu na ni wao ambao Tume ya Haki za Binadamu inaweza kuzungumza nao