mhizika
Member
- Jun 2, 2018
- 8
- 4
Dar es Salaam. Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Benard Rwanda amewataka majaji na mahakimu nchini kutumia busara, kuzingatia sheria na miiko katika kutoa haki mahakamani.
Amewataka kutojaribu kumtia hatiani mtu kwa kuwa tu wanajua tabia yake ni mbaya, bali wafanye hivyo baada ya kujiridhisha kuwa mhusika ametenda kosa.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 27, 2018 katika hafla ya kumuaga pamoja na mwenzake Jaji mstaafu Sauda Mjasiri iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu, jijini hapa.
Ametoa miiko 10 kama wosia kwa majaji na mahakimu na kuwataka kuhakikisha wanatumia busara na kuzingatia sheria inavyosema kwa kuwa mahakamani kila hatua ni sheria.
Ameitaka mahakama kujenga imani kwa wananchi, akieleza kuwa imani hiyo ndio nguzo muhimu ya mahakama na si sheria pekee.
“Wananchi wasipokuwa na imani na mahakama itakuwa ni hatari. Hapa majaji na mahakimu wafanye kazi kwa kufuata miiko na wajaribu kuangalia wasifanye vitu ambayo ni vya ajabu ajabu,” amesema.
Amewataka majaji na mahakimu kutokwepa majukumu yao katika kutoa maamuzi ya haki.
Akiwazungumzia wastaafu hao, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema Jaji mstaafu Rwanda ametumikia mahakama kwa miaka 37 huku Jaji Mjasiri akikitumikia chombo hicho cha Dola kwa miaka 15.
Source: Mwananchi