Neno Jaji, lina heshima kubwa sana Duniani. Na watu wakisikia mtu ni jaji, wanatarajia utakatifu ndani ya huyu mtu. Huyu siyo mtu wa kusukumwa sukumwa tu au kuamrishwa na watawala.
Kuna nchi, jaji mkuu na jopo lake wanao uwezo hata wa kumsimamisha kazi Rais, na kisha kusubiria hatua nyingine.
Hawa wa kwetu:
1. Wanateuliwa na Rais, hata kama huyo Rais hajui chochote. Mkiwa na Rais asiyejua chochote au anaendeshwa na wahuni, mnatarajia atateua jaji mkuu wa namna gani, majaji wa namna gani?
2. Hawa wa kwetu, kama inavyofahamika na ilivyohibitishwa na aliyekuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa CCM, bwana Rostam, ili kutoa hukumu, wanasubiria kuambiwa na serikali waseme nini; hivi hao kweli wanatakiwa kuitwa majaji? Jaji huwa ni mtu mwenye maamzi, hawa wa kwetu hawana maamuzi. Kiuhalisia hawa walitakiwa kuitwa vibarua wa watawala mahakamani, maana kibarua huwa hafanyi maamuzi yoyote bila ya kuambiwa na mwajiri wake.
3. Kwa kesi zote zinazohusu uovu wa watawala au serikali kwa ujumla, sote tumeshuhudia, hata wale ambao hawana hata elimu ndogo kabisa ya masuala ya sheria, jinsi hawa vibarua wa watawala mahakamani wanachofanya mahakamani. Wao wenyewe hujionesha wazi kuwa ni inferior kabisa mbele ya wale wanaoitwa mawakili wa serikali ambao ndio huwa wamepewa maelekezo ya moja kwa moja na watawala, jinsi hukumu inavyotakiwa kuwa kwa siku hiyo.
4. Kwenye kesi iliyotengenezwa na watawala dhidi ya Lisu, hawa vibarua wa watawala mahakamani, ndiyo wamedhihirisha kwa kila mtu jinsi wasivyo na mamlaka yoyote yale, isipokuwa kusubiria maelekezo ya mawakili wa serikali. Hata bila ya sababu ya msingi, mawakili wa serikali waliposema hakimu aahirishe kesi, hakimu alikuwa hana cha kufanya, zaidi ya kutii.
NB:
Siku nchi ikiwa huru kutoka kwenye mikono ya wahuni, taasisi ya kwanza inayotakiwa kufutwa na kuundwa upya, ni MAHAKAMA. Tasisi hii ambayo ni muhimu sana kwa ustawi wa haki wa Taifa, imechafuliwa mno, na sasa haina maana yoyote, na inatumika na wahuni kama chombo cha kubariki udhulumaji wa haki.
Taasisi ya pili itakayotakiwa kuundwa upya ni Jeshi la Polisi, ambalo sasa linatumika kama jumuia ya Chama Cha Mapinduzi.
Na taasisi ya tatu inayotakiwa kuundwa upya, ni TISS, ambayo kwa sasa inafanya kazi kama genge la wahuni.
Taasisi hizi ni muhimu sana katika ustawi wa haki na amani ya Taifa, lazima hizi taasisi tatu zifutwe na kuundwa upya ili ziutumikie umma badala ya kufanya kazi kama magenge ya wahalifu dhidi ya umma.