Maiti zaidi za wana CHADEMA zaokotwa Igunga!

Kwa binadamu yeyote mwenye hofu na Mungu ni vyema Kafumu akarudisha hekima yake kwa kujiuzulu ubunge ama la sivyo Mungu hapendi na kama damu ya Yesu ndo hii ya kwetu basi inalia na kamwe kilio cha damu hakitapita hata kwa vizazi vyao...damu inatoka kwa Mungu na kamwe damu hainunuliwi kwa pesa wala almasi,thamani ya damu ya watanzania wa Arusha,Igunga na kwingineko inaililia ccm na endapo damu hii ikijibiwa,Mungu akijibu,ccm mtapatilizwa na mauti ya karne


Tafadhari Kafumu achia ubunge wa damu,ubunge wako unanuka damu,unachululuzika damu...unadaiwa damu.
 
Yaani hao wanaodaiwa kuuawa hawana hata majina mkuu? kama mmpoja alikuwa maarufu hapo Ulaya kwa nini usimtaje, tutathitishaje kwa maelezo haya yanayo ning'inia?


Uthibitisho tafadhali ili kuepusha chuki zisizo na msingi baina yetu!

Nadhani unastahili kujibiwa.

Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.
 
2015 ifike tuchinjane tu ...minishajichokea na mingonjera hii kila siku..tutwangane kwanza ndo tutawekana sawa
 
Mimi siyo mdini ila nilikuwa nahisi tu...!

Tunalia polisi wafanye uchunguzi lakini mpaka sasa hivi hali ikoje?
kwa kuwa jeshi la polisi liko wizara ya mambo ya ndani , nimejaribu kuangalia(kwa mtazamo wa kisheheshehe) safu ya viongozi wake nikakutana na hiki....!
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi: Shamsi Vuai Nahodha
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi: Balozi Khamis Kagasheki
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi : Bw Mbarak Abdulwakil
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani : Bi. Mwamini Juma Malemi

-----
Mkuu wa Polisi : Saidi Mwema
-----
Usalama wa taifa ambao ndiyo unahusika na hata kuchakachua matokeo ya uchaguzi ili CCM ibaki madarakani iko chini ya
Rashid Othman.

Hii arrangement nadhani siyo ya bahati mbaya ...nadhani imewekwa hivyo ile kuweka harmony fulani katika utoaji wao wa maamuzi!
Tujiulize...hivi kada wa CHADEMA angepanda na silaha jukwaani kama akina Aden Rage angechukuliwa hatua ipi? Hivi ni kwanini makada wa CHADEMA walipekuliwa kama wana silaha na kupelekwa polisi wakati wenyewe ndiyo waliovamiwa na kurushiwa risasi na makada wa CCM? jiulize wabunge/makada wangapi wa CHADEMA wamekamatwa, wamewekwa ndani na kufunguliwa mashtaka tangia mwaka huu umeanza?
Mimi nadhani kuna mpango maalumu wa kuidhibiti CHADEMA kwa kutumia njio zozote zinazowezekana kama vile kutumia vyombo vya ulinzi na usalama wa taifa, dini nk
Kwa hiyo bila kukomaa na kuhamasishana wenye kwenye haya mauaji hatutafika popote.!
Ngoja nikatafute maandamano ya kupinga dowans , sijui yapo?
 
watu wanakufa ili mmoja awe Mbunge apate mshahara na aitwe mhemiwa watoto wake na familia yake iishi kwa fahari na amani. ikumbukwe siku za kuishi hapa duniani ni chache sana. Kafumu umepata ubunge kwa damu za wasio na hatia.
 
Hakika dr. Kafumu hataapishwa kuwa mbunge, kabla roho zilizodhulumiwa kusema! Hakika mungu yupo na atajibu, siku si nyingi.
 
Hicho walichokifanya Ccm ni genocide, watu ambao wanahusika na wenye hatia kwenye mauaji hayo ni viongozi wote wa juu
wa Ccm pamoja na mgombea ubunge kupitia Ccm walioshiriki huko Igunga. Ripoti ya mauaji hayo ipelekwe kwenye mahakama
ya Dunia pamoja na umoja wa mataifa, kuashiria kwamba hapa Tanzania sheria imekaliwa na Serikali ya Ccm na hivyo haki haita-
tendeka, ni kitu cha ajabu kulazimisha ubunge kwa kumwaga damu, ilo Watanzania atulikubali na tunalipinga kwa nguvu zote.
 
Wana Igunga poleni saana na je hao waliowekwa ndani bila sababu bado hawajaachiwa ?????????? Au wanasubiri kuwauwa na kuwatupa porini pia!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mama yangu watu hawa hawana hata huruma ya chembe naomba wanaoyajua wayaanike
 
Roho za marehemu hazitapumzika kwa amani kwa sisi kuziombea bali kwa sisi kuhakikisha wale waliozondoa roho hizo wanatiwa nguvuni na kuadhbiwa vikali. Zitapumzika kwa amani kama tutafanikiwa kuuvunjavunja mfumo wenye kutengeneza, kulinda, na kuficha wauaji wa aina hii.
 
Nahisi mwili unawaka moto kama nimepakwa pilipili, hi inashangaza sana! Ee Mungu epusha maafa kwa wanataifa hili.
 
For the Igunga Political massacre of that degree, I have a well-founded fear that a 'CRIME AGAINST HUMANITY' may well have been committed in the darkness. For certainity on this, some more competent players are highly inevitable to quil the air once and for all about the whole scenario.

We are very well drawing closer to that all-determining focal-point anyway.

 
Hakuna malefu yasio na ncha Nape na vijana wake watalipa damu za hao watu,ahadi yake aliyoitoa tumeiona I HATE ALL CCM MEMBERS.
 
Crimes against humanity

Crimes against humanity, as defined by the Rome Statute of the International Criminal Court Explanatory Memorandum, "are particularly odious offenses in that they constitute a serious attack on human dignity or grave humiliation or a degradation of one or more human beings.

They are not isolated or sporadic events, but are part either of a government policy (although the perpetrators need not identify themselves with this policy) or of a wide practice of atrocities tolerated or condoned by a government or a de facto authority. Murder; extermination; torture; rape; political, racial, or religious persecution and other inhumane acts reach the threshold of crimes against humanity only if they are part of a widespread or systematic practice.

Isolated inhumane acts of this nature may constitute grave infringements of human rights, or depending on the circumstances, war crimes, but may fall short of falling into the category of crimes under discussion."

Source:
http://en.wikipedia.org/wiki/Crimes_against_humanity

HOJA YANGU


Baada ya kusoma maana ya 'KOSA DHIDI YA UTU WA BINADAMU' kama ilivyofafanuliwa na mwongozo wa kisheria wa Mahakama ya Kimataifa wa Umoja wa Mataifa, sasa ni vema tukajaribu kuakisia yale yaliotokea Arusha, Mbarali na hivi sasa Igunga na tuone kama ni vipi huko.

Ndio, huu ndio wakati muafaka wa watu wachache tu kusimama katika jamii yetu hii iliojazwa woga wa kila aina na ukasimamia ukweli hata darini bila ajizi. Hadi hapo mtu huhitaji kutumia nguvu kupigana bali zaidi ni kutumia akili zaidi kutuliza kisheria wauaji wa leo wakawa kama tembe ya piriton mfukoni.

Ni kweli Mungu atatoa jibu zito la kuabisha mno katika mpango mzima wa mauaji haya ya kisiasa, lakini ni sharti kila mmoja wetu tujishungulishe - hawa wadhalimu hivi sasa wanatamani ardhi ipasuke iwameze wakiwa hai maana wanaelewa fika haya ninayoyaandika humu na makucha yake yote.

Jamani tusiishie tu kwenye kupiga tu kelele, juhudi zinazokubalika pia zionekane hapa. Wa-Tanzani tusijihisi wanyonge mbele ya Mafisadi.

Enyi wanaharakati wenzangu popote pale mlipo, hawa marehemu wetu wamekufa wakiwa wanalilia HAKI!! Wenye utaalam mbalimbali tuanze na kile tulicho nacho mikononi hadi sasa kuona kama kweli KOSA DHIDI YA UTU WA BINADAMU halijatendeka Igunga na kwingineko nchini hadi sasa.

Kwa uweza mkubwa sana wa Mwenyezi Mungu, kazi kubwa mno ilishafanyika Igunga kukusanya taarifa muhimu mno na wanaharakati waliojitolea na bado kazi inaendelea. Chonde, usikubali kuwadhulumu marehemu hawa kukalia taarifa muhimu pindi kunapo haja; hiyo ndio haki na heshima pekee tunayoweza kuwatendea marehemu wetu hawa na vizazi vyao na wala si vinginevyo.

Kila mmoja acheze nafasi yake vizuri BILA KUSUBIRI kusukumwa na mwingine katika hili. Ujue tangu sasa kwamba mbali na sheria za nchi yetu ambayo wengi tu wako juu yake, tusishangae kuona hata yule usiyemdhania AKILAZIMIKA kuchukua nafasi yake mwenyewe kizimbani kuji maswali magumu sana.

Natambua kwamba kuna usemi wa ki-Nigeria unaosema hata huo mdomo wa Mfalme umuonao mbele yako nao ulinyonya ziwa la mama!! Maana hapo ni kwa huwa kunafika mahala, ikibidi, mfalme kuwa sawa tu na wengine.

Tafakari sana kwamba leo hii Wa-Tanzania wameuaua kinyama Igunga na kudaiwa KUZIKWA KWENYE KABURI LA PAMOJA huko ma-porini, tukiyanyamazia tu bila kuchukua hatua za kisheria nje kabisa ya mamlaka zinazoonekana kutuhumiwa hivi sasa je huko kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 Wa-Tanzania tutarajie nini??

Kama ulikosa kusoma tahadhari za Mwandishi wa habari, Maggid Mjengwa hivi majuzi basi katafute hicho kijipande cha gazeti na akasome taratibu mwisho ukajiulize; Ni nani kati yetu wapenda mabadiliko ambaye yuko salama na mauaji kama haya??????????

Play your part today. Uwezo Tunao sisi wenyewe hapa.
 
Napinga wazo la CHADEMA nayo kufuga Militia Group kama hii GREENGUARD MUNGIKI ya CCM maana tukifanya hivyo basi na sisi tutakua tumeingia mkondo ule ule siasa za mauaji.

Umma inatutosha wakati wote na wala hakuna haja ya kulea kikundi cha wahuni ambao mwisho wa siku huenda ukashindikana kumdhibiti.
 

Serikali ya umoja wa kitaifa inawatosha sana nyie au siyo?

Si ni sawa tu cuf walipoua tukaunda serikali ya mseto?

Nasubiri kwa hamu sherehe ya serikali ya mseto (NDOA)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…